Rais Samia Suluhu amteua Jaji Jacob Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

Rais Samia Suluhu amteua Jaji Jacob Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

Hivi ni kigezo gan kinatumika kuteua majaji tu? Au kwa sbb wanatokea mahakaman kwenye " kutoa haki"? Halaf majaj ndo wa kina mustafa sihami?
 
Raisi wa JMT ambaye ni Mwenyekiti chama tawala anajua wazi kabisa ikiwepo katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi anaweza akashindwa na yeye keshoonja madaraka hawezi kukubali Hilo litokee.Kwa hiyo wataendelea na haya mambo ya teuzi zenye tija kwake mpaka siku watanzania wakichoka.
Katiba Mpya na tume huru ya uchaguzi sio kipaumbele Cha CCM!
 
NEC inayofanya kazi kwenye ngazi ya taifa tu,huku chini ni cadres wa chama dola ndio wanaendesha so called uchaguzi
 
... sasa hiyo Kamati ya Mutungi ya kusaka kinachodaiwa NEC huru ni ya nini hasa? Kamati iliyojaa makada wa CCM 100%! Bila Katiba Mpya hatutoki.
Maigizo yaendelee............ Halafu bado wanataka waheshimiwe wakati wameshindwa kujiheshimu.
 
Dah hili jicho langu sijui vipi..yaani zaidi ya uchama naona na ...haya majina mmmh!
 
Huyu alikuwa mjumbe wa NEC ile ile iliyovuruga uchaguzi na kupora kura , hatakuwa na jipya , Sasa ndio muelewe kwamba kile kikao cha Mutungi na akina Zitto , Lipumba na mamluki wengine hakikuwa na maana yoyote .

Hii ndio Tume huru ya uchaguzi ?
Hivi kwa akili yako mnategemea tume huru ije kama zawadi ya birthday? Mwaka 2020 mlipata mbunge mmoja, 2025 mnaweza kupata madiwani 3 na hakuna kitu mtafanya.
 
Hivi kwa akili yako mnategemea tume huru ije kama zawadi ya birthday? Mwaka 2020 mlipata mbunge mmoja, 2025 mnaweza kupata madiwani 3 na hakuna kitu mtafanya.
Uongozi wa sasa ni njia Muhimu ya kapata katiba mpya. Hata Sisi CCM tunaliona hilo. Mfano Kwa sasa viongozi wote wakuu ni Chaco la Katiba Sio wananchi wala wa CCM
 
Rais Samia Suluhu amemteua Jaji Jacob Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akichukua nafasi ya Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, Semistocles Kaijage ambaye amemaliza muda wake.

Jaji Mwambegele ni Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa NEC.

View attachment 2059505
 
Huyu alikuwa mjumbe wa NEC ile ile iliyovuruga uchaguzi na kupora kura , hatakuwa na jipya , Sasa ndio muelewe kwamba kile kikao cha Mutungi na akina Zitto , Lipumba na mamluki wengine hakikuwa na maana yoyote .

Hii ndio Tume huru ya uchaguzi ?
Huna taarifa. Mhe. J. Mwambelege hajawahi kuwa sehemu ya menejimenti ya kusimamia uchaguzi Mkuu wowote Tanzania.
Acha kuzusha
 
Back
Top Bottom