The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali imepokea ombi la wafanyakazi wa umma la kutojumuishwa kwa posho za wafanyakazi katika makato ya kodi na kuahidi kulifikisha suala hilo kwa vyombo husika vinavyoshughulika na masuala la mapato.
Ombi hilo liliwasilishwa na Katibu Mkuu Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi (TUCTA) kwa niaba ya wafanyakazi katika risala ya wafanyakazi kwenye kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi’ ambazo kitaifa zimefanyika mkoani Singida.