Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuna ukweliNaombeni na mimi nichambue ambacho huwa nakiwaza kuhusu Simba na Yanga.
Mtu yoyote akitaka aione Tanzania ni chungu, basi atake kuzimiliki hizi timu na kuzitenga na chama kile.
Hii ni kwa sababu hizi timu zinatumiwa kuwapunguzia stress za maisha Watanzania, hivyo zinafuatiliwa sana na serikali.
Jiulizeni, GSM kaleta maendeleo pale Yanga lakini anataka kuletewa mdhamini mwingine. Hii ni kwa sababu ya timu kuendelea kuwa karibu na serikali. Huyo mdhamini mpya atakuwa kama spy vile na atakuwa anaripoti moja kwa moja kwa aliyemleta.
Hizi timu hazitamilikiwa na mtu binafsi miaka ya hivi karibuni labda kile chama kiondoke madarakani.
Yaani hata mtu binafsi awe mjanja vipi kutaka kuzimiliki hizi timu kama anavyofanya GSM lakini ipo siku atagundulika tu akitaka kujimilikisha na atapewa zengwe baada ya kugundulika nyendo zake.
Kwa mfano, leo mashabiki wa Yanga wanamfurahia GSM ila siku GSM akigundulika ana njama za kujimilikisha Yanga utaibuliwa mgogoro mpaka mashabiki watashangaa.