Rais Samia Suluhu apokea andiko la ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027

Rais Samia Suluhu apokea andiko la ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amepokea andiko la Ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027, kutoka kwa Rais wa TFF Wallace Karia pamoja na Uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Mei 2023.

Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda kupitia Pamoja Bid wamedhamiria kuwa mwenyeji wa michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (African Cup of Nations) 2027.

Rais Samia amesema nchi hizo zinawania nafasi hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Michezo imepata, hivyo kuwa wenyeji wa AFCON 2027 kutaongeza hamasa zaidi kwa ukuaji wa michezo hususan soka.
Aidha, Rais Samia amesema michuano hi itachangia katika ukuaji wa utalii kwa kuwa ni mashindano ambayo hutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja Barani Afrika na maeneo mengi duniani kwa ujumla.
Fw48XGRakAAONxM.jpeg

MC19.jpg


MC14.jpg


===​
Rais wa Jarnhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiaa na Kenya na Uganda kupitia Pamoja Bid wamedhamiria kuwa mwenyeji wa michuano ya Fainali za Kornbe la Mataifa ya Afrika (African Cup of Nations) 2027.

Rais Samia amesema nchi hizo zinawania nafasi hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa ambayo Sekta ya Michezo imepata, hivyo kuwa wenyeji wa AFCON 2027 kutaongeza hamasa zaidi kwa ukuaji wa michezo hususan soka.

Aidha, Rais Samia amesema michuano hii itachangia katika ukuaji wa utalii kwa kuwa ni mashindano ambayo hutazamwa na zaidi ya watu bilioni moja Barani Afrika na maeneo mengi duniani kwa ujumla.

Vile vile, Rais Samia amesema mashindano hayo yataleta watu mashuhuri nchini wenye ushawishi duniani hivyo huwezesha na kunufaisha sekta nyingi za uchumi ambapo huchangia ajira, mapato kwa wafanyabiashara na serikali.

Kwa upande mwingine Rais Samia amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imeshafanya utafiti na kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Mashindano ya AFCON yataweka rekodi kwa mara ya kwanza kufanyika katika Ukanda wa Afrika Mashariki tangu yalipoanzishwa rasmi mwaka 1957.
 
Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda kupitia Pamoja Bid wamedhamiria kuwa mwenyeji wa Michuano ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (African Cup of Nations) 2027

Rais Samia Suluhu amesema Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, imeshafanya utafiti na kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo

Hii itakuwa mara ya kwanza kufanyika kwa Mashindano haya katika Ukanda wa Afrika Mashariki tangu yalipoanzishwa 1957


IMG_4786.jpg
 
Anaupiga mwingi itasaidia watumishi wenye mishahara midogo
 
ni jambo jema.
ila kwa sasa tuna viwanja vya kisasa vitatu;

1. Benjamin Mkapa stadium
2. Uhuru stadium
3. Chamanzi complex.

Hivyo Serikali inapaswa ijenga kiwanja kingine cha kisasa nje ya Jiji la dsm.
 
Karibu theluthi mbili ya watu wanaishi chini ya dola moja kwa siku sasa ni nani atakayeenda viwanjani kutizama hizo mechi.

Samia amekuwa rais asiyejali kabisa maendeleo na badala yake ameingilia mambo ya kipuuzi kabisa ili kujaribu kusahaulisha watu na madhaifu ya utawala wake.

Huyu inatakiwa 2025 aende kabisa nyumbani kwani uongozi umemshinda kabisa.
 
Karia na timu yako pamoja na wizara ya utamaduni, sanaa na michezo kuna mengi sana ya kufanya kabla ya hili tazama tu uwekezaji gani wa maana katika mpira tumefanya kuanzia miundombinu (viwanja, academies) au tunarukia tu ili nasi tuonekane tunaweza? Tulishawahi kuwa na timu ya vijana iliyoshiriki kombe la COPA Cocacola kama sikosei na kufanya vizuri wakaishia kutelekezwa hatuna budi kufanya mengi sana ya awali kabla ya kuanza kurukia haya sio wazo baya ila hatujawa tayari kwa vigezo vingi kuandaa michuano hii
 
Tanzania Kuomba kuwa Mwenyekiti wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027.

20230524_200209.jpg
 

Attachments

  • 20230524_200209.jpg
    20230524_200209.jpg
    79.5 KB · Views: 3
Kila la heri, ila hali ya upatikanaji wa dolar ni changamoto kubwa huko Burundi🥛😅🙏
 
Rais Samia Suluhu Hassan akipokea andiko la Ombi la Tanzania, Kenya na Uganda kuwa mwenyeji wa AFCON mwaka 2027, kutoka kwa Rais wa TFF Wallace Karia pamoja na Uongozi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 24 Mei 2023.

20230524_201338.jpg
 
Back
Top Bottom