Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Mh. Rais, najua unatambua kuwa safari ya kuyafikia maendeleo siyo nyepesi, siyo tambalale wala mteremko. Mh Rais sisi watanzania huwa tunalalamika sana linapoanza jambo fulani na kuinua sauti za kelele kila mahali ili mradi tu kila mtu kaongea.
Mh. Rais wetu, umekuwa muwazi sana katika serikali yako, wananchi tunaona miradi mbalimbali ikijengwa kutokanaa na makusanyo ya kodi na tozo zilizopitishwa na kupitia michakato ya kisheria. Tunaona dhamira yako ya dhati katika kuijenga nchi hii, tunaona kuwa unachohitaji ni kuona mwananchi anapata huduma bora zilizo karibu kabisa na watu walipo.
Mh. Rais, tunaona dhamira yako ya kuona hakuna mtanzania anayeachwa nyuma kimaendeleo wala kutengwa, tunaona ikijengwa nchi na uchumi unaomgusa kila mtu na kumnufaisha kila mmoja wetu.
Mh. Rais, najua kelele zitapigwa kwa sasa lakini matunda yake yataliwa na kutufaidisha watanzania wote kwa pamoja. Ni lazima tuwajibike kuijenga nchi yetu, lazima tuanze kuijenga nchi yetu kwa mikono yetu wenyewe kwa kuchangia maendeleo yetu wenyewe. Hata hao wa Ulaya walipitia huku, hakuna njia nyingine ya kutufikisha waliko fika kama tusipopitia huku.
Mh. Rais, endelea tu kusimamia kila kinachopatikana ili kisiguswe na mtu yoyote kwa manufaa yake binafsi, na ikitokea akibainika kagusa basi awajibishwe bila huruma wala kumpa nafasi ya pili. Maana atakuwa anachezea jasho la watanzania wanyonge walio amua kuijenga nchi yao kwa mikono yao wenyewe, kwa kuchangia na kujibana kutoka katika vipato vyao ili kujenga kesho iliyo bora zaidi, bila kuwa na mzigo wa madeni kwa nchi yetu.
Mh. Rais, jambo kubwa ninalotaka kukuhakikishia ni kuwa, huku niliko mtaani unakubalika sana na kuungwa mkono sana uongozi wako. Wakulima kwa sasa ni shangwe kwako, hasa katika kipindi hiki ambacho zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kupokea mbolea za ruzuku ukiendelea. Wananchi wanakupongeza kwa kuwa wanaona huduma zikisogezwa karibu yao na kuondolewa adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma.
Songa mbele Mh. Rais wetu, maana kazi ufanyazo zimegusa maisha ya watu hasa wanyonge, ipo siku watu watapiga magoti chini kukuomba msamaha kwa kelele zao za sasa. Maana kwa macho yao hawaoni kwa sasa kule tutakako kuwa kesho kwenye nchi ya asali na maziwa na yenye kutiririsha fursa mbalimbali.