Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Ndugu Rais,
Hili suala la wamachinga ni very sensitive nakushauri uende nalo kwa busara kubwa sana.
Nadhani uliona maelfu ya waliotoka mabarabarani kumlilia Magufuli, naweza kusema probably kuwa zaidi ya 70% ni Wamachinga.
Hili ni jeshi kubwa sana ambalo ukilizingua litakuzingua kweli.
Pamoja na mapungufu mengi tu ya mtangulizi wako katika masuala ya uongozi lakini katika vitu alivyotumia akili ni namna ya kudeal na wamachinga. Baada ya mtangulizi wako kugundua kuwa hakubaliki katika cadre ya wasomi na wafanyabiashara wakubwa, aliamua kurudi chini kwenye grassroots na kufanya urafiki na wamachinga. Hawa ndo waliomzika!
Pia tambua kuwa nchi hii ina tatizo kubwa la ajira, shukuru Mungu kuwa kuna namna japo haipendezi ambayo mamilioni ya wananchi wanajipatia riziki yao. Tafadhali usianze kuwadisturb hawa wamachinga, utapata tabu sana kutawala kama kundi hili la mamilioni litakukataa. Na utapata wakati mgumu zaidi wakitokea watu wa kuwasongesha mtaani.
Pia fahamu kuwa kitendo cha kundi hili kuweza kujipatia riziki kulipunguza sana wimbi la ujambazi mitaani. Chondechonde nakuomba Ndugu Samia, usidisturb kabisa kundi hili bali litafutie utaratibu mzuri wa biashara zao bila kuwaswaga ghafla.
Ndugu, Rais ukivunja vibanda vya wamachinga leo, sisi wenye kipato tutakushangilia, lakini kabla hujafanya hilo jiulize hawa wanaopata rizki kutokana na hivyo vibanda wakale wapi?
Ndugu Rais, naongea haya nikiwa mtu ninayependa miji iwe safi kweli, lakini sasa Wenzetu hawa wanahitaji nao mkono kwenda kinywani tufanyeje?
Angalia dissatisfaction isije ikawa kubwa sana mtaani utapata tabu sana kutawala nchi hii.
Ni lazima uendelee kujali watu masikini bila kuumiza Matajiri, Ukiigeuza serikali yako kuwa ya Matajiri na wenye kipato tu bila kuwaangalia walalahoi utafeli
Kuwa Makini sana!