Rais Samia sio Magufuli na hawezi kuwa Magufuli

Rais Samia sio Magufuli na hawezi kuwa Magufuli

Ashasembeko

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
226
Reaction score
914
Huwa napenda kupitia kwenye mitandao ya kijamii kuona namna gani waTanzania wanamchukuliaje Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Jicho langu limeona, Rais Samia anasupport kubwa katika mtandao wa Twitter kuliko Instagram na Facebook ambapo maoni dhidi ya aina ya uongozi wake yanaonekana kuwa polarized.

Kikubwa nilichokigundua katika mitandao ya Instagram na Facebook, watumiaji wengi huwa wanajaribu sana kumlinganisha na mwendazake katika kila jambo atakalofanya.

Mfano, Rais Samia anapenda kutumia usafiri wa ndege, kila Gerson anapotuhabarisha kuhusu hili, kuna baadhi ya watu hucomment vitu kama "Rais asafiri na barabara kama JPM aone shida za wananchi na kupunguza gharama" "Nimemiss JPM yeye alikuwa hapandi ndege". Haya maoni yanafikirisha sana. Hawajui kuwa msafara wa Rais ni ghali zaidi kuliko ndege, na pia wanasahau JPM alikua na tatizo la moyo ambalo lilimdhibiti asiwe anapanda ndege haswa kwenye safari za masaa mengi (akawahadaa watu kuwa ni kwasababu anabana matumizi).

Mfano mwengine ambao ndio umenifanya niandike andiko hili, ni katika ziara ya Rais Samia leo, Dar. Katika ziara yake, kuna baadhi ya comments zilimtaka Samia awafokee watumishi kama JPM alivokuwa anafanya. Yeye Samia alikuwa anawahoji na kuwauliza kwa ustaarabu tu. Ifike wakati tukubali kuwa Samia sio JPM, ana style yake ya uongozi na hata personality yake ni tofauti. JPM ni mmoja tu na kashaondoka, harudi tena.

Huwezi kumlazimisha Samia awe kama Magufuli haiwezekani, akifanya hivo atakua anaigiza na kama watanzania sidhani kama tunakata viongozi ambao hawapo authentic.

Kingine ni kuwa Samia, anaonekana kadelegate power/kampa nguvu kubwa Waziri Mkuu ukilinganisha na JPM ambapo maovu karibu yote alikuwa anataka afichue yete na utumbuaji alikua anataka afanye mwenyewe, kama sponsor wa taarifa za intelijensia alikuwa anabaki nazo yeye na kuwaambia wananchi wakati wa hotuba zake. Anachofanya Majaliwa sasa hizi ndio kazi haswa ya Waziri Mkuu kama mtendaji mkuu wa serikali. Na hii inarahisisha kazi ya Rais, maana anakuwa focused na mambo ya kitaifa na kimataifa - kuweka mahusiano sawa, kuvutia wawekezaji, ulinzi na usalama nk.

Samia sio JPM na hawezi kuwa JPM, mashabiki wa JPM walikubaliana na hili watakuwa huru sana, na wataanza kukosoa constructively. Kazi kwao.
 
E0NhMwdXIAAW0HL.jpeg
 
Umeongea mengi ila umekosema hapo kwa Majaliwa tu.

Majaliwa wa JPM alikuwa na power kubwwa kuliko majaliwa wa Samia.

All in all watu lazima watoe maoni japo kuwa ukweli unabaki kuwa Samia hawezi kufafa na JPM japo kuna mambo anatakiwa ajifunze hasa ufuatiliaji na usimamiaji.
 
Hata sisi hatutaki awe kama JPM maana JPM alikuwa mmoja tu. Ili iweje kwanza!?
ili muanze kuimba yale manyimbo yenu ya kishindo cha awamu ya 6
Atake asitake tumwongezee muda
Serikali ya wanyonge
Na takataka nyinginezo
 
Umeongea mengi ila umekosema hapo kwa Majaliwa tu.

Majaliwa wa JPM alikuwa na power kubwwa kuliko majaliwa wa Samia.

