Rais Samia: Serikali yenu ni sikivu, tutaangalia njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi

That's the probs hujafuatilia... Tunazungumzia ucheleweshwaji wa malipo ya wastaaf ambapo ilielezwa pesa zilikwenda kweny matumiz mengine!! So kama mafao ya wastaaf hutumiwa kwa matumiz mengine je ukifuatwa utaratib wa marekani watapataje hilo fungu la kupelekwa kweny matumiz mengine?
Hilo nimelifuatilia na nimelisema hapo juu, wewe ndiye hujanifuatilia. Halafu umekuwa vague katika kujieleza mpaka nikawa sijakuelewa unaongelea kipi hasa, ikabidi niombe ufafanuzi.

Marekani pesa za mafao zinazowekwa katika mifuko ya serikali (social security fund) zinawekezwa katika US Treasury Securities tu. Haziwekwi kwingine kokote.

US Treasury Securities is the safest investment available in the US.

Maana yake, unless serikali ya Marekani ifilisike na dollar ya Kimarekani isiwe na thamani yoyote, utalipwa mafao yako.

Serikali ya Marekani haiwekezi hela za mafao kwenye kitu chochote kingine zaidi ya US Treasury Securities, full stop, hakuna kuchujua pesa kujenga daraja, hakuna kuwekeza kwenye stocks, hakuna kuwekeza kwenye real estate, hakuna.

Hapo ndipo kunapokuwa na usalama. Huko Tanzania mara hela mjengee daraja, mara nuwekeze kwenye real estae, mara mkopeshe watu, na hapo ndipo mnapopigwa.

Kwenye mifuko ya binafsi (401k) mchangiaji mwenyewe unaamua uweke wapi pesa zako, kama unataka kweka kwenye stick markets sawa, kama unataka kuweka kwenye real estate indexes sawa, kama unataka kuweka kwenye US treasury securities, sawa.

Hapo utaona mchangiaji kalindwa pote, na hela yake haiwezi kupelekwa asikotaka.

Kwa Wamarekani hili si suala la uwekezaji tu, ni suala la maadili, hutakiwi jutumia oesa za mtu kuwekeza katika mambo ambayo hajakubaliana nayo.
 
Wiki iliyopita nilikuwa naongea na dogo mmoja kaja US kusoma Masters yake ya Finance.

Tukawa tunaongelea hili jambo, nikashangaa sana Tanzania halipo.

Nikamwambia huku kuna watu wanapenda waamue hela zao zinawekezwa vipi.

Kwa mfano, kuna watu ni wanamazingira hawataki hela zao ziwekezwe kwenye makampuni ya mafuta, hata kama hayo makampuni ndiyo yanayotengeneza faida.Wao wanapendelea zaidi wawekeze hela zap kwenye makampuni ya reneable energy, na wanapewa nafasi ya kuwekeza huko au kwingine kokote wanakotaka. Na ukishindwa kuwapa nafasi hiyo, unakosa business yao, wanaenda sehemu nyingine ambapo wanapata nafasi hiyo.

Tunahitaji competition, tunahitaji mabadiliko ya sheria kuanzisha mifuko ya binafsi mingi zaidi (isiyotozwa kodi) kama mfumo wa 401k wa US.
Unafananisha huko mbinguni kilipo kiti cha enzi cha Biden na Buhigwe na Paje Kizimkazi liwakapo ziwa la moto?

Kuwa Africa ni laana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna maendeleo bila kufananisha na kuweka malengo ya kufikia wenzetu waliotuzidi.

Unataka tujifananishe na nani sasa mkuu, Niger ?

Hawa Wamarekani ni watu tu, na wao walikuwa na matatizo kama yetu wakajipanga na kuyatatua.

Habari za laana ni mindset tu, ukiamini katika laana habari hizo zinakuwa a self fulfilling prophecy, ila laana haipo.

laana ni jibu la excuse la mtu mjinga na mvivu ambaye hataki kujipanga kukabiliana na matatizo ayatatue.
 
Hakuna maendeleo bila kufananisha na kuweka malengo ya kufikia wenzetu waliotuzidi.

Unataka tujifananishe na nani sasa mkuu, Niger ?
Braza mimi nakuelewa sana, najaribu kukukumbusha level mliyoko na huku tuliko.

Bahati mbaya hakuna kiongozi wa kututoa hapa, tupo kwenye mkwamo.

Na viongozi wengi wa Africa wanafanana kwa sababu wa Africa tunafanana, wa Africa ni nyani...si unajua nyani akiona shamba la mahindi.

Africa ni laana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akizungumzia kuhusu malalamiko yaliyopo kwenye kikokotoo katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, leo Septemba 4, 2023, Rais Samia amesema Serikali inafanyia kazi suala hilo na itaangalia njia nzuri ili kuondoa maneno mengi.

