Rais Samia Suluhu Hassan, inatubidi tukueleze wazi kuwa mvuto wako unazidi kushuka hapa nchini na katika Jumuiya za kimataifa

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Nalazimika kukueleza Rais wangu Mpendwa, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kuwa mvuto wako unazidi kushuka, kadri siku zinavyosonga mbele.

Kwa kweli Mimi nilikuwa mmojawapo niliyekuwa nakuunga mkono sana, baada ya wewe kuchukua mikoba ya aliyekuwa Rais wa awamu ya 5, Rais John Magufuli baada ya kufariki mwaka 2021.

Vile vile nilitiwa moyo sana baada ya wewe kutamka wazi kuwa kule tulikotoka Kwenye awamu ya 5 hatuyakurudia na ukaanzisha 4R"s za kuirejesha nchi Kwenye misingi ya Demokrasia na kuishi Kwa amani badala ya kufarakana.

Hata hivyo kutokana na mwendo tunaokwenda nao nchini hivi sasa, matumaini yangu yote yamepotea na naona wewe Rais Samia, umeamua kuirejesha nchi "gizani" nchi yetu ya Tanzania, kule alilokuwa akiielekeza Mwendazake John Magufuli.

Kitendo kibaya zaidi ulichokifanya Rais Samia,ni Cha kuzuia maandamano ya amani, yaliyoratibiwa na Chama kikuu Cha upinzani nchini Cha CHADEMA, wakiwa katika maombolezo yao, kutokana na kifo Cha kinyama alichofanyiwa kiongozi wao, Ali Kibao, ambaye alishushwa kibabe na watu waliojitambulisha kuwa ni askari Polisi na baadaye kuuawa na mwili wake kutupwa Kwenye vichaka vya Ununio.

Vile vile hao CHADEMA walitaka kufanya maandamano hayo, yaliyozuiwa kibabe na Jeshi letu la Polisi, Kwa nia ya kulikumbusha Jeshi letu la Polisi, Ili watueleze viongozi wa CHADEMA, akina Soka na wenzake wako wapi??

Wewe mwenyewe uliandika katika ukutasa wako wa X zamani ukiitwa Twitter, kuwa umesikitishwa sana na kifo Cha Ali Kibao na ukalitaka Jeshi la Polisi, likuletee haraka iwezekanavyo taarifa za kina kuhusu kifo hicho Cha Ali Kibao.

Hivi sasa ni zaidi ya wiki mbili tokea kifo hicho Cha Ali Kibao, tunashuhudia kimya kizito na hakuna taarifa yoyote inayotolewa na wewe Rais kuhusiana na kifo hicho.

Mungu ibariki Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…