All in all watu lazima watoe maoni japo kuwa ukweli unabaki kuwa Samia hawezi kufafa na JPM japo kuna mambo anatakiwa ajifunze hasa ufuatiliaji na usimamiaji.
Kuna watu watumishi wengi sana waliganya ya hovyo ila Majaliwa alishindwa kuwachukulia hatua sababu walikua na protection ya JPM. Mfano. Kakoko, na RAS mmoja wa kule Tarime.

Kumbuka pia katika sakata la korosho, Waziri mkuu alikuwa ashapata wafanyabiashara wa kununua korosho lakini JPM mbele ya media akamlatalia na akaamuri jeshi lisimamie zoezi. Usishau JPM alitishia kumtwanga shangazi yake.
 
Huwa napenda kupitia kwenye mitandao ya kijamii kuona namna gani waTanzania wanamchukuliaje Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Jicho langu limeona, Rais Samia anasupport kubwa katika mtandao wa Twitter kuliko Instagram na Facebook ambapo maoni dhidi ya aina ya uongozi wake yanaonekana kuwa polarized...
Hawana elimu kuhusu kisaidizi cha mapigo ya moto 'pacemaker'
 
Huwa napenda kupitia kwenye mitandao ya kijamii kuona namna gani waTanzania wanamchukuliaje Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Jicho langu limeona, Rais Samia anasupport kubwa katika mtandao wa Twitter kuliko Instagram na Facebook ambapo maoni dhidi ya aina ya uongozi wake yanaonekana kuwa polarized...
Hana ubavu huo period, na hawezi kumfikia Magu. Ni ngumu watu kuwachambulia kujua raisi wao yukoje, hasa walioshuhudia awamu4, 5 na hii ya 6 ambayo ni extremely soft.
 
Mleta mada kuna tofauti kubwa ya Magufuli na Samia, Magufuli akienda sehemu yeyote ujue ana data ya mradi huo A to Z , hivyo aliwayliza watendaji wake kuwa je hili mnalifahamu? huwezi kuwa na mtendaji wao anaefuatilia na kusimamia kazi na asijue chochote kuhusu mradi husika huyo ni mtendaji au zwazwa?

Tusipende kukumbatia watu wavuvi kwa kisingizio cha kufokewa, that's very weak for Tanzanian citizens , watu dhaifu huzaa taifa dhaifu ndo tulilonalo sasa, nani akubembeleza hapa duniani? nafasi ni chache, wasomi ni wengi kwa pembeni kama huwezi wengine wafanye.

Kuna wengine wanajidanga ohh Rais ni taasisi OK kwanini tusipigie kura taasisi kwenye makaratasi ? ulizeni watu wanavyo survive private sector ndo mtajua nini ya kufanya kazi kwa bidii, kule watu hawa bembelezani, hujui kama contract yako kila mwaka itakuwa extended as the results matokeo ya kampuni huwa positive kuliko mashirika ya umma, kama tunataka maendeleo tuache kurendemuka kama mrenda.
 
Huwa napenda kupitia kwenye mitandao ya kijamii kuona namna gani waTanzania wanamchukuliaje Rais wetu Samia Suluhu Hassan. Jicho langu limeona, Rais Samia anasupport kubwa katika mtandao wa Twitter kuliko Instagram na Facebook ambapo maoni dhidi ya aina ya uongozi wake yanaonekana kuwa polarized...
Heshimu watu na utu uwepo moyoni , Rais SSH ana utu na busara hata kama mtu kakosea anaheshimu utu hadhalilshi wengine
 
Mleta mada kuna tofauti kubwa ya Magufuli na Samia, Magufuli akienda sehemu yeyote ujue ana data ya mradi huo A to Z , hivyo aliwayliza watendaji wake kuwa je hili mnalifahamu?...
Na hayo ndo yalituchelewesha awamu ya nne, kubembelezana na kuoneana aibu huku nchi inaelekea shimoni. Ni swala la muda tu mtaanza kusikia ufisadi wa kutisha.
 
Back
Top Bottom