Maneno Meier
JF-Expert Member
- May 12, 2013
- 2,467
- 1,697
Asante sana Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu mpendwa, kwa msimamo wako thabiti ulio tuonyesha tarehe 28 mwezi Desemba mwaka 2021 huko IKULU Magogoni wakati wa kushuhudia kutia saini mkataba wa kuendeleza SGR yetu kipande cha tatu kati ya Makutupora Singinda na Tabora.
Kusema kweli, hotuba yako uliyo itoa siku ile ya kutia saini imewafanya watanzania wengi wawe na matumani makubwa sana na wewe. Ilikuwa hotuba nzuri sana na iliyo jaa faraja, furaha na msisimko mkubwa kwetu. Watanzania tumefurahishwa sana na hotuba ile. Kwa dhamira ulizo zitoa na ahadi uliyo wapa watanzania kwenye hotuba yako, naona imani na matumaini makubwa yamerejea tena kwa watanzania. Watanzania wanakuona sasa uko nao pamoja. Hivyo ndivyo tunavyo taka viongozi wetu wawe.
Watanzania wanataka kuona viongozi wenye msimamo kama wako, japo kuwa kuna baadhi ya watu kama akina Tundu Lissu ambao siku kama ya juzi tarehe 31.12.2021 anatoa hotuba yake ya kufunga mwaka kwa madhumuni ya kukuvunja moyo wewe na watanzania kwa ujumla. Ni absurd!
Huyu jamaa mimi namwona bado hajitambui na inaelekea aidha amepitwa na wakati au ni limbukeni wa wazungu. Ina maana yeye hivi vita vya maendeleo ya uchumi ambavyo vinatokea kwenye karne yetu hii ya 21 duniani, havioni wala kusikia? Demokrasia na haki gani za binabadam anazo zipigania yeye wakati ulimwengu mzima umejawa na predators?
Inasikitisha sana na ni haibu kubwa kuona mtanzania aliyebobea kisheria na kuiva kisiasa na kiitikadi kama yeye kuweza kuwa zuzu na kukubali kutumiwa na wazungu. Nani anafanya vitu kama hivyo ulimwengu huu wa leo? Jamaa nahisi kakamatwa pabaya sana na wazungu wake mpaka nina mwonea huruma. Ni kweli kwamba huyu mtu ana akili timamu? Maana naona matendo anayo yafanya ni kama ya mtoto wa darasa la tatu vile!
Wito wangu kwako Mama yetu, ningekuomba kwa heshima kubwa hawa watu kuwapuuzia na wala usihangaike kuwasikiliza. Achana nao kabisa kabisa. Na wala usitishike na vitendo vya mabwana zao EU, England na Amerika. Wana nini cha ku-offer? Hawana kitu. Hizi nchi nikuambie Rais wangu haziwezi kufanya chochote. Wachina wamekwisha wamaliza kiuchumi kwa ujinga wao. Hivi sasa wana haha tu na kujaribu kuyatisha mataifa mengine kivita na hasa China. Wathubutu basi kuanzisha vita dhidi ya mchina, nafikiri huo ndiyo utakuwa mwisho wa existence yao. Wanashindwa na nchi masikini kama Afghanistan na Iran sembuse China? Wafie mbali huko!
Nikirudi kwenye mada yangu, kitu ambacho ningependa kukiongeza ni kwamba, pamoja na mipango yote hii ambayo serikali yako imekususdia kuikamilisha, nakuomba chonde chonde Mama yangu jaribu sana kutilia mkazo kwenye madini yetu ya Helium. Mama kama utakuwa hujui au pengine washauri wako hawaja kushauri vizuri, basi ningekuomba fanya haraka sana upate taarifa muhimu juu ya madini haya ya Helium.
Hivi sasa ulimwengu una uhaba mkubwa sana wa haya madini ya Helium. Wataalam na makampuni yanayo tegemea madini ya Helium katika kufanya utafiti na alikadhalika uzalishaji wa mitambo inayo tumia Helium gas , kama MRT/MRI wanaumiza vichwa hivi sasa jinsi ya kupata solution juu ya upatikanaji wa hii inert gas Helium. Tanzania kwa hivi sasa imekuwa ni tegemeo kubwa sana la hii gas duniani, kwani wataalam wanasema deposit ya hii gas iliyogunduliwa nchini ni Cubic meter za ujazo trilioni 1.5, ambayo ni sawa na mara saba ya mahitaji ya dunia kwa mwaka. Mahitaji ya dunia kwa mwaka ni Cubic meter za ujazo trilioni 0.22. Ujazo huu, kwa maana nyingine, ni kwamba unaweza kutumika kwenye idadi ya utegenezaji wa mitambo ya MRT/MRI milioni 1.2. Katika Research na utengenezaji wa hii mitambo Helium gas is inevitable!
