Rais Samia: Nilimwondoa Kidata TRA sababu niliona mwishoni atadata

Mkuu huna kitu,nyosha maelezo vinginevyo watakuita akina pangu pakavu weka mchuzi.

Mwl.Nyerere pamoja na mambo mengi ya kuikomboa Africa lakini alitugeuza watu baki kisa English communications language. Akijua knowledge is power,
Wabongo wako vizuri lakini hawafahamiki kimataifa.
Ila watoto wao .......
mambo mengi huwa sikubaliani na Nyerere
 
Mwambieni mama apunguze matumizi serikalini, vinginevyo kuna bomb litalipuka.Achukue hatua kabla,mwenzake Ruto kaanza kupunguza.Hali mbaya mtaani
Hiyo ndo point ya msingi ..huyu mama amekuja kuongeza matumizi ya serikali wanaoumia ni sis walipackodi
 
Anawaaminisha wajinga kwamba Kariako ni sehemu muhimu sana kwa uchumi wa nchi, umuhimu upi wakati asilimia 100 products ni za nje tena lower qualities
Hiyo kodi si aichukue huko bandarini aacha kuwwpa wwtu mianya ya rushwa ya kutembea kukagua risit
 
Lipo kundi la Watoto wa Mjini la Amos Makala na Dr Nchimbi na wenzao bila shaka na Rais akiwemo na limetangazwa hadharani.

Je mama leo alikuwa anamsajili Kamishina Mkuu wa TRA kwenye kundi hilo kwa kumuita mtoto wa mjini?
Hakuna cha mtoto wa mjini wala nn hapo ni upumbavu ndio unaonekana.
 
Amemuelezea Kidata kama Mkuu wa TRA mwenye msimamo imara sana.Akasema hata wao viongozi hawakumpenda kwa sababu wakitaka bidhaa fulani isilipiwe ushuru yeye alikuwa anaweka ngumu.
Kwa namna alivyomuelezea,Kidata ndiyo anafaa kama anataka makusanyo yaongezeke.
 
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amemuondoa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Alphayo Kidata kwenye nafasi yake kwakuwa aliona atadata kwa jinsi anavyoandamwa lakini amekiri kuwa TRA chini ya Kidata imefanya vizuri na kuongeza mapato hadi kufikia Tsh. trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa 97.67% ya lengo la kukusanya Tsh. trilioni 28.30 katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2023/24 ambalo ni ongezeko la 14.50% ikilinganishwa na makusanyo ya Tsh. trilioni 24.14 katika Mwaka wa Fedha uliopita, 2022/23.

Akiongea leo July 05,2024, Ikulu ya Tunguu, Zanzibar wakati akiwaapisha Viongozi Wateule, Rais Samia amesema “Yusuph Mwenda kwanza hongera kwa kazi nzuri uliyofanya Zanzibar, tunakupeleka TRA (kuwa Kamishna mpya), TRA chini ya Kidata imefanya vizuri sana, mapato yamekua sana, sitegemei kama utashuka, kwanini nimemuondoa Kidata?, Kidata nimemuondoa niliona mwisho atadata, kazi kafanya nzuri sana lakini niliona atadata jinsi anavyoandamwa , sasa nakupeleka wewe Kijana wa Dar es salaam
Mtoto wa Mjini, uhuni wote ulioko TRA kule umefanywa na wewe ukiwa mulemule pengine uli-participate”

“Mipango yote mule ya kupenya, ya kufanyaje na Bandari mnatoa wapi mnapenyeza wapi unaijua Yusuph nenda kaizibe, nenda kaizibe, tunachohitaji ni mapato, tunachohitaji ni kupungua kukopa, tunakopa tunajichetua kila anayekuja akija European Bank yes yes, akija huyu Yes, World Bank wanatunyanyasa tumo tu, nini?, tuna miradi ya maendeleo inataka pesa, pesa hatuna tunakopa, tunakopa tunanyanyasika, je tukiwaomba itakuwaje?, kwahiyo twende tukanyanyue za kwetu”

“Serikali imefanya yote, tumeweka mazingira mazuri ya kufanya biashara, mazingira mazuri ya kufanya uwekezaji, Wawekezaji wanakuja, biashara zinafanyika kodi hazilipwi, Kariakoo pale tatizo ni kulipa kodi ukienda leo wanakuambia hiki kesho wanakuambia hiki, Kariakoo pekee yake kuna mapato kama yatakusanywa vizuri kwa mwaka yanaendesha Wizara tatu lakini hamkusanyi kuingia Serikalini, inawezekana mnakusanya kuingia mfukoni lakini hamkusanyi kuingiza Serikalini nenda kazibe hilo”

“Mwenda unaijua vizuri TRA ulikuwa sijui Mkurugenzi wa kodi zipi lakini ulikuwa unajua mnaibia vipi na wenzio kwahiyo yale mliokuwa mkiiba vichochoro vile nenda kazibe tunahitaji fedha, nimekuamini na najua utakwenda kufanya kazi”

#MillardAyoUPDATES

NB: Kiukweli 2025 tugangamale vingine tutakuja kuwa Zimbambwe iliyochangamka.
Ingekuwa mataifa mengine Kwa hotuba hiyo ya raisi wangesha andamana
 
Ila samia anachekesha, Kwa hiyo amemteua mwizi akazibe milango ya wizi?
 
Back
Top Bottom