Rais Samia Suluhu Hassan: Alama ya mwisho ya anguko la Utawala wa CCM, Tanzania

Ha hahahaaaaa,dah wewe nakujua toka ungali katoto ulikuwa kaongo kama shetani, sa hivi ndio naona umebobea kabisaaa.
 
Kwa wanaofahamu huu ndo mwisho wa CCM .kuna mabadiliko makubwa yanakuja na kwa Kasi kubwa mno .Nawaambia wenye masikio na wasikie.Viongozi wote wa kuteuliwa kuweni na heshima kwa kila mtu maana mnaemtukana Leo kesho atakua boss wenu .
 
Mama hatagombea na Hilo analifahamu
 
Huwezi kuingia msikitini ukasema "Bwana Yesu Asifiwe" au ukaingia kanisani ukasema "Takbir mwenyeji wakakuitikia ʾAllāhu ʾakbarᵘ, zaidi wakikuheshim watakutoa nje sehemu zingine unaweza jikuta mwili wako unamaumivu makali

Samia anataka kuleta utamaduni ambao haupo CCM toka imeanzishwa mwaka 1977 sasa unapoleta utamaduni mpya sehemu kuna mawili ww kufail au watu kukufelisha coz kila kitu kwao kitakuwa kigeni
 
Siku hizi mnajitahidi Sana kutishia nyau utafikiri mnaongea na watoto
 
Ndugu unamaanisha nini? Mabadiliko gani ? Yan kwa ccm hii ianguke ni ngumu sana kibinadamu kuwaza kua IPO siku ccm inaweza kuanguka ,japo kwa Mungu kila kitu kinawezekana.
 
Endelea kuota ndoto nyevu wakati ukitembea mchana jua kali na bahasha ya ajira
 
Okay. Sabay Yuko wapi? Lolote laweza kutokea.
 
Ndugu yangu inawezekana kuna baadhi ya ulioyasema yakawa na ukweli fulani lakini ukweli wa mambo kwa hivi sasa hakuna chama chochote cha upinzani kinachoweza kuishinda CCM nasema tena hakuna hivi vyama tulivyonavyo viongozi wapo kwa ajili ya matumbo yao tu.

Mpaka sasa Viongozi wa vyama vya upinzani wanategemea huruma ya CCM harafu unasema kuna mpinzani wa kuchukua Nchi hapo? Asilimia90 ya viongozi wa upinzani wapo tayali kuludi CCM ilimradi tu ahakikishiwe kuwa atapewa/atapata cheo kwa hiyo kufikili au kudhani kuwa hawa viongozi wa sasa wa upinzani wanaweza kuchukua Nchi ni kujidanganya na ni sawasawa na kuota ndoto za mchana

Ule morali uliokuwepo kwa Wananchi miaka 6 iliopita umepungua sana haswa baada ya wapinzani kukubali kununulika kama bidhaa Wananchi wengi wameshawagundua kuwa hao ni njaa tu
 
Nakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa...

Kuna kosa likifanyika tu 2025, hiki nilichokiandika hapa kitatimia bila shaka...

Itakuwaje? Tusubiri tuone wafanye kosa hili..
 
Il
Ili kuchukua nchi upinzani unahitaji kufanyiwa reform ndani na pengine uwepo wa sheria zitakazowawezesha kuungana na utashi wa kisiasa kuchukua uongozi wa nchi na hususani upinzani makini na serious kuliko ilivyo sasa. Lipo tatizo kwenye upinzani wa sasa bahati mbaya sana.
 
Nafikiria bila kupata majibu kama CCM inakubalika..

Kwanini ikatae mabadiliko ya katiba?

Hivi hata kipofu au yeyote asiyeweza kuona akisomewa baadhi ya madhaifu ya katiba hii hawezi kuacha kushangaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…