Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,710
- 9,063
Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan(SSH), awali ya yote na kwa moyo wa dhati kabisa nikupongeze kwa kuapishwa kuwa Rais wa 6 wa JMT. Watz wanajua huu ni mpanho wa Mungu.
Wewe ndiye ulikuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba,(BMK) mkiwa na marehemu Samwel Sitta. Mchakato ulifanyika, tukapata Rasimu ya Katiba na KATIBA PENDEKEZWA. Kama nakumbuka vizuri zilitumika Fedha za walipa Kodi wa Tanzania takribani Tshs. 270 Billioni.
Hayati JPM alipoingia madarakani yeye akadai swala la KATIBA MPYA halikuwa kipaumbele chake wala halikuwa kwene Ilani ya Uchaguzi!!! Sijui kama halikuwa swala la Ilani ilikuwaje Serikali ya CCM A4 chini ya Mhe. Jakaya Mrisho Kikwerte iliamua kutumia mabilioni yote hayo kuwalaghai Watanzania.
Maadamu wewe sasa ndio uko Ikulu jikoni, ni wakati wa kukamilisha upishi huu au mchakato wa KATIBA MPYA. Napenda niku hakikishie kuwa hiyo itakuwa ni zawadi yako kwa Watanzania itakayo kujengea Heshima kubwa sana! Hakika Itakuwa ni alama utakayo waachia Watanzania na wata kukumbuka daima milele ikizingatiwa kuwa wewe ni Rais Mwanamke wa Kwanza Tanzania tangu tupate Uhuru.
Asalaam Aleikum