Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Hapana

Mmoja uvuvi na mwingine Mifugo hamna naibu pale.
Nimeandika possibility mbili mkuu unasema Hapana kwa IPI?? Nimetoa na mfano wa Wizara ya Ujenzi & Uchukuzi napo wako wawili hivyo hivyo
 
Ukiwa msukuma na uko juu tegemea watu wa kaskazini kukushabulia kwa tuhuma feki..
Kweli kabisa. Yaani Kigogo anawajengea watu chuki kiasi kwamba kuna mtu hata si mtumishi,si mfanya biashara yaani anamchukia Dotto kanakwamba alimkamata akiiba hizo hela. Tuache haya mambo.

Unaweza kumchukia mtu kwa sababu za mtu mwingine ambaye wewe hujui yeye anamchukia mtu huyo kwanini.

Pia,kwanini watu wanampangia Rais watu wa kuteua?

Yaani nchi hii imefika mahali pa ajabu sana.

AWAMU YANGU MTANYOOKA. KUMBUKENI HII ID YANGU. NITAWAKUMBUSHA.
 
JPM atabaki kuwa mwamba aliyejenga viongozi imara akiwemo rais SSH na VP
Usinipangie eti kwamba simkubali
Na Kama hilo linakuuma kajinyonge
Wengi wameanza kubweka baada ya JPM kuondoka, bado JPM atabaki mwamba hata mufanyeje kama ilivyokuwa kwa Nyerere basi ndivyo kwa JPM hakuna wa kumlinganisha naye itachukua miaka mingi sana labda kizazi kingine.
 
Hakuna mapendekezo zaidi ya kurejea katika rasimu ya Katiba ya Warioba. Hiyo ndiyo itakuwa msingi wa taasisi Imara na kuondoa mrundikano wa madaraka kwa mtu mmoja.
Tutoe mapendekezo, mfumo imara uwe vipi?Tufute nn? Tuboreshe wapi? Wapi tupaache kama palivyo?
 
Kashuka kuwa msemaji wa serikali? Toka kuwa msemaji wa taasisi moja na kuwa msemaji wa nchi nzima Kashuka? Duuuh mei bii kuna pasipekitivu inaangaliwa, ila kapanda cheo
Taasisi moja sio!? Hivi unaelewa ukubwa wa hiyo Taasisi unayoizungumzia!?

Unajua kwanini kwenye orodha ya Makatibu Wakuu, yule Katibu Mkuu wa Ikulu kwanini amewekwa wa kwanza?

Msemaji wa Serikali ni Idara iliyo chini ya Wizara ya Habari. Ila Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais ni Kurugenzi iliyopo Ikulu. Fanya kuoanisha mwenyewe ujue nani mkubwa wa mwenzake hapo.
 
Kuna ma RC na Ma DC wa hovyo sana Mbeya, Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Hai na Pwani. Piga kalamu hao
 
Hivi watu ni kwamba kusoma hamjui au tatizo nini? Msigwa kabaki pale pale zaidi kaongezewa majukumu
Sio kweli, Awali alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu na sasa hivi anakuwa mkurugenzi wa idara ya habari maelezo ambayo ipo chini ya Wizara ya habari. Ametoka ikulu
 
Kiukweli Bado upande wangu Siamini kama Msemaji wa Ikulu Ofisi MOJA tu Anaweza kuwa Mkubwa kimamlaka na kimaslahi Kumzidi MSEMAJI MKUU WA SELIKALI. ninavyojua Mimi Msemaji wa Ikulu Hawezi kwenda kuongea Issue yoyote inayohusu wizara yoyote au Tukio lolote la Kitaifa Yeye Atasubiri issue ya Ikulu tu.

Mfano. Kipindi cha Corona imepamba moto waliokuwa wamepewa mamlaka ya kuliongelea alikuwa Rais,MAKAMU, Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na MSEMAJI WA SELIKALI..

Sasa leo mtu Akiniambia Msemaji wa Ikulu ana Cheo Kikubwa Kuliko MKURUGEZI WA HABARI MAELEZO NA MSEMAJI MKUU WA SELIKALI Bado inashindwa kuniingia Hebu wataalamu waje Wanifafanulie.. Binafsi naona Msigwa Hajashushwa Cheo.. labda kukosa mapocho pocho ya Ikulu.
 
Ninyi remnants wa Mataga mnapenda mambo yafichwefichwe ili Upigaji wenu wa kishamba usijulikane....
Yawezekana kweli ni mtu mwema kwa nchi yetu sikatai. Ila asiifanye chuki yake kwa watu wengine iwe ndiyo chuki ya nchi nzima kwa watu anaowachukia yeye.

Yapo anayootea na yanakuwa....ila kuna pengine anaenda chaka mazima. Ila asimpangie mtu watu wa kufanya nao kazi. Naona yeye ni yule anayetaka mtu aharibikiwe ili apate wakumbeza.
 
Watu wamemkariri Kigogo sana. Wakati hapa hata hajajuwa kama kuna uteuzi leo. Nimeona anaotea mama anaenda Zenji kumbe maza anakamua uteuzi Dar.
Watu wamekuwa hawamsomi vizuri.

Alisema Lawrence Mafuru na Nehemiah Mchechu watateuliwa...Ameangukia pua!

Naona sasa hivi ana hasira na mama! Majina yote toka VP amekuwa amekosea!!
 
Back
Top Bottom