Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 3,978
- 6,739
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, anatarajia kupokea tuzo ya “The Gates Goalkeepers Award” ikiwa ni kielelezo cha matokeo makubwa ambayo yamepatikana katika uongozi wake kufuatia ripoti ya utafiti wa demografia na afya ya mwaka 2022 inayoonesha kupungua kwa vifo vitokanavyo na uzazi kwa kiwango cha asilimia 80 pamoja na watoto wachanga.
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo wakati akitoa taarifa ya upokeaji wa tuzo hiyo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, zinazoandaliwa na taasisi ya The Gates Foundation, mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Wizara ya Afya, Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mhagama amesema tukio hilo linafanyika nje ya Marekani katika nchi ya Tanzania kwa mara ya kwanza na Rais Samia ndiye kiongozi wa kwanza kupata tuzo hiyo kwa bara la Afrika.
Jambo lililochagizwa na uongozi wake mahiri uliopelekea mafanikio makubwa nchini hususani katika sekta ya afya kwa kuitendea haki na kusababisha mataifa makubwa Duniani kutambua mchango wake.
Enewei! Ukiona kila unachokiongea watu wanapiga makofi mengi usidhani wanafurahi, wengine wanatoa kejeli zao kupitia makofi.