Tutu kalundji
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 532
- 1,287
Wakati Madame President, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anaingia ikulu alikuta mtangulizi wake Hayati John Pombe Magufuli akiwa kapiga hatua nzuri ila nchi ilikuwa na mzigo wa kuhudumia project nyingi ambazo zilihitaji mabilioni ya shilingi kuweza kukamilisha kwa wakati.Hapo hapo uhusiano na mahusiano na mataifa fadhili haukuwa rafiki.Rais Samia Suluhu Hassan akakuna kichwa kuangalia jinsi ya kukamilisha miradi husika mbali na vipaumbele vyake.Huu ulikuwa mtihani mkubwa wa kwanza kwa Madam President ila tunajifanya hatulioni zaidi ya kukaa tunalaumu tu.
Hayati Magufuli alisitisha ajira kwa wanachuo kutoka kada mbali mbali,hali hii iliongeza mrundikano wa vijana waliohitimu vyuo mbali mbali nchini huko mtaani.Rais Samia Suluhu Hassan kaajiri maelfu ya wahitimu na hivyo kuongeza Fursa za ajira kwa vijana.Hili hatumpongezi tumekaalia roho mbaya tu kwa kiongozi wa nchi.
Hayati John Pombe Magufuli alisitisha ongezeko la mshahara kwa watumishi wa umma(annual increment)kwa utashi wake binafsi bila kuzingatia vigezo vya kisheria,RAIS Samia tangu aingie madarakani amekuwa akiongeza mshahara kwa watumishi wa umma,kupandisha madaraja na hata mwaka huu zaidi ya watumishi 219,042 nchini wamepandishwa vyeo na hivyo mishahara yao itapanda mwezi juni.Hili hatuliongelei hata kidogo.Watanzania wenzangu tuwe fair.Mnyongeni haki yake mpeni.
Kuhusu Demokrasia,Kipindi cha Hayati Jpm ndio tuliona msururu wa wanasiasa wa upinzani upinzani wakihama vyama vyao na kujiunga CCM kwa kurubuniwa,Bunge kutokuwa live n.Samia karudisha Bunge live nk.Ndio kipindi ambacho Kiongozi wa upinzani Tundu Lissu alipigwa risasi na kunyimwa stahiki zake.Rais Samia kipindi hicho akiwa Makamu wa Rais alisafiri mpaka Nairobi na kumjulia hali.
Ulikuwa ni uamuzi mgumu sana aliouchukua Samia ila aliamua kufanya hivyo kwa upendo.Kama mnakumbuka kipindi hicho viongozi wa kiserikali na Wanasiasa hasa wa CCM walikuwa wanaogopa kwenda Nairobi kumjulia hali Tundu Lissu kwa kumuogopa Jpm ila Ssh aliamua liwalo na liwe.Na hata baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuingia madarakani aliamuru Tundu Lissu alipwe stahiki zake na pia kuamuru Wanasiasa waliokimbia nchi kurudi nchini ili tulijenge Taifa.
Sote tulishuhudia Jina Godbless Lema wakirudi kutoka uhamishoni Canada,Tundu Lissu kutoka Ubelgiji nk.Leo inakuwaje tumuite Samia adui wa Demokrasia?Siyo sawa tuweni fair,mama anajitajidi sana!
Uwekezaji wa Dp world kama wangewekeza wazungu je tungepiga kelele?Kwangu Mimi naona idadi ya wawekezaji wa kigeni iendelee kuliko wazawa.
Wazawa tuna shida nyingi mno kusimamia maeneo nyeti kiuchumi.Yaani binafsi nashauri Serikali iongeze wawekezaji wengi sana wa kigeni mfano wa Dp world kuongeza tija katika uzalishaji.
Mara ngapi tunalia kuhusu mashirika ya umma yasivyo na tija kwa Taifa,halafu tunapata mwekezaji Bado tunalaumu!Watanzania tunasimamia wapi?Tuache kupelekwa kwa mikumbo.
Suala la Rais kuteua wasaidizi wa karibu na familia nalo tulijadili kweli?Wewe unaweza kufanya kazi na mtu usiyemjua kweli,ili iweje?Ubahatishe au?Hapa Rais yupo sahihi kwa 100%Hata Marekani Trump kampa mkwewe baadhi ya shughuli nyeti kuzisimamia.Hayati Jpm mwenyewe aliteua wengi waliokuwa karibu nae.Hapa Rais yupo sawa!
Suala la October 29,2025 ingekuwa ni wewe ndie mkuu wa nchi ungeacha wanaojiita waandamaji wavunje na kuchoma maduka ya watu,kuiba,kuchoma matairi na kuzuia vyombo vya usafiri visipite barabarani?Ndio maandamano yanavyotakiwa kweli kuwa ?Ukweli uliopo katika harakati za wanausalama kupambana na nguvu ya watu hao ni lazima tu watu waumie na hata kupoteza maisha.Hapa Sisi kama Taifa tushikamane na kusimama tena huku tukiangalia namna ya kunitengenezea Tanzania imara kwa siku za baadae.
Kuhusu ufisadi mnakumbuka enzi za Hayati JPm kuringana na ripoti ya CAG kiasi cha shs trioni 1.5 hakikuonekana kimefanya nini zaidi ya upotevu wake?Mnakumbuka Hayati aliingia mgogoro mkubwa na CAG wa kipindi kile?Tumuungeni mkono Mama ubadhilifu upo katika serikali yoyote duniani kikubwa ni vyombo vilivyopewa dhamana kupambana na wezi!Sasa tunaaminishwa kipindi kile hapakuwepo na ubadhilifu!Serious?
Mwisho kaboresha huduma nyingi za kijamii mfano katika sekta ya afya kajenga vituo vingi vya afya,kajenga mashule mengi tena ya kisasa.Nilikuwa najaribu kuhesabu idadi ya shule za sekondari alizojenga ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda tu ni zaidi ya tano,hapa naongelea halmashauri moja tu kati ya mbili zilizo kwenye wilaya.Jamani haya hatuyaongei tumekaa kimya tu,hatumtendei haki mama wa watu.
Issue ya kupanda bei ya mafuta hili nalo ni kichekesho cha Karne.Hivi sote hatujui ni issue ya kidunia?Hapa Rais Samia tunamlaumu kwa lipi watanzania?Kwamba yeye anaweza kuzuia kupanda kwa mafuta duniani?
Nilichokibaini;
Wengi wa wanaompinga Rais Samia ni wale wenye ajenda za
1.Mfumo dume;Kundi hili haliamini kutawaliwa na mwanamke.Yaani hawa wao hawataki kabisa kuwa chini ya mwanamke.
2.Baadhi ya wanamtandao; hasa wa utawala uliopita na wapo nje ya mfumo wa Sasa wa utawala.
3.Udini;Obviously kwa Tanzania hili lipo tu.