Rais Samia ni kiongozi pekee mpaka sasa aliyefanikiwa kupata uungwaji mkono na kukubalika na makundi yote na vyama vyote

Rais Samia ni kiongozi pekee mpaka sasa aliyefanikiwa kupata uungwaji mkono na kukubalika na makundi yote na vyama vyote

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Ni historia ambayo Rais Samia amejiandikia na kujiwekea kwa kufanikiwa kupata uungwaji na kukubalika na makundi yote na vyama vyote, hii Ni kutokana na Imani kubwa ambayo watu wamejenga na kuwa Nayo juu ya Rais Samia,

Hakuna mtu au kundi ambalo Ni tishio katika uongozi wa Rais Samia, kwa kuwa watu wote na makundi yote Yana matumaini na Imani na Rais Samia kuhusu madai yao, vyama vya siasa vina matumaini na Imani na Rais Samia Ndio sababu unaona vikiwa tayari kukaa Naye katika meza ya mazungumzo na hata kupanda jukwaa moja na Rais Samia Kama tulivyoona katika ziara yake ambayo wapinzani wamejitokeza kumuunga mkono mh Rais na kuhubiri habari za maendeleo na umoja wa kitaifa na kutanguliza mbele maslahi ya kitaifa

Hali hii imeleta umoja wa kitaifa na kuleta mshikamano na Sasa tunabishana na kupambana kwa hoja tu ya namna ya kuijenga nchi yetu na njia za kupita kupata maendeleo, hii Ni kutokana na kuwa nais Samia Ni mama mwenye dhamira njema na mwaminifu Sana katika kauli zake, Ni mama na kiongozi anayezungumza kilicho katika moyo na kifua chake.

Rais Samia ameonyesha kuwa na dhamira njema katika kulitumikia Taifa hili, Ni kiongozi ambaye ameonyesha kuumizwa Sana na matatizo ya watu, Ni kiongozi anayetamani kila Siku Taifa letu linakuwa kiuchumi na watanzania tunaondokana na Hali ya umaskini na kwamba kila Siku watanzania tunafanikiwa kupata Milo mitatu mezani petu,

Kila mtanzania anamatumaini kuwa kesho yake itakuwa njema na kila mtu anajiona kuwa anaweza pata fursa ya kiuchumi bila kujarisha Hali yake.

Serikali ya Rais Samia imejikita katika kusaidia watu na siyo kuwaumiza watu, serikali ya mama Samia imejikita katika kumtafutia mtanzania fursa za kiuchumi na siyo kuwa kizuizi katika fursa za kiuchumi, Rais Samia amejikita katika kuona kila siku watanzania tunaaamka na kupata Tabasamu jipya na siyo kuishi kwa kukosa matumaini.

Rais Samia anataka kuona kuwa kila mtu anafaidika na jasho lake na juhudi zake katika kujitafutia na kujikwamua kiuchumi, ndio sababu anajitahidi kuweka mazingira mazuri ya kumuwezesha kila mtu mahali anapojishughulisha na kazi anafaidika na kuinuka kiuchumi kupitia mikono yake na ubunifu wake

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Ndugu zangu Ni historia ambayo Rais Samia amejiandikia na kujiwekea kwa kufanikiwa kupata uungwaji na kukubalika na makundi yote na vyama vyote, hii Ni kutokana na Imani kubwa ambayo watu wamejenga na kuwa Nayo juu ya Rais Samia,
Mkuu una takwim zzt zile znazoensha mama anakubalik na vyama vyote
 
Ndugu zangu Ni historia ambayo Rais Samia amejiandikia na kujiwekea kwa kufanikiwa kupata uungwaji na kukubalika na makundi yote na vyama vyote, hii Ni kutokana na Imani kubwa ambayo watu wamejenga na kuwa Nayo juu ya Rais Samia...
Hizo propaganda zenu zina chosha, na za kishamba achieni vyama vya siasa ndo mtajua uhalisia wa watu.
 
Ndio Nina ushahidi huo, angalia katika ziara aliyoifanya huko kigoma, angalia kauli za akina Mbowe namna ambavyo wamekuwa wakimzungumzia Rais Samia katika namna ya kumuunga mkono, viongozi mbalimbali wa kisiasa wameonyesha wazi wazi kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa
Mkuu una takwim zzt zile znazoensha mama anakubalik na vyama vyote
 
Ndio Nina ushahidi huo, angalia katika ziara aliyoifanya huko kigoma, angalia kauli za akina Mbowe namna ambavyo wamekuwa wakimzungumzia Rais Samia katika namna ya kumuunga mkono, viongozi mbalimbali wa kisiasa wameonyesha wazi wazi kumuunga mkono mh Rais wetu mpendwa
Tanzania tuna vyama kama 20+ ss unasem vp vyama pinzan vinamuunga mkon wkt waliongea n wawil tu zitto na mbowe...

eb nipe takwim mzee
 
Naona umasikini wako wa kipato na akili umekufanya kumgeuza binadamu mwenzio "mungu-mtu".