Source: Rettender Fund wendet Heliumkrise ab - Forscher entdecken gigantisches Helium-Reservoir in Tansania - scinexx.de
Kitu kingine ambacho kimetokea katika ugunduzi huu ni kwamba ni kwa mara ya kwanza Helium gas na Nitrogen zimeonekana zikitoka moja kwa moja zenyewe juu kutoka kwenye miamba ya Rift Valley. Na vile vile ni kwamba Helium gas inayotoka ni asilimia kumi ya ujazo wa gases zote zinazo toka chini, hii ni asilimia kubwa sana, na ni kitu ambacho mpaka sasa katika uvunaji wa Helium gas haijawahi kutokea.
Hii ni picha ya baadhi ya mitambo iitwayo MRT / MRI (Magnetic Resonance Tomography)
Hii picha inaonyesha view ya eneo la Rift Valley nchini Tanzania ambako wataalam Kutoka University of Oxford na Kampuni ya Helium One ya Uingereza wamegundua hiyo Helium Gas.
Source: Rettender Fund wendet Heliumkrise ab - Forscher entdecken gigantisches Helium-Reservoir in Tansania - scinexx.de
Hii ni picha ya Mr. Tom Abraham-James kutoka Kampuni ya Helium One ya Uingereza akichukua sample ya Heliumgas kutoka kweye dimbwi ambalo Helium gas inatoka yenyewe kutoka chini ya ardhi karibu na ziwa Eyasi nchiniTanzania.
Source: Rettender Fund wendet Heliumkrise ab - Forscher entdecken gigantisches Helium-Reservoir in Tansania - scinexx.de
Kwa hali hii nashangaa sana Rais wetu Mama Samia unavyo weza lala vizuri usingizi na kukwaruzana na watendaji wako na vile vile hata kujiingiza kwenye maneno kuhusu mikopo au deni letu la Taifa na Spika wa Bunge Mh. Ndugai, badala ya kufuatilia uvunaji wa hii Helium gas yetu iliyo gunduliwa nchini na ambayo kwa sasa ni tegemeo kubwa la Dunia.
Spika wa Bunge Mh. Ndugai hakuwa na nia yoyote ile ya kuku-attack wewe wala serikali unayoiongoza. Itakuwaje aku-attack wewe wakati yeye mwenyewe hiyo mikopo ndiyo aliipitisha Bungeni? It makes no sense! Hiyo ni perception potufu na ya kimasikini tuliyo nayo sisi watanzania kwa njaa na stress zetu za maisha. Na wengine kutaka kujipendekeza kwako. Lengo la Spika mbona liko wazi kwa mtu anaye taka kumwelewa? Yeye na lengo la kuelezea maswala ya tozo na katika jitihada hizo akajikuta anagusia mambo ya mikopo kwa lengo la kusisitiza umuhimu wa sheria ya tozo ambayo Bunge limeipitisha na ambacho, kwa mtazamo wangu, sio kitu kibaya kukizungumzia. Kwani ni siri?
Ni kweli kama nchi itakuwa na deni kubwa la Taifa na kushindwa kulipa, kama majirani zetu wakenya na Zambia ambao wanaweza lazimika ku-default, eh sio kitu cha busara. Kwa rasilimali tulizo nazo kwa kweli hata mimi nashangaa sana kwanini tuendelee kukopa?
Mh. Spika wa Bunge huko nyuma amejaribu sana kuwakumbusha mawaziri kweye sekta nyeti kama za madini na nishati kutumia uwezo wao na madaraka waliyopewa na umma kuchakata madini yetu hasa ya chuma ili yaweze ku-boost uchumi wetu na kuleta ajira kwa vijana wetu. Nina mwelewa vizuri sana anavyosikia uchungu tukiendelea kukopa badala ya kutumia rasilimali zetu.
Mama Samia kulingana na taarifa hii nzuri ya Helium gas ebu jaribu kukaa na watendaji wako ili mjue jinsi gani nchi yetu tunaweza nufaika nayo. Vihimize vyombo vinavyo husika kufanya feasibility study ya haraka haraka tujue faida na hasara tunazo weza pata. Kama faida ni TSH trilioni 10 na uwekezaji ni TSH trilioni tatu, kwa mfano, kwanini sasa tusite kukopa na kuwekeza kwenye uvunaji wa hiyo gas? Kopa tu Mama na tuwekeze haraka ili tuipate hiyo faida ya TSH trilioni saba na kusonga mbele. Usichelewe sana Mama!
Watakao kuchelewesha Mama, naomba usiwe na huruma nao hata kidogo, fukuza tu mama na waweke wengine. Tuna vijana wengi wasomi ambao wana ghadhabu na maendeleo ya nchi yetu.
Naomba kuwasilisha.