Rais Samia: Nia yako njema ya uchunguzi mauaji ya kibao lakini ninashauri iundwe tume huru kuchunguza na sio Polisi

Glenn

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2015
Posts
69,329
Reaction score
164,730
Nchi imejawa na simanzi kwa mauaji ya kikatili. Kitendi kiovu kilichopindukia mauaji haya ni muendekezo wa vitendo vya kikatili, utekaji na kupotezana.

Imesimuliwa kuwa mzee Kibao alitekwa hivi karibuni ajishushwa ndani ya basi na watu wenye silaha wakijitambulisha ni askari polisi tena wakiwa na pingu.

Baada ya utekaji huu, katibu wa CHADEMA John Mnyika alipaza sauti kuwa mmoja kiongozi wao ametekwa.

Polisi kana kawaida yao walijitokeza kutoa kauli kama tulivyowazoea. Leo hii nchi imepigwa butwa kwa kutaarifiwa kuwa mzee Kibao ameokotwa akiwa mfu.

Sakata hili limenuibua Mwenezi wa ccm kukemea, kutoa pole na kutoa wito kwa polisi kufiatilia.

Mbali na Makalla, Rais Samia naye amekemea na kutoa pole na wito kwa Polisi kumpa taarifa yamauaji haya.

Ni jambo jema Rais kuagiza hivyo lakini; Je polisi watatia taarifa sahihi?

Je kwanini hata kitendo cha uchunguzi leo hospitalini hawakutaka mawakili washiriki?

Soma Pia:
Ninashauri iundwe tume huru kuchunguza na sio polisi
 
Angalia Glenn usijeangukiwa na jumba bovu. Mimi usiku huu naondoka kwenda mkoani. Jumba bovu loading to someone.
 
Nchi imejawa na simanzi kwa mauaji ya kikatili. Kitendi kiovu kilichopindukia mauaji haya ni muendekezo wa vitendo vya kikatili, utekaji na kupotezana.

Imesimuliwa kuwa mzee Kibao alitekwa hivi karibuni ajishushwa ndani ya basi na watu wenye silaha wakijitambulisha ni askari polisi tena wakiwa na pingu.

Baada ya utekaji huu, katibu wa CHADEMA John Mnyika alipaza sauti kuwa mmoja kiongozi wao ametekwa.

Polisi kana kawaida yao walijitokeza kutoa kauli kama tulivyowazoea. Leo hii nchi imepigwa butwa kwa kutaarifiwa kuwa mzee Kibao ameokotwa akiwa mfu.

Sakata hili limenuibua Mwenezi wa ccm kukemea, kutoa pole na kutoa wito kwa polisi kufiatilia.

Mbali na Makalla, Rais Samia naye amekemea na kutoa pole na wito kwa Polisi kumpa taarifa yamauaji haya.

Ni jambo jema Rais kuagiza hivyo lakini; Je polisi ambao ni watuhumiwa watatia taarifa sahihi?

Je kwanini hata kitendo cha uchunguzi leo hospitalini hawakutaka mawakili washiriki?

Soma Pia:
Ninashauri iundwe tume huru kuchunguza na sio polisi
Mtuhumiwa hawezi kujichunguza. Kama kweli hawahusiki waruhusu uchunguzi huru na baadae iundwe Tume ya Haki Jinai.
 
Polisi wa Tanzania hawaaminiki tena kiukweli.
 
imagine mtu anakamatwa kwenye basi, yupo safarini, anafungwa pingu, na anauawa. kwahiyo siku hizi ukiona mtu anajitambulisha polisi na anataka kukuarrest, pambana hadi kufa manake hata usipopambana kufa utakufa tu, au wanataka wananchi wafanye nini.
 
Abiria wameinyesha unyinge sana
 
watanzania wanaheshimu sana sheria, wanaheshimu polisi, ndio maana polisi anaweza kuingia tu kwenye basi, akasimamisha basi na kusema anamkamata mtu, anamfunga pingu, anaondoka naye. kama yeye mwanaume, si amuulie pale pale kwenye basi, kwanini wanaondoka naye wakamuulie huko yeye akiwa peke yake wananchi wapo mbali? waoga tu hao. damu ya mtu haijawahi kwenda bure, awe na dhambi asiwe na dhambi kama imemwagwa bila hatia, huwa inalia ardhini na kushitaki kwa Mungu.
 
Polisi wa Tanzania hawaaminiki tena kiukweli.
Ni ushuhuda wa kweli, kuna polisi alikuwa dereva amestaafu kabla ya muda wake wa kustaafu...
Anasimulia inatisha kuwa gari yake ilikuwa inatumiwa na kikosi maalum cha mauaji tena matukio mengine ni unyang'anyi wa nguvu.

Alinionyesha mmoja wa polisi kijana kuwa ndiye kinara wa kuua na anekolea damu za watu
 
imagine mtu anakamatwa kwenye basi, yupo safarini, anafungwa pingu, na anauawa. kwahiyo siku hizi ukiona mtu anajitambulisha polisi na anataka kukuarrest, pambana hadi kufa manake hata usipopambana kufa utakufa tu, au wanataka wananchi wafanye nini.
sasa hv inaonekana polisi si mahala salama tena ni heri wakuulie hapo hapo hadharani tu
 
Serikali zinazokandamiza na kupora haki za watu ndizo zinazoweka sheria kali za umiliki wa silaha ili ziendelee kunyanyasa watu. Ingekuwa Marekani mtu hao washenzi wangekula chuma. Watu wanatembea na bunduki kwenye gari. Sasa wewe jichanganye utake kumkamata mtu kinyume cha sheria uone kitakachokupata.
 
Auwae kwa upanga, naye atakufa kwa upanga pia.
 
Back
Top Bottom