Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Unajikombakomba...
 
Najua anajua kuwa anachomekewa au anaamua na yeye kuwachomeka wakati anajua mzigo unamwangukia si afanye vetting upya? Maana walishasema wanalamba asali (Makamba senior voice). Wanatumia kijiko au kidole wanajua wao.
 
Pascal kosa lile lile ulilofanya kwa kuimba na kusifia magufuli ATCL baadae ukaja kuomba radhi unalirudia tena.
Ukinikumbusha nilifanya kosa gani kwa Magifuli na ATCL kisha nikaomba msamaha, nitakushukuru.
Pascal uwe na akiba ya maneno usijimalize kiasi hichi mkuu.
Mbona mimi ni mtu wa akiba sana ya maneno, mfano mzuri ni ujio wa Magufuli, niliusema humu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli nikasema niliambiwa sababu, jee uliwahi kuzisikia nikizisema?.

Nimeitwa kuhojiwa Bungeni Dodoma, uliwahi nisikia nikisema kulitokea nini?.

Kuhusu 2025 kuna kitu nakijua, nimekieleza humu kwenye sauti HII jee nimekitaja?.
P
 
Ukinikumbusha nilifanya kosa gani kwa Magifuli na ATCL kisha nikaomba msamaha, nitakushukuru.
Pascal,

Ulisifu sana huku ukiingiza na ukabila kwamba sisi “wasukuma”
Binafsi nilishangaa sana lile bandiko lako likifurahia kujaa kwa ndege. Tena kipindi magufuli akifanya vitu kwa ubabe mkubwa bila ya kushirikisha hata mihimili mingine.


Baadae mkuu pascal ukaja kusema hivi

Post in thread 'Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka'
Kweli Magufuli anataka kuifufua ATCL, ila hii "kachumbari ya ndege" anazonunua inatia mashaka

Mkuu pascal hukuandika kitu kibaya ila ulikuwa Ukisifia sana huku ukiweka suala la ukabila. Mtu kama wewe kwa kazi yako kuna mambo unapaswa kuyaepuka.

Ulikiri mwenyewe hukuwa unaelewa unachosifia. Ndio maana nikasema hata yanayoendelea sasa kuwa na akiba ya maneno pascal. Muda huwa ni mwalimu mzuri.

Labda kama uwe umeamua kuwa waimba mapambio kama wengine, ila kwako nafikiri haipo hivyo.
 

Attachments

  • 3D6DADBB-1DC4-4F03-8E7A-11C779F2F746.jpeg
    119.3 KB · Views: 2
Ili nikaufanyie nini huo uteuzi?. Mtu ayesaka uteuzi anaweza kutoa hoja kama HII ?.
P
expand...
"hata hili kosa la uteuzi wa marehemu sio lake!, this is bonafide genuine mistake ya communication break down, by the time Lupa, anakutwa na umauti, uteuzi ulikuwa tayari ila mkeka haujapanda. Wakati tangazo la msiba linatoka, hakuna aliyenote mteuliwa mmoja yuko amefariki jana yake!. Hili ni kosa genuine, let's not make.a big deal!.
P"
Hiki ni nini kama siyo kujaribu kujionesha ili ukumbukwe kwenye uteuzi?
 
Kwanza asante kunikumbusha, yote niliyoyasema kuhusu JPM na ununuzi wa ndege mpya ni ya kweli kabisa, na nilieleza kila kitu,
Hii maana yake, kiongozi anaweza kufanya jambo baya na tukamshutumu, mbele ya safari hilo jambo baya likaleta matokeo mazuri, wewe wewe ulielaani lile jambo baya, utapongeza, hayo mazuri ya jambo baya!.

Ubakaji ni kosa la jinai, lakini ukimbaka mgumba, aliyeolewa na tajiri, lakini ananyanyaswa na kusimangwa kwenye ndoa yake kwa sababu ya ugumba, akashika ujauzito, na kuiokoa ndoa yake, kimoyo moyo atakushukuru, na mtoto akitimiza miaka 3, mwanamke huyo atakutafuta na kukupa, umbake tena ili apate mtoto wa pili. This time akakupa yote!, ila haimaanishi kile kitendo cha ubakaji ni kizuri na sio kosa.

