Rais Samia sio Magufuli na hawezi kuwa Magufuli

Mleta mada kuna tofauti kubwa ya Magufuli na Samia, Magufuli akienda sehemu yeyote ujue ana data ya mradi huo A to Z , hivyo aliwayliza watendaji wake kuwa je hili mnalifahamu? ...
Naunga mkono.
 
Mleta mada kuna tofauti kubwa ya Magufuli na Samia, Magufuli akienda sehemu yeyote ujue ana data ya mradi huo A to Z , hivyo aliwayliza watendaji wake kuwa je hili mnalifahamu? ...
Hoja yako ya kwanza haina mashiko na sidhani kama ulifuatilia vizuri ile ziara ya jana ya Samia. Alivoenda kutembelea hiyo miradi alikuwa anajua tayari mambo yanayoendelea ndio maana 'akawashtukiza'. Alisema mwenyewe hata alipowahutubia wananchi Kariakoo, aliposimamisha uongozi mzima wa soko, na alisema pia katika mradi wa BRT pale mbagala.

Angekua hajui kinachoendelea au 'mvivu' kama unavyomuita, yale maswali aliyokuwa anamuhoji yule mtendaji wa BRT aliyajuaje? Hoja yangu bado ipo pale pale, approach yake ni tofauti na JPM aliekuwa tu anafoka tu sa nyengine bila sababu na kudhalilisha watumishi ili aonekana ni Rais mkali na makini. Uongozi hauendi hivyo.

Hoja yako ya pili, ni kweli kuwa kiongozi ni kiini kizuri cha kusukuma gurudumu la maendeleo, ila kiongozi asipotengeneza taasisi dhabiti maono yake yanaweza yasitekelezeke maana anaishia kufanya kila kitu mwenyewe. Mfano mzuri kabisa ni kifo cha JPM, aya nyie mnaeamini kuwa alikuwa Rais bora na kuwa alifanya mengi, hayo mambo yanaendeshwaje bila yeye kuwepo na hakuinvest katika taasisi imara? Ndio haya mambo tunaona kila Rais akija anakuja na mambo yake, mwishowe maendeleo ya nchi hayawi endelevu, yanaishia kuwa ya miaka kumi au mitano. Kiongozi imara ni muhimu ila taasisi imara ni muhimu zaidi maana ndio zitalinda maendeleo yaliyoasisiwa na kiongozi huyo hata asipokuwepo.

Na kuhusu 'kubembelezana' - huyo JPM na style yake ya kutobembelezana kalifikisha wapi taifa. Umeongelea kuhusu results, twende kwenye takwimu za serikali, angalia ukuaji wa uchumi wakati wa JPM na waliomtangulia kina Kikewte na Mkapa. Wakati wa JK na Mkapa uchumi ulikua unakua kwa asilimia 7-8% ila kwa JPM ukaanza shuka kila mwaka, mpaka anafariki uchumi ulikua unakua kwa asilimia 4.7%, tena Benki ya dunia inasema uchumi ulishuka hadi asilimia 2.

Hizi ndio results za kutombelezana. Kwa maoni yangu style ya JPM inafaa kwenye ujenzi tu, na ndio maana miondombinu ulikua inaenda, ila kwenye maswala mengine aliboronga, hata kwenye rushwa, na ripoti za CAG zimethiirisha hivyo. Tunaona hata washikaji wake kina Kakoko walivyokwapua mabillioni hazina. Yeye mwenyewe atueleze kwanini kampuni yake ambao umiliki ameupa jina la rafiki yake, ndio ulikua unapewa tender nyingi katika uongozi wake ikiwemo uwanja wa ndege chato. Waandishi wa habari, mmeanza pata uhuru, fuatiliani hii story na ii kampuni.
 
Uongozi sio kufokafoka na kutukana watu.

Kiongozi inapendeza uwe na lugha ya kistaarabu, Rais anawezaje kutamka "mbaki na mav* yenu" yani hata mimi anonymous naona tabu kuandika.

Samia kwa kiasi kikubwa sana ni kiongozi bora
 
Ndiyo maana JPM alikuwa mwanamume na Samia ni mwanamke,JPM ni mkristo na Samia ni mwislam,JPM ni msukuma na Samia ni Mzanzibar, hata siku moja hawawezi fanana sera, mitazamo, akili na upeo.
 
