Katiba ya sasa ina mapungufu mengi. Kwa mfano, inampa madaraka makubwa sana rais, ina vipengele vingi vinavyotoa haki na vingine kama zinachukua haki hizo na kujipinga.
Lakini, kimsingi, inatoa haki nyingi za kibinadamu zinazotokana na Universal Declaration of Human Rights. Kwa mfano, kama haki za watu kukutana (freedom of assembly). Haki hizi, ambazo ni za kikatiba na kibinadamu, zilivunjwa na rais Magufuli alipokataza mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Magufuli alivunja katiba waziwazi, hii hii tuliyo nayo sasa.
Na kwa sababu nchi yetu haina utamaduni mzuri sana wa kuheshimu katiba, Magufuli hakuwajibishwa.
Kwa hivyo, point yako ina mantiki, kwamba, hata mazuri ya katiba hii ya sasa tunaweza tusiyatumie, kwa sababu, hatuna utamaduni wa kuheshimu katiba. Tuna utamaduni wa kuendeshwa kwa amri kutoka juu.
Ndipo hapo habari ya katiba ni kijitabu tu inapokuwa na mantiki.