Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Mheshimiwa Rais,
Umefanya ziara ya kikazi huko UAE, hilo ni jambo zuri tunalifurahia
Lakini wakati ukifanya Ziara hiyo, Watanzania hatujasahau kuwa Kampuni ya waarabu wa UAE iitwayo OBC imekuwa ikimezea mate ardhi ya wananchi inayokaliwa na wamasai huko Ngorongoro.
Tuna historia nzuri namna Mwana mfalme Brigedia Al Ali alivyopewa vitalu vya uwindaji kifisadi huko Loliondo enzi za utawala wa mzee Mwinyi, na tunajua namna alivyokuwa akikingiwa kifua na tawala zilizofuata.
Sasa tunapata wasiwasi kuwa umeenda huko kipindi hiki ambacho kuna vuguvugu la kutaka kuwaondoa wamasai kwa visingizio feki vya kutunza mazingira na uhifadhi lakini dalili zote ni. kutaka kuipa hiyo kampuni ya UAE eneo zaidi. Hatujui kama kwenye meza ya majadiliano hilo mmelizungumza, lakini hata kama mmelizungumza, mheshimiwa rais hiyo kitu ni kaa ya moto achana nayo kabisaa maana sisi wsnanchi hatuwezi kuikubali.
Tunajua miezi mitatu iliyopita alikuwepo waziri wako wa fedha huko UAE ndugu Mwigulu Nchemba, na tunajua kuwa kipindi Mwigulu alipokuwa naibu katibu mkuu wa CCM enzi za Kikwete amewahi kuunda kamati ya kuchunguza ishu za migogoro ya Ngorongoro, na hatujui kamati yake ilikuja na findings zipi, kwa hiyo tulipomuona kaenda huko UAE, na kisha aliporejea nchini tukaanza kuona harakati za kuwaondoa Wamasai Ngorongoro zimeshika kasi, tukahisi hapa lazima kuna kitu mwarabu keshafabya behind the scene!
Mwisho nataka nikwambie mheshimiwa Rais, kama mmewekeana saini ya kusafirisha wanyama wetu ili Dubai watengeneze Mbuga yao kwa kutumua wanyama kutoka Africa kama tulivyoona kwenye mitandao nayo achana nayo. Hao watu wana hela, na wanaweza kuathiri utalii wetu sana kama wakiweza kutengeneza mfano wa Safari za Afrika.
Tunajua, Mwarabu ni mzuri sana wa kugawa "Takrima", Tafadhali ndugu Rais hakikisha mwarabu hatii mguu kwenye Mbuga zetu, wanyama wetu na kikubwa zaidi kufukuza wananchi wetu ili yeye apate nafasi ya vitalu zaidi vya uwindaji.