Rais Samia Suluhu akizungumza na Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala D. Harris

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamala D. Harris, Makamu wa Rais wa Marekani, leo Aprili 15, 2022 katika Ikulu ya Washington DC Nchini Marekani.

"Utawala wetu umedhamiria kwa dhati kuimarisha ushirkiano na Tanzania na nchi za Kiafrika kwa ujumla" - Kamala Harris

“Nashukuru sana uwepo wangu hapa, nashukuru sana Makamu wa Rais kwa kunikaribisha hapa, hii ni mara yetu ya kwanza tunakutana, hivyo natumia nafasi hii kumpongeza Rais Joe Baden na wewe pia Makamu wa Rais kwa kushinda uchaguzi mwaka 2020,” – Rais Samia

“Tanzania tilikuwa tunafuatilia uchaguzi wenu, kwa mara ya kwanza kulikuwa na mwanamke katika nafasi ya kuwa Makamu wa Rais, hilo lilituvutia.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania naipongeza Serikali ya Marekani kwa msaada mkubwa wa maendeleo ambao mmekuwa mkitupatia kupitia USAID kwa miaka mingi hasa katika maendeleo ya kijamii,” Rais Samia.

“Kuhusu Covid-19, Nchi yangu ipo katika hali nzuri na imekuwa ikipata msaada kutoka Marekani, kuna chanzo zaidi ya dozi milioni tano ambazo tumepata kutoka Marekani.

“Kuhusu haki za binadamu na demokrasia, Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala hayo, ambapo tumefanya juhudi kubwa kuhakikisha kuna umoja, mshikamano na heshima kwa Watanzania wote,” Rais Samia.

"Kuhusu biashara na uwekezaji, tunajua tunatakiwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara, Serikali yangu inashirikiana na sekta binafsi, ninachoomba ni Marekani kushawishi sekta binafsi kuja Tanzania kufanya biashara na sisis, tunawakaribisha sana," Rais Samia.

“Napenda pia kukutaarifu Makamu Rais kuwa nikiwa hapa Marekani, nitazindua The Royal Tour ambayo ni programu inayolenga kuonesha uwezo wa Tanzania katika sekta za Utalii na Uwekezaji," Rais Samia.

“Kuichagua Marekani kuwa sehemu ya kufanya Uzinduzi si bahati mbaya, tulifanya hivyo makusudi, lengo ni kuufanya mradi uonekane duniani kote, ili watu wengi wafike Tanzania kutembea,” Rais Samia.
 
Naona wameililia sana nafasi hii ya 'photo op', mwishowe wamepewa fursa.

Sasa sijui ni kipi wanakitafuta!
 
Pongezi kwa Mhe. Rais Samia na Makamu wa Rais wa Marekani.

Hakika Rais Samia anaupiga mwingi haijawahi kutokea.

Kwa mwendo huu wa Mhe. Rais Samia tutegemee mambo makubwa sana kwa maendeleo ya Nchi yetu.
 
Wakati Rais Obama amekuja Tz na kuitembelea ikulu ya Magogoni alitoa speech nzuri sana ambayo wasaidizi wa JK hawakuweza ku-grasp. Obama alisema, its high time kwa Afrika kuona namna ya kufanya biashara na US.

Leo madam SSH kapata fursa ya kukutana na VP Kamala Harris, bila shaka msingi wa mazungumzo yao pia ungejikita kwenye namna ya Tz kufanya biashara na US kwenye mambo kadhaa kama vile namna ya TIB na TADB kupata mikopo nafuu kwenye IFC na other investment banks ili Tanzania ikuze exports ya processed and packaged consumables kama Korosho, cocoa, textile products na vingine vingi ili tupate forex zaidi, tutapanua tax base na kuwekeza kwenye sekta zingine ambazo zitasisimua biashara na kukuza uchumi.

Hatuwezi kumpangia mkulu nini asemezane na wakubwa wenzie, ila kama angeweza kudandia input ambayo Obama alichokoza akili zetu, kuna pahala tungetoboza.

Otherwise mazungumzo ya kutokuwa na element kuweka mechanism ya kuwa na nyavu za kuvua samaki wetu wenyewe, instead tunapewa samaki kila siku, sio afya sana kwa taifa.

Kila la heri mkulu kwenye ziara US
 
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kamala D. Harris, Makamu wa Rais wa Marekani, leo Aprili 15, 2022 katika Ikulu ya Washington DC Nchini Marekani.

