Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi wa Tanzania na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka leo tarehe 27 Mei, 2023 Fumba - Zanzibar.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora George Simbachawene amesema Historia ya Kada hizo itamkumbuka Rais Samia kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuzipigania.
Waziri Simbachawene amewapongeza kwa kazi kubwa wanayofanya ambapo amesema Wateule wengi wa nyadhifa mbalimbali za kiserikali huingia kwenye ofisi zao bila ujuzi mkubwa wa kazi zao, lakini watunza kumbukumbu na secretaries ndio husaidia kuwafundisha kazi.
Amesema kundi hili la watunza kumbukumbu, Siri na Taarifa za Serikali ni watu Muhimu kwa kulinda Uhai na Usalama wa Watumishi wa Umma na Serikali kwa Ujumla hivyo wanapaswa kuheshimiwa.
Amekubaliana na kauli mbiu ya mwaka huu inayosisitiza Nidhamu, Uadilifu na Utunzaji Siri kwa kusisitiza kuwa nidhamu na Uadilifu huzaa ufanisi wa kazi kwa kukamilisha kazi inavyotakiwa, kwa kiwango kinachotakiwa na wakati unaotakiwa. Mambo haya pia ni chachu ya kuleta maendeleo kwa mtu binafsi na Taifa.
Kuhusu uwepo wa changamoto ya baadhi ya waajiri Kutotoa ruhusa kwa watu wa kada hizo kuhudhuria mafunzo na vikao vyao, Rais Samia amewataka Mawaziri wanaohusika na mambo hayo kukutana na Waajiri hao na kuzungumza ili kuondoa changamoto hiyo.
Rais Samia amewaasa wanataaluma hao Kuzingatia weledi kwa kushirikiana katika kutekeleza majukumu yao, wazingatie miongozo na mipaka ya kiutendaji. Waende kuishi kiapo chao cha uaminifu.
Shamrashamra za Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka wakati wa kilele cha Mkutano wao wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye viwanja vya Fumba kwa ajili ya kushiriki Kikao maalum cha Makatibu Mahsusi pamoja na Watunza Kumbukumbu na Nyaraka kabla ya kufunga Mkutano wa Kitaaluma wa Chama cha Makatibu Mahsusi Tanzania (TAPSEA) pamoja na Menejimenti ya Watunza Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA) uliofanyika katika Viwanja vya Fumba Zanzibar tarehe 27 Mei, 2023
Akizungumza kama Mgeni Rasmi kwenye Mkutano huo, Rais Samia amesema Safari yake ya kiuongozi ilianzia kama Mtunza kumbukumbu ndio maana tangu aingie madarakani amekuwa analikumbuka kundi hili lililokuwa limesahaulika.