Rais Samia: Nimewatia wadhamini timu za Simba SC na Yanga SC

Hapa Kuna rasilimali inauzwa ili tuambiwe ni udhamini wa yanga na simba.
Mwekezaji anakuja kuwekeza kwenye mpira wa yanga na simba au anakuja kuvuna madini na pesa za bandari yetu?
Tusipokaa sawa tunakuwa watumwa
 
Naombeni na mimi nichambue ambacho huwa nakiwaza kuhusu Simba na Yanga.

Mtu yoyote akitaka aione Tanzania ni chungu, basi atake kuzimiliki hizi timu na kuzitenga na chama kile.

Hii ni kwa sababu hizi timu zinatumiwa kuwapunguzia stress za maisha Watanzania, hivyo zinafuatiliwa sana na serikali.

Jiulizeni, GSM kaleta maendeleo pale Yanga lakini anataka kuletewa mdhamini mwingine. Hii ni kwa sababu ya timu kuendelea kuwa karibu na serikali. Huyo mdhamini mpya atakuwa kama spy vile na atakuwa anaripoti moja kwa moja kwa aliyemleta.

Hizi timu hazitamilikiwa na mtu binafsi miaka ya hivi karibuni labda kile chama kiondoke madarakani.

Yaani hata mtu binafsi awe mjanja vipi kutaka kuzimiliki hizi timu kama anavyofanya GSM lakini ipo siku atagundulika tu akitaka kujimilikisha na atapewa zengwe baada ya kugundulika nyendo zake.

Kwa mfano, leo mashabiki wa Yanga wanamfurahia GSM ila siku GSM akigundulika ana njama za kujimilikisha Yanga utaibuliwa mgogoro mpaka mashabiki watashangaa.
 
Kuna ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…