Na hayo ndo yalituchelewesha awamu ya nne, kubembelezana na kuoneana aibu huku nchi inaelekea shimoni. Ni swala la muda tu mtaanza kusikia ufisadi wa kutisha.
Yaliwachelewesha nini wakati hali ya uchumi Tanzania ilipaa na maisha kwa watanzania yalikuwa ya raha mstarehe mfano;ajira zilikuwepo,mishahara ya watumishi ilipanda kila mwaka,soko huria kwa wafanyabiashara,miundo mbinu ya kuunganisha mikoa,hali ya siasa nchini ilikuwa bora kuliko tawala zilizopita na hizi zilizopo,vyombo vya habari kufanya kazi kwa uhuru zaidi,kwa mara ya kwanza baada ya kupita miaka mingi Tanzania ilifuzu kucheza CHAN chini ya kocha Mbrazil Maximo nk.
 
Hoja yako ya kwanza haina mashiko na sidhani kama ulifuatilia vizuri ile ziara ya jana ya Samia. Alivoenda kutembelea hiyo miradi alikuwa anajua tayari mambo yanayoendelea ndio maana 'akawashtukiza'...
Watu ni wajinga jamani! Ndio matokeo ya kumfuatilia kigogo haya?

Unasema kampuni ina jina la rafiki yake kisha unasema ni ya hayati? Ulikuwepo wakati inaanzishwa?

Hayo mengine ni porojo tu.

Hili taifa tutaelewana tu baada ya miaka 2 ijayo.
 
Sijawahi sikia tatizo lolote la moyo linalo msababisha mtu kutopanda ndege.
 
Magufuli alikuwa dikteta mwenye roho mbaya, Samia ni muungwana na yupo makini
 
Sikubaliani na hoja zako zote
 
Uongozi sio kufokafoka na kutukana watu.

Kiongozi inapendeza uwe na lugha ya kistaarabu, Rais anawezaje kutamka "mbaki na mav* yenu" yani hata mimi anonymous naona tabu kuandika.

Samia kwa kiasi kikubwa sana ni kiongozi bora
Wevi na wazembe lazima waambiwe hivyo..
 
Hahaa!!!walihadaiwa sana na bi.kirembwe haya mazombi
ili muanze kuimba yale manyimbo yenu ya kishindo cha awamu ya 6
Atake asitake tumwongezee muda
Serikali ya wanyonge
Na takataka nyinginezo
 
Jamani wacheni turudishe utu na amani ya Taifa letu;hamwoni watu wanafurahi kuona tuna Rais asiyetukana na mwenye kujali utu??Mnataka nini zaidi.Mama tupo nyuma yako kazi iendelee
 
Pamoja na mapungufu ya Magufuli, ila kuna mambo tuliyasahau maana alikuwa mkali, umeme saizi unakatwatwa tu bila sababu tu,yaani leo dsm kkoo.....mambo ya majeneta kama kawa now....
 
Amekiri mwenyewe...

Amekiri kuwa anawateua maRC na maRAS wakamsaidie kazi kwani hayati JPM alikuwa ana uwezo mkubwa wa kuhesabu mabati na vyombo vya ujenzi pamoja na kukagua CONSTRUCTION issues....yeye ni mchumi tu what an exquisite comment our beloved President uttered!

We really admire her Excellency President.....

Yes ,she directs us on a RIGHT TRACK....

May Almighty God grant her tranquility and healthy aaamen aaamen!!!

#KaziInaendeleaKwaKasiYaKutisha
#NchiKwanzaKablaYaNafsiZetu
 
Samia kwa kiasi kikubwa sana ni kiongozi bora
Samia ana nafasi kubwa sana ya kuacha ENDELIBLE legacy hapa nchini kama atakuwa mtawala anaependa haki; na hilo litamkwepesha hata kutoka kwa wale watakaotaka kumshauri visivyo!!! Haki hutokana na taasisi imara na hilo ndio liwe lengo lake kuzijenga hizo taasisi.
Kule kwenye chama aendeleze yale aliyoyaacha mwendazake kwa kuhakikisha kuwa ccm inakuwa na vitega uchumi imara ili isiwategemee wafanya biashara kwa shuhuri zake na kwa kufanya hivyo ataziba mianya ya mwanzo wa rushwa[magendo]!!
Hao ccm ya Msoga ni wanachama waliolelewa kwa fedha za wafanya biashara hivyo wao na rushwa ni watoto wa baba mmoja!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…