Rais Samia, siyo kupanda kwa bei ya vyakula pekee, ambako kutawafanya Gen Z ya Tanzania waingie barabarani

Rais Samia, siyo kupanda kwa bei ya vyakula pekee, ambako kutawafanya Gen Z ya Tanzania waingie barabarani

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Nimemsikia Rais Samia Jana, wakati akihutubia wakazi wa Mtibwa -Morogoro, akiwa katika ziara Mkoani humo, akiwatahadharisha wateule wake, hususani walioko Kwenye wizara ya kilimo kuwa chakula ni jambo nyeti sana, ukitokea upungufu wa chakula nchini, unaweza walazomisha vijana wanaotambulika siku hizi kama Gen Z, waingie mitaani na kuandamana.

Ninachomwambia Rais Samia, ni kuwa Kuna mambo mengi sana ya hovyo, yanayofanyika nchini kwetu, ambayo hao vijana wa Gen Z wa nchini kwetu, wanayavumilia, lakini naamini, itakapofika mwisho wa uvumilivu wao, wataingia barabarani na kuandamana.

Matatizo hayo ni pamoja na vijana wengi sana wanaomaliza elimu ya vyuo vikuu kila mwaka, kukosa ajira nchini

Vile vile mifumo ya nchi hii ndilo tatizo Kuu linaloliangamiza Taifa letu.

Hii nchi kiuhalisia Haina mipaka ya utendaji wake wa kazi, Kati ya mihimili mikuu 3 ya Dola, ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.

Katika nchi yetu, serikali, chini ya Rais wa Jamhuri ndiye mhimili Mkuu, ambao Kwa maneno ya Mwendazake John Magufuli kuwa ndiyo mhimili uliojichimbia zaidi chini!

Katika nchi yetu Rais amepewa madaraka makubwa mno ya ki-mungu- mtu, kunakofanya mihimili Ile mingine ya Bunge na Mahakama, isiweze kufanya kazi Kwa uhuru.

Mimi huwa najiuliza hivi kama kweli mihimili hii 3 ingekuwa inafanya kazi Kwa uhuru bila kuingiliwa na mhimili mwingine, hivi ni kwanini wale wabunge 19 wa viti maalum, wanaendelea kuwemo Bungeni Kwa mwaka wa 4 hivi sasa, wakati inafahamika wazi kuwa wabunge hao hawana chama wanachokiwakilisha Bungeni, baada ya Chama Cha Chadema, wanachodai kuwa wao ni wanachama wa chama hiko, kusema kuwa imeshawafukuza zamani sana, tokea mwaka 2020??

Hivi inakuwaje Spika wa Bunge, achukuwe uamuzi wa kumfukuza Mbunge Luhaga Mpina, ambaye amesema kuwa Waziri Bashe amelidanganya Bunge, ambao ni wajibu namba moja wa wabunge wa kuisimamia serikali, wakati alipotoa taarifa ya uagizaji wa sukari, wakati kulipotokea upungufu mkubwa wa sukari, mwishoni mwa mwaka Jana??

Kwa hiyo nimwambie Rais Samia, kuwa vipo viashiria vingi sana, vinavyoweza kusababisha hii Gen Z ya hapa nchini kuweza kuandamana na Wala siyo tuu kwa kukosa sukari, kama alivyotahadharisha Rais Samia Jana, ambako yupo ziarani Mkoani Morogoro.

Mungu ibariki Tanzania
 
Bado hujayajua Matatizo ya Watanzania vizuri wewe:

1: Kuna watu hawajui hao wabunge 19 ( Japo ni hoja ya Msingi)
2: Ajira sawa
3: Kupotea watu kunakoitwa kutekwa
4: Gharama za maisha kupand6:a kiholela ukilinganisha na nchi jirani zinazotuzunguka mfn.Mafuta,Sabuni, Sukari
5: Ufisadi uliokithiri
6: Upendeleo katika teuzi mbalimbali( Kwa uchache)
7: Stahiki mbovu za watumishi, (Kikokotoo na Mishahara isiyokidhi, nk)
yapo mengi
 
Bado hujayajua Matatizo ya Watanzania vizuri wewe:
1:Kuna watu hawajui hao wabunge 19 ( Japo ni hoja ya Msingi)
2: Ajira sawa
3:Kupotea watu kunakoitwa kutekwa
4:Gharama za maisha kupand6:a kiholela ukilinganisha na nchi jirani zinazotuzunguka mfn.Mafuta,Sabuni, Sukari
5:Ufisadi uliokithiri
6:Upendeleo katika teuzi mbalimbali( Kwa uchache)
7:Stahiki mbovu za watumishi, (Kikokotoo na Mishahara isiyokidhi, nk)
yapo mengi
Naunga mkono hoja uliyoitoa Kwa asilimia 100

Bahati nzuri umefafanua vizuri sana kuhusu matatizo mengi sana, yanayowakabili watanzania Kwa sasa.

Ikiwa watawala wetu wataendelea kutudharau, hadi kufikia kutwambia kuwa wasiridhika na hali hiyo, wahamie Burundi!
 
Ajira na kodi za hovyo hovyo zinaweza kusababisha G z kutembea Road na hakuna wa kuwazuia..
 
Kumbe Message kutoka Gen Z ilikuwa received and derivered!
 
Back
Top Bottom