"Tupo tunakifanyia kazi na kuona jinsi tutakavyoenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kutaka kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo. Ni hali ya mifuko ilivyo. Tukisema kila anayetoka boom lako hilo hapo, boom lako hilo hapo, miaka 2 tu mifuko ile imekauka." Amesema Rais Samia.

Ameongeza, "Tuliweka hivi ili kuweka sustainability ya mfuko, sasa kwa sababu imepigiwa kelele sana sio tu na jeshi la polisi lakini na wengine, tutakwenda kuangalia sababu tunasema siku zote Serikali yenu ni sikivu. Tutakwenda tuangalie njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi"
Kwani mtu si ana chukua alicho weka? Na akiondoka ana kija mwingine na michango yake?
 
Braza mimi nakuelewa sana, najaribu kukukumbusha level mliyoko na huku tuliko.

Bahati mbaya hakuna kiongozi wa kututoa hapa, tupo kwenye mkwamo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sawa.

Lakini kutaka kiongozi akutoe hapo kwenye mkwamo ni moja ya sababu upo hapo kwenye mkwamo.

Naelewa kanuni ya Noblesse Oblige. To whom much is given, much shall be required. Hata Bwana Yesu (the philosopher, before you religious zealots get a hard on from my mere mention) alitoa mfano wa talanta na kusema aliyepewa nyingi atadaiwa marejesho mengi zaidi.

Kwa hiyo nakuelewa sana hapo kwenye uongozi.

Lakini pia, uongozi hauji tu, unatokana na jamii. Na jamii ikiwa haijachukua ownership ya nchi, haithamini meritocracy, haithamini elimu, uongozi obviously tutapata wa kubahatisha.

Wewe mwenyewe ni kiongozi mkuu.
 
Kwa hiyo nini kifanyike?

Maana we are stuck big time.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo nini kifanyike?

Maana we are stuck big time.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wananchi wanatakiwa kuchukua ownership ya nchi, ya mambo yao. Hizi habari za kutegemea viongozi wafanye mambo vizuri, wakati viongozi hawana incentive ya kufanya mambo vizuri, ni tatizo.

Pia, viongozi wanahitaji kuona wananchi wako active, wanachangia mawazo, wanaweka pressure. Kuna viongozi hawajui mambo, au wanajifanya hawajui mambo, inabidi wananchi waache huu utamaduni wa kutegemea viongozi.

Nina hakika kuna haki fulani za kikatiba zinavunjwa unapochukua pesa za mfanyakazi halafu ukaamua kuziwekeza bila sio tu kupata ruhusa ya mfanyakazi huyo, bali pia mara nyingine bila hata kumuarifu.

Hapa zilitakiwa kuwepo kesi kadhaa kushitaki kwenye suala hili.Najua kuna watu watasema mahakama zetu zinaamua mambo kisiasa, lakini kukiwa na pressure ya kutosha wananchi watashinda tu.

Pia watu wanahitaji kuongelea zaidi haya mambo kuweka awareness, watu wengine washajichokea wanaona kuwa na maamuzi na hizi hela si haki zao, inabidi waeleweshwe, na hata wasipofaidika wao, wanaokuja waweze kufaidi kutoka kwenye reforms.

Zaidi, ni vigumu kubadilisha mifumo hii bila ya kubadilisha siasa, mara nyingi siasa mbaya zinachangia ubovu huu wa mifumo ya mafao.Pesa nyingi za mafao hutumika kwenye miradi ya kisiasa, kukopesha viongozi wa kisiasa (ambao hawatoi collateral na hawalipi mikopo) na mara nyingine hata kuepeleka pesa kwenye kampeni za kisiasa.

Tunahitaji kubadili utamaduni huu wa siasa mbovu, tunahitaji uwazi zaidi, tunahitaji ushirikishwaji wa umma zaidi, na tunahitaji ushindani zaidi.

Yani ifike wakati watu waweze kuamua kabisa kwamba hatutaki kuwekeza kwenye mifuko ya mafao ya serikali, kwa sababu haina rekodi nuri, tunataka kujiwekea pesa za mafao kwenye mifuko binafsi au kutoweka kabisa.

Kwa nini mtu alazimishwe kuwekeza katika mfuko ambao hauamini?
 
Akizungumzia kuhusu malalamiko yaliyopo kwenye kikokotoo katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, leo Septemba 4, 2023, Rais Samia amesema Serikali inafanyia kazi suala hilo na itaangalia njia nzuri ili kuondoa maneno mengi.

"Tupo tunakifanyia kazi na kuona jinsi tutakavyoenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kutaka kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo. Ni hali ya mifuko ilivyo. Tukisema kila anayetoka boom lako hilo hapo, boom lako hilo hapo, miaka 2 tu mifuko ile imekauka." Amesema Rais Samia.

