fundimchundo
JF-Expert Member
- Jul 23, 2010
- 739
- 1,032
Bunge letu linahitaji kuongezewa chachu ya aina fulani ili liweze kuichambua kikamilifu Miswada ya Serikali.
Vile vile Bunge letu linahitaji Sauti ya Upinzani yenye kukubalika mbele ya jamii yetu ya Kitanzania.
Kwa kuwa Kada wawili wa CCM wamekuwa Wabunge wa Kuteuliwa, Humphrey Polepole na Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, basi ikimpendeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, itapendeza sana Mhe. Zitto Zuberi Kabwe wa ACT-Wazalendo, akateuliwa kuwa Mbunge, katika zile nafasi za Rais.
Hali hii itaimarisha Muungano wetu kwa kuwa ACT-Wazalendo imekubali kushiriki katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar.
CCM, kwa upande wa Tanzania Bara, itakuwa imeungana na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika kuonesha dhamira njema ya kushirikiana na makundi yote ndani ya Nchi yetu, katika kuijenga Nchi yetu.