“Nashukuru sana uwepo wangu hapa, nashukuru sana Makamu wa Rais kwa kunikaribisha hapa, hii ni mara yetu ya kwanza tunakutana, hivyo natumia nafasi hii kumpongeza Rais Joe Baden na wewe pia Makamu wa Rais kwa kushinda uchaguzi mwaka 2020,” – Rais Samia

“Tanzania tilikuwa tunafuatilia uchaguzi wenu, kwa mara ya kwanza kulikuwa na mwanamke katika nafasi ya kuwa Makamu wa Rais, hilo lilituvutia.

“Kwa niaba ya Serikali ya Tanzania naipongeza Serikali ya Marekani kwa msaada mkubwa wa maendeleo ambao mmekuwa mkitupatia kupitia USAID kwa miaka mingi hasa katika maendeleo ya kijamii,” Rais Samia.

“Kuhusu Covid-19, Nchi yangu ipo katika hali nzuri na imekuwa ikipata msaada kutoka Marekani, kuna chanzo zaidi ya dozi milioni tano ambazo tumepata kutoka Marekani.

“Kuhusu haki za binadamu na demokrasia, Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala hayo, ambapo tumefanya juhudi kubwa kuhakikisha kuna umoja, mshikamano na heshima kwa Watanzania wote,” Rais Samia.

"Kuhusu biashara na uwekezaji, tunajua tunatakiwa kutengeneza mazingira rafiki ya biashara, Serikali yangu inashirikiana na sekta binafsi, ninachoomba ni Marekani kushawishi sekta binafsi kuja Tanzania kufanya biashara na sisis, tunawakaribisha sana," Rais Samia.

Kaenda kupiga picha tu, hakuna cha kuzungumza hapo
 
Mama anatema yai la dunia ya kwanza, angekuwa yule jamaa Sasa hivi wakenya na waganda wangekuwa wanavurumusha matusi tu kwa lugha mbovu
 
Tanzania : Royal Tour imeuzwa mbele ya madame Mh. Kamala D. Harris

Ahadi gani zimetolewa na pande mbili yaani US na Tanzania.

Pia Mh. Kamala D. Harris makamu wa rais wa US amesema nini baada ya mazungumzo yao ya faragha ambapo press release kamili itatolewa baadaye na Ikulu ya Marekani ya White House.

Tutege masikio baadaya ya kusoma taarifa hii ya Ikulu Mawasiliano ya Tanzania juu ya mapokezi mazuri na agenda alizozibainisha Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya mazungumzo yao rasmi wakiingia faragha na wajumbe wao.
 
Inatusaidia nini sisi ikiwa sabuni tu B29 ni sh 600 siku hizi.Upumbavu ni kupost na kusifu samia kukutana na harris huku maisha yanazidi kuwa magumu kila uchwao, yapi majukumu ya serikali kwa wananchi wake? Ni kuzurura kama anavyofanya samia?
 
Wakati Rais Obama amekuja Tz na kuitembelea ikulu ya Magogoni alitoa speech nzuri sana ambayo wasaidizi wa JK hawakuweza ku-grasp. Obama alisema, its high time kwa Afrika kuona namna ya kufanya biashara na US.

Leo madam SSH kapata fursa ya kukutana na VP Kamala Harris, bila shaka msingi wa mazungumzo yao pia ungejikita kwenye namna ya Tz kufanya biashara na US kwenye mambo kadhaa kama vile namna ya TIB na TADB kupata mikopo nafuu kwenye IFC na other investment banks ili Tanzania ikuze exports ya processed and packaged consumables kama Korosho, cocoa, textile products na vingine vingi ili tupate forex zaidi, tutapanua tax base na kuwekeza kwenye sekta zingine ambazo zitasisimua biashara na kukuza uchumi.

Hatuwezi kumpangia mkulu nini asemezane na wakubwa wenzie, ila kama angeweza kudandia input ambayo Obama alichokoza akili zetu, kuna pahala tungetoboza.

Otherwise mazungumzo ya kutokuwa na element kuweka mechanism ya kuwa na nyavu za kuvua samaki wetu wenyewe, instead tunapewa samaki kila siku, sio afya sana kwa taifa.

Kila la heri mkulu kwenye ziara US
I hope there is trade mission in the entourage. As citizens we are ignorant of the itinerary
 
Back
Top Bottom