Rais Samia sema neno juu ya upandaji wa bei ya mafuta

Rais Samia sema neno juu ya upandaji wa bei ya mafuta

Black BackUp

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
780
Reaction score
740
Habari wanabodi.... Kauli ya Rais ni Sheria....

Watanzania wote tuna imani na tunaamini kwamba Rais akitoa kauli juu ya jambo fulani bhasi hakuna mtu wa kupinga, kinachofuata hua ni utekelezaji na utendaji juu ya kauli hiyo.

Sasa bhasi kwa pamoja tumuombe Rais Samia aseme neno Juu ya upandaji wa ghafla ya bei ya mafuta.

Bei iliyoongezeka Apr 2026 ni kubwa kuwahi kutokea, kupanda kwa takribani tsh 1000 kwa maramoja ni kumuumiza mtumiaji wa mwisho ambae ni mwanachi.

Tulishaona na kusikia kauli za baadhi ya watumishi wa serikali wakituhakikishia hakutakua na ongezeko la la bei ya mafuta lakin imekua kinyume na matokeo yake bei imepanda maradufu.

Leo pia tumeona kiongozi wa shirika ewura/Latra akisema hatutegemei kuona ongezezeko la bei katika huduma za kijamii kama vile usafiri ukizingatia upandaji wa bei ya mafuta. Swali je hii itawezekena nauli kutokupanda au bidhaa kutokupanda bei ukilinganisha na upandaji mkubwa wa ghafla wa bei ya mafuta?

Tumuombe rais Samia atusaidie kupunguza mzigo huu wa bei ya mafuta ama kwa kuweka ruzuku kama alivofanya katika sekta ya kilimo kwa maana ya uweka mbolea ya ruzuku. Bhasi na kwenye mafuta kuwe na pesa kidogo ya ruzuku katika kila lita ili kupunguza gharama ya maisha kwa kwa wananchi.

Nawasilisha.......
 
Atakwambia Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake
 
We bado unaitegemea serikali, inafaa kuitwa mtu mjinga.
Serikali hii isip na huruma wala mapenzi na raia wake.
Haya mafuta hata kabla ya vita yalipaswa yasiwe bei kubwa kivile, toxo pekee yake zilikuwa ni kama 1300, hivyo ukiona mafuta ni 2800, basi ujue yameingia nchini kwa kama buku jero hivi.

Shida ya serikali zetu za kiafrika ni viongozi kuwa wabinafsi mnoo.
Walipaswa wapunguze matumizi ya serikali, lakini wapi.
Leo waziri mkuu qnaomba bajeti ya trilioni 12 na katika hizo 8.7 ni matumizi tu, sasa unajiuliza hawa watu hawajielewi ama wamejitiwa uchizi kwa tamaa ya madaraka na pesa.
 
Ufuatao ni utabiri wa hali ya hela,
Vyuma vitaendelea kukaza tahadhari mnapewa,

–Nikki Mbishi (TUKUSA 3VI)
​
 
Habari wanabodi.... Kauli ya Rais ni Sheria....

Watanzania wote tuna imani na tunaamini kwamba Rais akitoa kauli juu ya jambo fulani bhasi hakuna mtu wa kupinga, kinachofuata hua ni utekelezaji na utendaji juu ya kauli hiyo.
Sasa bhasi kwa pamoja tumuombe Rais Samia aseme neno Juu ya upandaji wa ghafla ya bei ya mafuta. Bei iliyoongezeka Apr 2026 ni kubwa kuwahi kutokea, kupanda kwa takribani tsh 1000 kwa maramoja ni kumuumiza mtumiaji wa mwisho ambae ni mwanachi.

Tulishaona na kusikia kauli za baadhi ya watumishi wa serikali wakituhakikishia hakutakua na ongezeko la la bei ya mafuta lakin imekua kinyume na matokeo yake bei imepanda maradufu.
Leo pia tumeona kiongozi wa shirika ewura/Latra akisema hatutegemei kuona ongezezeko la bei katika huduma za kijamii kama vile usafiri ukizingatia upandaji wa bei ya mafuta. Swali je hii itawezekena nauli kutokupanda au bidhaa kutokupanda bei ukilinganisha na upandaji mkubwa wa ghafla wa bei ya mafuta?

Tumuombe rais Samia atusaidie kupunguza mzigo huu wa bei ya mafuta ama kwa kuweka ruzuku kama alivofanya katika sekta ya kilimo kwa maana ya uweka mbolea ya ruzuku. Bhasi na kwenye mafuta kuwe na pesa kidogo ya ruzuku katika kila lita ili kupunguza gharama ya maisha kwa kwa wananchi.

Nawasilisha.......
sote ni mashahidi ya kinachoendelea katika nchi yanapotoka mafuta, haupo muujiza wa kudhibiti athari za mapigano ya mashariki ya kati katika sekta ya mafuta na uchumi wa dunia kwa ujumla.

Dr.Samia Suluhu Hassan hawajibiki kutoa kauli wala hahusiki kwa kinachoendelea yanapotokea mafuta.
Kama taifa na dunia nzima kwa ujumla inafaa kuwa wastahimilivu na wenye subra katika kuzibali athari za moja kwa moja katika uchumi kutokana na vita vya mashariki ya kati.

my friends, ladies and gentleman
Ni muhimu kujiandaa na ongezeko la gharama kubwa zaidi za mafuta pengine zaidi ya za leo.
 
Back
Top Bottom