Rais Samia Suluhu awasili nchini Korea Kusini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol

Rais Samia Suluhu awasili nchini Korea Kusini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea, Yoon Suk Yeol

kizi kid

Member
Joined
Dec 7, 2023
Posts
15
Reaction score
18
Rais Samia Suluhu awasili nchini Korea Kusini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Yoon Suk Yeol. Ikumbukwe kuwa Korea ni moja ya washirika wakubwa wa maendeleo tangu tarehe 30 Aprili 1992.

Uhusiano wa Tanzania na Korea umegusa maisha ya wananchi moja kwa moja na lazima na no muhimu kufanya kazi ya kuukuza na kuuongezea tija zaidi. Rais Samia amesema Baadhi ya miradi mikubwa ambayo Tanzania na Korea wameshirikiana kuifanikisha ni pamoja na Daraja la Mto Malagarasi, Daraja la Tanzanite na Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila.

Vile vile Ziara hiyo inatarajiwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa kazi ya Diplomasia ya Uchumi, na baada ya mazungumzo kati viongozi hao kutashuhudiwa utiaji saini makubaliano mbalimbali ya kukuza zaidi uhusiano yakigusa hasa sekta za uchukuzi, uchumi wa buluu, usafiri wa anga, madini ya kimkakati, utamaduni, sanaa na kilimo.

Rais Samia pia anatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa kampuni kubwa za Korea kwenye sekta za nishati, miundombinu na uandaaji wa filamu.

PIA SOMA
- Raisi Samia kafanya ziara nchini Korea ya Kusini leo 31/05/2024

Hapo roho yake kwatu kwa kula Bata yuko vzr kwakweli!!

Na hiki yuko tayri kukifanya cku zote za miaka 5 yake.

KAZI ni kipimo cha UTU
 
Rais Samia Suluhu awasili nchini Korea Kusini kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Korea, Mheshimiwa Yoon Suk Yeol. Ikumbukwe kuwa Korea ni moja ya washirika wakubwa wa maendeleo tangu tarehe 30 Aprili 1992.

Uhusiano wa Tanzania na Korea umegusa maisha ya wananchi moja kwa moja na lazima na no muhimu kufanya kazi ya kuukuza na kuuongezea tija zaidi. Rais Samia amesema Baadhi ya miradi mikubwa ambayo Tanzania na Korea wameshirikiana kuifanikisha ni pamoja na Daraja la Mto Malagarasi, Daraja la Tanzanite na Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila.

Vile vile Ziara hiyo inatarajiwa kuwa ni sehemu ya utekelezaji wa kazi ya Diplomasia ya Uchumi, na baada ya mazungumzo kati viongozi hao kutashuhudiwa utiaji saini makubaliano mbalimbali ya kukuza zaidi uhusiano yakigusa hasa sekta za uchukuzi, uchumi wa buluu, usafiri wa anga, madini ya kimkakati, utamaduni, sanaa na kilimo.

Rais Samia pia anatarajiwa kuwa na mazungumzo na viongozi wa kampuni kubwa za Korea kwenye sekta za nishati, miundombinu na uandaaji wa filamu .
Tunaofurahia hii ziara ni wapenzi wa tamthilia za Kikorea, raha sana.
 
Wahuni sio watu wazuri, wanamzururisha bi ushingi kama lile roboti Eunice la Nape ili wapige posho kilainiiii.
Safari zisizo na matokeo chanya kwa nchi bali matumbo yao
 
Mama yupo vizuri,South Korea ni kigogo wa uundaji wa meli,mitambo ya akila aina.Walete kwenye LNG project direct bila kupitia kwa mawakala wataijenga tena kwa viwango in short period.
Mama usisaukutembelea Bosun jiji la viwanda.
 
Hapo roho yake kwatu kwa kula Bata yuko vzr kwakweli!!

Na hiki yuko tayri kukifanya cku zote za miaka 5 yake.

KAZI ni kipimo cha UTU
Kwa akili zako unaona kaenda kula bata!?..Marais wa marekani toka 1998 walikuja hapa isipokua Biden na trump tu,walikuja kula bata!?.. Erdogan alikuja, Marais wawili wa china wamekuja hapa,walikuja kula bata!?..Korea anajenga upya muhimbili na rais wao kamualika Samia,we unaamini wamealikana kula bata!!?..punguwani wahed
 
Analipiza, wakati wa Magufuli alikuwa anapimiwa safari za uwakilishi, sasa anakomoa, anasafiri kila siku mwisho atakosa pa kwenda ataenda mbinguni.
Shirika letu linapata hasara kila siku, wao husafiri hata sehemu za kupiga simu wao wanaenda na ndege bure.
 
Huyu alifaa kuwa mfanyakazi wa kawaida wa wizara ya mambo ya nje, siyo hata waziri
Kwani wenzetu mnazitafsiri vipi ziara za nje za Rais? Kwani mnadhani Mbowe na Lissu wasingefanya ziara za nje, Chadema ingeweza kusimama kwa ruzuku?

Hilo daraja la Tanzanite mlilokuwa 'mkidanganywa' limejengwa kwa hela za ndani, mnajisikiaje kujua kwamba South Korea iliweka hela pale hadi kukamilika kwake?

Kufanya mazungumzo na viongozi wa kampuni kubwa za Korea kwenye sekta za nishati, miundombinu na uandaaji wa filamu ni jambo kubwa kwa kupanua wigo wa ajira kwenye sekta hizo.

Na mazungumzo hayo yanaweza kuzaa ushirikiano utakaokuza teknolojia, utalii, kuwekeza katika studio za filamu nchini na ujenzi wa Chuo cha Filamu cha Taifa.

Kila siku tunalalamikia uwezo wa filamu zetu, mnadhani tunawezaje kupandisha uwezo bila ya kushawishi walioendelea kusaidia kutoa elimu kwa wasanii wetu?

Pia, sote tunajua kama tuna mfumo wa kizamani wa kutangaza maeneo yetu ya utalii, ndiyo maana tunapitwa mapato ya utalii na vinchi kama Rwanda.

Sisi tuna aina zote za utalii, lakini Mongolia wenye utalii wa Utamaduni tu wanatupita kwa mapato, kwa hiyo naona haya mazungumzo ya Rais na kampuni kubwa za kule, yanaweza kutatua shida hii.

Pia, Rais atashiriki Jukwaa la Afrika na Korea (Korea-Africa Summit) linalowaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika na Serikali ya Korea, na kushirikishana uzoefu na mikakati katika usalama wa chakula na madini.

Hili ni jukwaa muhimu sana kwa sisi tunaolima mazao ya chakula na tuna aina kadhaa za madini, huwezi kupuuza ushiriki wetu kwenye jukwaa hili, ambalo Rais wetu atapata nafasi ya kuhutubia.

Hivyo, siyo kila ziara ni za kuzilaumu tu, hata kama zina tija kama ziara hii. Zipo ziara tunazoweza kusema hazina tija, lakini siyo hii.

Ova
 
Back
Top Bottom