Ameongeza, "Tuliweka hivi ili kuweka sustainability ya mfuko, sasa kwa sababu imepigiwa kelele sana sio tu na jeshi la polisi lakini na wengine, tutakwenda kuangalia sababu tunasema siku zote Serikali yenu ni sikivu. Tutakwenda tuangalie njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi"
Huyu msimuamini katu. Ni mwongo. muulize nyongeza ya mshahara vipi?
 
Wale watu wa west watusaidie
 
Wale watu wa west watusaidie
Watu wa west na wao wanatafuta West yao usawa huu.

Anza kujisaidia watu wakuone unasaidika, sasa sisi hatuna hata kesi moja mahakamani, hata ile ya ku prove tu kuwa mahakama sinaamua kwa kufuata amri kutoka juu, tunataka watu wa west watusaidie?

Hapo utakuwa kama mtu anayeanzisha mchango, akiulizwa "wewe mwenyewe unazo ngapi?" inabidi aoneshe initiative.

Ni vigumu kumsaidia mtu ambaye hajajionesha kuwa ana deserve kusaidiwa.
 
asante rafiki, watu wa west umewafahamu lakini?
 
Legacy inazidi kupoponyolewa [emoji23][emoji23]
Kikokotoo ilikua kianze mwaka 2018,baada ya malalamiko mengi Magufuli akakisitisha ( hata kama tutasema yeye ndiye alikianzisha).

Kikokotoo hiki kimeanza 2023, sasa hapa nani wa kulaumiwa kama siye huyu anaeahidi kuwa msikivu juu ya kikokotoo..

Najua utasema hajakianzisha yeye,lakini nguvu alizonazo ambazo mnasema ameleta mabadiriko mengi,zilimshinda nini kuzuia hicho kikokotoo na aliombwa asitishe kwenye mei mosi ya 2021 akasema kitaendelea..

Hapo kapopoa legacy ya nani?

Tunaangalia aliyehitimisha jambo siyo alieanzisha
 
Aliyeleta kikokotoo 😁😁
 
Sema Mwendazake ndio alifabya huu upumbavu,ila juzi nimeona pssf wanasema Serikali imelipa nusu ya Madeni Yao hivyo Kwa Sasa ukistaafu sio kesi.

Yule katili ulikuwa ukistaafu unakaa miaka 3 au 2 unasubiria mafao
Acha chuki za kishamba hapa unaongea uongo na takataka.
 
Serikali inapaswa iwe bunifu,initiative na yenye utaalamu na viwango vya juu sio mnafanya maujinga alafu mkikosolewa ndiyo mnajidai wasikivu!!
Isijinyee kisha ujisifu unaweza kujisafisha...ulipaswa uwe msafi Toka awali usijichafue!!!
 
Akizungumzia kuhusu malalamiko yaliyopo kwenye kikokotoo katika ufunguzi wa Kikao kazi cha Maafisa waandamizi wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, leo Septemba 4, 2023, Rais Samia amesema Serikali inafanyia kazi suala hilo na itaangalia njia nzuri ili kuondoa maneno mengi.

"Tupo tunakifanyia kazi na kuona jinsi tutakavyoenda vizuri kwa sababu masuala ya kikokotoo haya si tu matakwa ya Serikali kutaka kuja na kikokotoo, ni hali ya uchumi na hali ya mifuko yenu ilivyo. Ni hali ya mifuko ilivyo. Tukisema kila anayetoka boom lako hilo hapo, boom lako hilo hapo, miaka 2 tu mifuko ile imekauka." Amesema Rais Samia.

Ameongeza, "Tuliweka hivi ili kuweka sustainability ya mfuko, sasa kwa sababu imepigiwa kelele sana sio tu na jeshi la polisi lakini na wengine, tutakwenda kuangalia sababu tunasema siku zote Serikali yenu ni sikivu. Tutakwenda tuangalie njia nzuri tunayoweza kufanya ili kikokotoo kisilete maneno mengi"
Mama Yetu tunakupenda sana. Ni kweli Wazee wengi wamepoteza maisha kwa mishtuko ya namna kikokotoo kipya kilivyo. Nikushauri mambo 2.
1. Pesa za mifuko ya jamii ni nyingi zinatosha endapo hazitatumika kuwekeza miradi ya hovyo isiyo na tija na ya kifisadi. Baadhi ya majengo yasiyo na tija yaliyojengwa kwa pesa za mifuko yauzwe pesa irudi.
2. Watumishi wanaostaafu wachague kati ya option mbili, kupata fedha nyingi za mafao ya mkupuo na kidogo yale mafao ya mwezi(kikokotoo cha zamani) Au mafao kidogo ya mkupuo na kifogo yale mafao ya mwezi( kikokotoo kipya,). Hili litatatua ujanja au shinikizo la wateule wako kuwa Watumishi ndo waliamu au kukubali kikokotoo kipya .
 
Back
Top Bottom