Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Eric Hamisi ndiye Mkurugenzi Mkuu wa TPA sasa.
 
Angalizo
Pale TPDC aliyewekwa ana ujuzi upi? isiwe mambo binafsi yamemtoa aliyepo maana panahitajika wanaoweza ku-negotiate mambo ya gesi kwa maslahi ya nchi! Dr Matarajio kafanya lipi baya? Au atakuwa kizingiti cha wanaowania vitalu?
 
Najua ni mahitaji ya lazima ya sasa ila naona kama NCHI, tunatumia muda mwingi kuteua, kuapisha na kujadili nyazifa za wanasiasa na watendaji wa serikali. Haya mambo ukiyatafakari sana utagundua hayatuongezei tija kihivyo na yanatupotezea muda na kutuingiza gharama nyingi zisizo na maana sana.

Ila huo ni mtazamo wangu tu.
Kweli na wananchi tunashabikia ki uhemko bila kujua faida yake au hasara.......kwasababu kuna watu wametimuliwa na wengine wamepata
 
Ado ado ndio mwendo. Hata wale mateja kule sober house nasikia huwa wanapewa dawa kidogo kidogo mpaka wananyimwa kabisa.

Ujue hii mdogo mdogo ndio tamu maana mwisho wa siku jamaa hasikiki tena.
 
Back
Top Bottom