Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa, Kata ya Lupaso, Masasi Mkoani Mtwara tarehe 16 Septemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu mara baada ya kuwasili nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin William Mkapa, kata ya Lupaso, Masasi Mkoani Mtwara tarehe 16 Septemba, 2023.