Mtu mwenye utimamu wa akili kamwe hawezi kuwa muabudu mtu badala ya mfumo.
Hapana mkuu Mimi ninaeleza na kutoa mtizamo wangu juu ya kinachoendelea huku mtaani, lakinipia ushujaa siyo kupinga kila kitu, penye ukweli na mazuri Ni uungwana kupongeza na kuunga mkono, unaweza ukakubaliana na Sera na ukapingana na njia za utekelezaji wa Sera, lakini siyo unapinga Sera Hadi namna ya utekelezaji wake hata Kama machoni pa watu inaonekana Sera Ni nzuri
 
Naona ana dhamira nzuri Samia, Katiba inampa nguvu za kuwa Dikteta wa hatari kabisa, lakini ameamua kuibadilisha😍😍

Hii ni dhamira nzuri sana.
 
Tanzania tuna vyama kama 20+ ss unasem vp vyama pinzan vinamuunga mkon wkt waliongea n wawil tu zitto na mbowe...

eb nipe takwim mzee
Angalia vyama vyenye wanachama na wakereketwa wengi mitaani, achana na vyama ambavyo unakuta havijawahi kupeleka hata mbunge mmoja bungeni au hata kufahamika tu uongozi na viongozi wake kwa watanzania, Kuna vyama vinafahamika kwa msajili tu wa vyama vya siasa vilipokwebda kupata usajili
 
basi mkuu ukwel ni kwamba huku mtaan raia hawamuelw bi mkubwa ...km unabisha ingia ww mwnyw mtaan ufanye taft acha nadharia mkuu
 
Ndugu yangu Lucas,

Hizi sifa bandia mnazombandika Rais wetu ni kumkosea yeye na Mungu pia.

Rais anapaswa kufahamu kuwa anaangushwa na wasaidizi wake ambao mwenendo wao ni kama kuna mkakati wa kusababishia anguko kubwa la kisiasa mbeleni.

Rais aambiwe ukweli kwamba hao wanancgi wanaokusanywa kila anapokatiza hukusanywa kutoka kwenye matawi ya CCM kwa malori na usafiri mwingine hivyo wanamhadaa kuwa anungwa mkono huku wananchi wakiendelea kunung'unikia utawala wake kama chanzo cha anguko la kouchumi na kuleta hali ngumu ya maisha.

Anao muda wa kurekebisha na kuondokana na nyie wapigadebe ili ajikite kwenye kuukabili ukweli kwa nia ya kufanya mambo yenye tija.
 
Ndugu yangu Ni ui
Ila hili jamaa linapenda kusifia! Hivi usikute lipo kwenye pay roll ya Chongolo eti.
Ndugu yangu Ni uungwana na Jambo la Afya kupongeza pale mtu anapofanya vizuri ili kumpa nguvu ya kufanya vyema zaidi, hii ndio sababu hata ya kuanzishwa kwa tuzo mbalimbali Duniani Kama sehemu ya kutoa hamasa kwa watu wanaoonekana kujitoa na kujitolea katika kuwatumikia watu na kuleta matumaini
 
Pamoja na inflation ila Mheshimiwa tumekuona kwenye ajira mpya.
 
Mimi nimeona na kushuhudia kabisa namna watu wanavyokwenda kumsikiliza Rais kwa hiyari yao kabisa inayochagizwa na upendo mkubwa walio nayo kwa mama samia, lakini pia napenda nikutaarifu tu kuwa Kama mtu hakupendi na hakukubali watu wasingeweza kwenda kumsikiliza hata Kama wangeletewa gari la bure milangoni mwao.

Hivyo mafuriko yanayojitokeza kumlaki na kumpokea mh Rais wetu ni ushahidi wa namna anavyokubalika na kupendwa na watanzania, ndio sababu watu wanakuwa tayari kusafiri umbali mrefu kwenda kumpokea mh Rais
 
Pamoja na inflation ila Mheshimiwa tumekuona kwenye ajira mpya.
Hata suala la mfumuko wa Bei mh Rais amejitahidi Sana kukabiliana nalo Kama tulivyoona katika mbolea ambapo baada ya kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini kwa Sasa mbolea inapatikana kwa nusu Bei ukilinganisha na msimu uliopita,
 
Tanzania Low IQ hata propaganda zao very simple, usikute huyu kama kaajiriwa kabisa kufanya propaganda na analipwa!
Tanzania Low IQ hata propaganda zao very simple, usikute huyu kama kaajiriwa kabisa kufanya propaganda na analipwa!
Hapana Mimi silipwi kitu Wala na mtu yoyote Yule Bali Ni Upendo wangu kwa mh Rais unaotokana na kuridhishwa na kuvutiwa na utendaji kazi wake uliotukuka uliogusa maisha yetu watanzania kila mtu kwa eneo lake, Hakuna aliyeachwa nyuma na juhudi za Rais, Hakuna aloyetengwa katika ujenzi wa Taifa letu Wala Hakuna aliyepuuzwa katika mawazo yenye lengo la kujenga Taifa letu, kila mtu ana nafasi katika Taifa letu
 
Back
Top Bottom