Rais Samia Suluhu awaapisha Mabalozi Ikulu. Asema Tozo za Miamala zitaendelea ila zitarekebishwa

Rais Samia Suluhu awaapisha Mabalozi Ikulu. Asema Tozo za Miamala zitaendelea ila zitarekebishwa

Tozo zitaendelea ?, kwani nani alisema zisiendelee.., zitarekebishwa lini na vipi ? Hapo ndio kuna tatizo.., kila siku zinavyozidi kwenda na huu muendelezo ni hasara kwa biashara za watu (no body is gaining)
Habari kamili subiri saa mbili tbc utapata jibu kamili
 
Kwamba tozo zinazoongezeka inaenda kutumika kujenga Barbara vijijini na huduma ya maji,sasa unajiuliza kodi inayokusanywa inapelekwa wapi??
Vilaza kama wewe ndiyo washauri wa Abubakar, so ukiwa na source moja ya income unaridhika na kuanza kucheza bao?
 
Rais kasema suala la miamala litakuwepo pale pale japo kurakuwa na unafuu kigog.

Lakini kazungumzia barabara mbovu vijijini na ukosefu mkubwa wa maji. Mwigulu alikuwa sahihi kututaka tuhamie Burundi
Sasa ndio umeandika nini mkuu. ''kurakuwa, kigog'' ni kiluga gani mkuu
 
kama kasema hayo kuhusu tozo baada ya kuchanjwa basi hii chanjo ina madhara makubwa.
 
Ahsante sana Rais wangu kwa msimamo THABITI kwa mwendo huu tutafika vizuri.

nadhani wanao pima kina cha maji kwa rula bado hawajui kina vizuri.

nafurahia sana makato haya yaendelee kama kawaida watazania wengi wanataka kero zao za maji, elimu, afya na miundombinu itatuliwe na sote tuko tayari kuchangia maendeleo yetu, marekebisho kidogo tu.

kazi iendeleee.

tulipe tozo kwa maendeleo yetu ss wenyewe.

Mungu ibariki Tanzania
 
Why Mama anaapisha mabalozi wengine wasio na vituo? Wanapewa posho, mishahara na magari ya gharama kubwa.

Mwisho wa siku kina Togolani wanashinda Twitter kupost meme.
Exactly.
 
hivie ule mpango wa kuligawa jiji la dar bado upo???
Mwendazake wakati anafanya yale maamuzi kichwa ilikuwa imeshavurugika, maana siku 2 later ndiyo akapotea mazima, pamoja na yote aliyofanya mabaya na mazuri I miss the guy sometimes
 
Mama yupo kwa ajili ya Tanzania, na Tanzania ipo kwa ajili ya mama. Tukiacha kutumia akili tulizopandikizwa na magaidi, tutamuelewa sana bimkubwa. Mama ni mtu wa haki, na ameamua kuisimamia haki bila kujali nani anasema nini.
Haki dhuluma
 
Back
Top Bottom