Mchango mzuri, ila naomba nikupinge kwa hoja
1. Kusema magufuli alideal na wamachinga kwa akili hili si kweli hata kidogo, angedeal nao kwa akili angewatengenezea maeneo rasmi ya kufanyia biashara, alichokuwa anakitafuta ni cheap popularity, hakuwa na nia njema nao, kufanya biashara barabarini ni sawa tu na kujenga nyumba kwenye reserve ya barabara.
2. Umesema kuwa tatizo ni ajira, Hata kama ajira hakuna lazima tuwe na utaratibu wa kufanya biashara ya umachinga
3. Eti kuwaruhusu wamachinga barabarani imepinguza uwalifu, hili sio kweli hata kidogo, kuruhusu watu kufanya biashara za umachinga barabarani maeneo yasio rasmi ni hatari zaidi kwa uwalifu, kumbuka machinga wanaongezeka kila uchao ukawajaza barabarani unadikiri kitakachotokea nini.
4. Tusiwaone wamchinga kama untachable, kwa kuhofia kukosa kura kutoka kwao, lazima tuwe watu wa kufuata utaratibu na sheria za nchi, hakuna jamii ambayo eti wao wanapaswa kupata upendeleo sana kuliko nyingime mope hio si sawa.
5. Kupata riziki kwa kuwaruhu machinga kufanya barabarani sio sawa, haitamsaidia kuwa na bishara endelelevu atakuwa mtu wa kuhama hama kamamifugo, hilo haliwezi kuwa sawa, kama tunatanga kuwasidia hawa machinga wapewe maeneo rasmi ya kufanya biashara zao.
6. Mmama hinga hapaswi kuwa mmachinga siku zote anapaawa baadaye awe mangi, hapo na serekali itapata kodi yake.
7. Mimi sio muumini sana wa umachinga, kuzalisha wimbi kubwa la wachuuzi ni nikujitengezea bomu kubwa sana hapo baadaye, nani wasiojua kuwa ili kukwepa kodi wenye maduka wanawapa machinga bidhaa amabazo ndiyo wanapanga barabarani, wengine wanazunguka nazo mtaani, taifa litakuwa la wa wachuuzi, taifa likisha kuwa machinga wengi, serekali haipati kodi yake, hatuwezi ijenga nchi kwa uchuuzi, lazima tuwe na biashara rasmi serekali ipate kodi yake.
Tumeshudia baadhi ya maeneo wameweka biashara mpaka kwenye nyumba za watu.
Ukipita maeneo ya pale kariakoo barabara ya msimbazi ni vurugu tu wanazua maduka, wanauza bidhaa ile ile inayouzwa dukani ilo hali yeye halipi kodi.
Mwisho sasa ni wakati wa kuwatafutia maeneo rasmi lakini serekali iweke mikakati ya kuhakikisha tunaondokana na hili wimbi la kuzalisha wachuuzi.