Kununua ndege bila business plan ni kosa. Kununua ndege kwa cash kwa mtindo wa kupiga tanchi ni kosa. Kurusha ndege kubwa za long distance haul kwa short distance routes ni kosa, engine zina wear and tear mapema!.
Ila ndege imejaa unatoa pongezi!.
Sijawahi kuliombea msamaha hili la ndege popote!.
P
 
kiufupi mkuu pascal ulitoa sifa kwa kitu usichokielewa. Nashukuru kwa kukiri kwa barafu hukuwa unaelewa na sasa unaelewa.
Kama nilivyosema, hakuna mkamilifu, no.one is perfect, kuna siku niliwakosea Chadema humu niliposema CHADEMA yakubali yaishe! yamtambua Rais, yampongeza Rais

Mhe. Regia Mtema akanishukia Pasco Tuombe radhi CHADEMA-Umemwelewa Vibaya Hon Mbowe

Niliomba radhi Nawaomba radhi wana CHADEMA, nilimwelewa vibaya Mhe. Mbowe - Pasco

Hivyo nikokosea huwa naomba msamaha, ila yote niliyoeleza humu kumhusu JPM ni ukweli mtupu na sijawahi kuombea msamaha. Hata Samia, tunampongeza kwa mazuri yake na kumkosoa panapostahili ukosoaji.

P
 
kiufupi mkuu pascal ulitoa sifa kwa kitu usichokielewa. Nashukuru kwa kukiri kwa barafu hukuwa unaelewa na sasa unaelewa.
Ndugu yangu passion_amo1, pole sana kwa kutwanga maji kwenye kinu. JF kwa sasa imekuwa zaidi ya kokoro, inazoa hadi visivyozoeleka. Kuna wakati nashawishika kuwa nchi hii ina laana ya aina fulani, laana kubwa...hebu tafakari hii...

Anatokea kiongozi muovu kama shetani (ni kweli binadamu, kwa uovu wake wote kama binadamu, hawezi kuwa muovu kuliko shetani) anaiba, anatesa na anaua. halafu kama janja ya panya anapuliza alipouma kupunguza maumivu.

Kila baada ya kufanya kufuru anapuliza palipoumia kwa jitihada kama ya kugawa hela kwa waathirika na ndugu zao. Sifa zinaanza kumiminka kwa jinsi anavyowajali anaowaongoza na ni vigelegele kina kona. Masikini Tanzania yetu.
 
Mkuu Mag3,

Kiukweli nilichokuwa ninamuonyesha hapo pascal ndicho anachoendelea kukifanya.

Katika ule Uzi pascal aliandika akiwa na mapenzi ya kikabila akisema kwamba sisi wasukuma kitu ambacho kwa taaluma yake si sahihi hata kidogo.

Na watu walimtafsiri kama alikuwa chawa akililia nafasi kwa mzee wetu magufuli.

Nilishangaa sana kwanini mtu kama Pascal aandike vitu kama vile na ni mtu mwenye taaluma ya Habari. Kiukweli iliweka maswali mengi sana.

Sasa baada ya kukiri kwamba hakuelewa nini alichokuwa anakipa sifa kuna mtu akamjibu baada ya “kufa magufuli ndio akili imekurudi sasa Hongera sasa”

nilikuwa ninamwambia Pascal awe na akiba ya maneno na asiwe mjuaji sana.
 
Tatizo liko hivi hao wanaoteuliwa kuahirisha kufikiri kwa nafsi a.k.a kujizima data, herding behavior is an occurrence of entrusted people suspending their individual reasoning because of flattering or working towards group objectives and fear of their leaders, yaani unayeteuliwa unapokuwa nyumbu nipale anaposhindwa kufanya maamuzi kwa masilahi ya taifa badala yake anajipendekeza ama kutumikia kundi fulani au uoga wa viongozi wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…