Dr. Faustine Ndugulile ameondoka katika kipindi ambacho alitazamiwa kuwa mkuu wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika. Ametuachia majonzi makubwa sana! Sasa tunatamani mtu mwingine achukue nafasi yake.
Kwa bahati mbaya kila mtu siku hizi anaamini fedha na siasa ndio inampa mtu haki au sifa za kuwa kiongozi!
Lakini napenda kusema kuwa ni vizuri watanzania wenye uwezo na weledi katika nyanja mbalimbali wakapatiwa nafasi ya kujulikana na kung'aa kulingana na umahiri wao. Na kama kuna nafasi zozote za uteuzi au uchaguzi, basi mng'ao wao utaonekana na kuwafanya wachaguliwe au kuteuliwa.
Tuachane na huu mtindo ulioingia wa kutumia nguvu nyingi kung'arisha watu hata wale wasioweza kung'aa.
Ninaomba sana Tanzania isitumie nguvu kubwa ya kisiasa na fedha kufanya kampeni ili watanzania wachaguliwe kwenye nafasi mbalimbali ndani na nje ya nchi. Tujitahidi kuinua elimu yetu na professionalism yetu kwani kwa jinsi mambo yalivyo sasa inahitaji kutumia siasa na fedha nyingi mno kumpata mtu mwenye "weledi" wa kimataifa au hata kitaifa.
Tuweke nguvu zetu na fedha zetu kwenye mambo muhimu ya taifa letu kama vile maji, umeme, huduma za afya, elimu na uchumi.