Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Aisee kumbe tuna safari ndefu kweli kweli,mi nilijua tupo katikati ya njia,kumbe ndo kwanza tunaanza kuvaa viatu vya kutembea katika safari yetu hii pendwa ya kuvuka upande wa pili wa njia...
 
Mama Samia hapo TPDC kaharibu ,aliekuwepo si tu ana akili bali ni mzalendo namba moja wa hapa nchini ,kama sio yeye wachina walishakwapua vitalu vya gesi bure baada ya kupewa na Muhungo ,yeye alikomaa hadi kusimamishwa kazi
Mkuu Makupa heshima yako.
 
Mama Samia hapo TPDC kaharibu ,aliekuwepo si tu ana akili bali ni mzalendo namba moja wa hapa nchini ,kama sio yeye wachina walishakwapua vitalu vya gesi bure baada ya kupewa na Muhungo ,yeye alikomaa hadi kusimamishwa kazi
Hata tra kaharibu.
 
Kwanini Wizara ya Mifugo ina makatibu wakuu wawili na hakuna naibu?
Nadhani itakuwa ni Typo tu. Hapo huyo wa chini ni Naibu Katibu mkuu(nikiangalia kwa mpangilio huko juu)

Au pia inawezekana zile wizara kubwa wanachagua makatibu wakuu wawili(kisekta) kama Uchukuzi KM wake na Ujenzi inakua na KM wake

Ila inakera sana hii taarifa ina makosa mengi sana sijui kwanini huwa hawafanyi Proof reading kwa taasisi kubwa kama Ikulu

Naona kuna mtu hapo jina Twalib wameandika kwa capital TWalib halafu na jina la Mtoto wa Mkapa Nico wamekosea Anaitwa Merinyo wao wameandika vitu gani sijui
 
Kashuka kuwa msemaji wa serikali? Toka kuwa msemaji wa taasisi moja na kuwa msemaji wa nchi nzima Kashuka? Duuuh mei bii kuna pasipekitivu inaangaliwa, ila kapanda cheo
Kuna mmoja anasema atakua anasoma tu magazeti ofisini sababu hamna cha kufanya, Serikali iko bize kila siku hukosi la kusema...
Hizo ni chuki tu..
 
Tutapiga mark time sana kwa katiba hii mfumo huu uliojichokea.
Waliochabaki nacho raia "fulani mtu sana", "fulani jembe", "mkunaji amepata upele" "fulani kaula" na blah blah nyingine nyingi zisizo na kichwa wala miguu kwa miaka yote.
Tutoe mapendekezo, mfumo imara uwe vipi?Tufute nn? Tuboreshe wapi? Wapi tupaache kama palivyo?
 
Back
Top Bottom