Rais Samia: Nitaendeleza mazuri yaliyoanzishwa na Hayati Magufuli

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Leo ikiwa ni kumbukizi ya Hayati Dkt. Joseph Pombe Magufuri, Rais Samia Suluhu amemtakia pumziko la amani na amesema anaendelea kuendeleza yale yote mazuri yaliyoachwa na uongozi wa Awamu ya tano.

Miaka 2 tangu magufuri aondoke na ikiwa ni miaka 2 tangu Rais Samia Suluhu ashike madaraka tumeona amekamilisha miradi mingi iliyoachwa na mtangulizi wake, lakini pia anaendeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa kasi ya ajabu ikiwemo Daraja la Kigongo-Busisi ambalo litaanza kutumika 2024, ujazaji maji wa katika Bwawa la Nyerere ambalo tunatarajia kuanza majaribio mwakani n.k.

Lakini pia kwa kipindi cha miaka 2 Rais Samia Suluhu amefanikiwa kutoa ajira na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri kupitia kilimo, elimu ya ufundi pamoja na mikopo inayotolewa kwa masharti nafuu.
 
Mama akishirikiana vizuri na wapinzani ataweza kumaliza salama muda wake hadi 2025.
 
Leo ikiwa ni kumbukizi ya Hayati Dkt. Joseph Pombe Magufuri, Rais Samia Suluhu amemtakia pumziko la amani na amesema anaendelea kuendeleza yale yote mazuri yaliyoachwa na uongozi wa Awamu ya tano.

Miaka 2 tangu magufuri aondoke na ikiwa ni miaka 2 tangu Rais Samia Suluhu ashike madaraka tumeona amekamilisha miradi mingi iliyoachwa na mtangulizi wake, lakini pia anaendeleza miradi mikubwa ya kimkakati kwa kasi ya ajabu ikiwemo Daraja la Kigongo-Busisi ambalo litaanza kutumika 2024, ujazaji maji wa katika Bwawa la Nyerere ambalo tunatarajia kuanza majaribio mwakani n.k.

Lakini pia kwa kipindi cha miaka 2 Rais Samia Suluhu amefanikiwa kutoa ajira na kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri kupitia kilimo, elimu ya ufundi pamoja na mikopo inayotolewa kwa masharti nafuu.
Ni sawa
 
Oi
Kuna mdau ambaye ameelewa mama anasema nini?

Mie naamini vitendo kuliko maneno
 
Mbona Mwinyi hawamtukani humu?

Mbona Mkapa hawamtukani humu?

Kuna shida kwa huyo mtu wako
Iwepo shida isiwepo tunachokitaka ni nyie kumleta ajibu hayo matusi yenu.

Mnapambana na marehemu halafu mnavaa suti na tai kujifanya wazima kichwani
 
Sio jambo la afya kwa Rais kuruhusu mtangulizi wake akashifiwe mitandaoni akiona.

Anatengeneza precedent mbaya.

Akistaafu yakimkuta yanayotokea kwa mwenzake asilalamike.
Yamkute kwani amewatesa wapinzani au kuteka na kutesa? Malalamiko mitandaon ukiachilia wenye chuki na JPM wapo wanahoja, juu ya kufanya upinzani hasa CDM ni adui wa utawala wake. Na hilo ndilo lafanya raia waseme maumiv waliyopitia!!
 
Sio jambo la afya kwa Rais kuruhusu mtangulizi wake akashifiwe mitandaoni akiona.

Anatengeneza precedent mbaya.

Akistaafu yakimkuta yanayotokea kwa mwenzake asilalamike.
Ameshikwa pabaya! sinto shangaa nikija sikia hakutaka hata kuendelea.
Nadhani pia nguvu kubwa ya mabeberu inatumika, ilitumika kwani....
Hayati hakuwa na vita na Mwafrika, na huo ndio ukweli. Hivyo basi uadui au chuki kubwa zimetoka nje.

Chumi, au Uchumi wa wenye kuhodhi madaraka kwenye chumi mbalimbali Duniani ulishuka... ghafla na kwa haraka. Kwa hayo... Vinyongo vya usasi vimejengeka.....

nitagota hapo

Vishinikizo siyo madogo, na ndio maana ule usemi wa kuwa, 'Kuwa kiongozi sio kazi rahisi' kwa maoni yangu unakuwa na maana, aidha utumike au utumikiwe.

Ni vigumu kuwa na "utu"
 
Sio jambo la afya kwa Rais kuruhusu mtangulizi wake akashifiwe mitandaoni akiona.

Anatengeneza precedent mbaya.

Akistaafu yakimkuta yanayotokea kwa mwenzake asilalamike.
pia kuzuia watu wasitoe hisia zao kuhusu utawala uliokwisha ni Udikteta

Mwinyi aliruhusu Nyerere kusemwa
Mkapa aliruhusu Mwinyi asemwe

Jakaya aliruhusu Mkapa asemwe

JPM aliruhusu na kusaidia sana Jakaya kusemwa
na sasa si dhambi Samia akiruhusu na hata kusaidia JPM kusemwa

na baada yake nae atasemwa

hutaki kusemwa usiwe Kiongozi
 
Unataka afanyeje? Aunde kikosi cha kuteka wanaomsema vibaya Magufuli? Au nae azime mtandao?
 
pia kuzuia watu wasitoe hisia zao kuhusu utawala uliokwisha ni Udikteta

Mwinyi aliruhusu Nyerere kusemwa
Mkapa aliruhusu Mwinyi asemwe

Jakaya aliruhusu Mkapa asemwe

JPM aliruhusu na kusaidia sana Jakaya kusemwa
na sasa si dhambi Samia akiruhusu na hata kusaidia JPM kusemwa

na baada yake nae atasemwa

hutaki kusemwa usiwe Kiongozi
Muda utakupa majibu.
 
Rais Samia Suluhu ameruhusu uhuru wa vyombo vya habari pamoja na uhuru wa watu kutoa maoni yao hivyo hii ni moja ya uhuru ndio maana wa kutukana anatukana wa kusema vizuri atasema na sisi wazalendo tutaendelea kusema mazuri yanayofanywa na serikali yetu
 
Back
Top Bottom