Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi kwa kuzaliwa

Rais Samia Suluhu Hassan ni kiongozi kwa kuzaliwa

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Nazani mmewahi kusikia Kuna swali linaulizwa iwapo kiongozi Bora anazaliwa au anatengenezwa, Ndugu zangu ukimfuatilia mh Rais mama Samia suluhu Hassani Tangia wakati ule wa bunge maalumu la katiba namna alivyookuwa anasimamia bunge lile lililokuwa limesheheni vichwa vya kila aina, wabobezi wa kila nyanja na watu wa Rika zote toka makundi ya aina zote na jinsi mh mama Samia suluhu Hassani alivyowezaga kulimudu na kulituliza vizuri.

Hakika utakubaliana nami kuwa mh Rais alizaliwa Ni kiongozi, Ni mama mwenye Hekima na busara zisizo na kifani, Ni kiongozi asiye na mihemuko,Ni kiongozi mwenye utulivu katika maamuzi, Ni kiongozi asiye hamaki Wala kukurupuka katika Jambo lolote lile, Ni kiongozi anayejuwa kuchuja kauli zake kabla ya kutoka, Ni kiongozi mwenye breki ya ulimi wake.

Ndugu zangu kauli za kiongozi au ulimi wa kiongozi unaweza ukaligawa Taifa au kuliunganisha Taifa, ulimi wa kiongozi hasa Rais unaweza kuleta umoja na mshikamano au mtafaruko katika Taifa,ulimi na mdomo wa Rais unaweza kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa au kuwakimbiza, ulimi wa kiongozi unaweza Jenga ujirani mwema au kuubomoa.

Ndugu zangu Ni kauli na matendo mema ya mh Rais wetu yaliyosababisha kuona Leo hata viongozi wa upinzani wakisimama mahali kutoa neno uone wakihubiri Aman mshikamano na uzalendo kwa nchi yetu, Kuna wakati baadhi ya viongozi wa upinzani walikuwa wakitoa maneno mpaka unashaangaa, maana yalikuwa ni maneno yaliyoonyesha mioyo yao ilikuwa Ina majeraha ,vidonda, maumivu, machungu, simanzi,visasi, ndio maana uliona wakawa wanaomba hata mabaya yatupate Kama Taifa.

Ndugu zangu lakini mh Rais kwa Sasa amelituliza Taifa, Ambapo kila mmoja anaona ananafasi katika ujenzi wa nchi hii, mioyo ya wengi Ina amani, Na Sasa Kuna kuaminiana Kama Taifa na kusikilizana katika kutafuta muafaka kwa mstakabali wa Taifa letu.

Hongera Sana mh Rais mama Samia suluhu Hassani na pole Sana kwa kazi kubwa unazofanya kututumikia sisi watanzania Hadi unakosa muda wa kupumzika, wananchi tunaendelea kukuunga mkono na kuzidi kukuombea Afya njema, Songa mbele Wala usikatishwe Tamaa na wachachee maana umeleta matumaini kwa wengi na wengi tuna Imani na wewe mh Rais wetu, Maana tunaona dhamira yako ya dhati katika kulijenga Taifa letu.
 
Ndugu zangu Nazani mmewahi kusikia Kuna swali linaulizwa iwapo kiongozi Bora anazaliwa au anatengenezwa, Ndugu zangu ukimfuatilia mh Rais mama Samia suluhu Hassani Tangia wakati ule wa bunge maalumu la katiba namna alivyookuwa wengi na wengi tuna Imani na wewe mh Rais wetu, Maana tunaona dhamira yako ya dhati katika kulijenga Taifa letu
Hujaweka namba ya simu chawa.
 
Nimefungua nini hiki Mungu wangu. Asubuhi tu nimekutana na upuuzi.
Umekutana na somo linalopaswa kuigwa na viongozi wengi kutoka kwa mh Rais kuwa wanatakiwa wajuwe kuwa ukiwa kiongozi unapaswa kuwa mnyenyekevu na uombe hekima na busara toka kwa Mwenyezi Mungu katika kuongoza watu
 
Kama kuongea ukweli Ni kuwa chawa Basi acha niwe chawa wa mh Rais wakuyasema mazuri yote ayafanyayo na yanayokonga nyoyo za watanzania kwa sasa
Wapumbavu sana nyie hapo hapo ukute unashabikia mambo ya Kenya huku kwenu umekatwa mkia unashabikia ujinga.

Yaani watu wanateseka wanaongezewa matozo ya kishenzi shenzi unaleta uhayawani hapa,? Wapumbavu sana vijana wa CCM mko hovyo kuliko funza
 
Wapumbavu sana nyie hapo hapo ukute unashabikia mambo ya Kenya huku kwenu umekatwa mkia unashabikia ujinga.

Yaani watu wanateseka wanaongezewa matozo ya kishenzi shenzi unaleta uhayawani hapa,? Wapumbavu sana vijana wa CCM mko hovyo kuliko funza
Wapi nimeshabikia habari za Kenya, Mimi nipo na mh Rais wangu hapa Tanzania pamoja na wakulima wenzangu tukiwa tunajiandikisha majina kwa ajili ya kupewa mbolea ya Ruzuku
 
Ndugu zangu Nazani mmewahi kusikia Kuna swali linaulizwa iwapo kiongozi Bora anazaliwa au anatengenezwa, Ndugu zangu ukimfuatilia mh Rais mama Samia suluhu Hassani Tangia wakati ule wa bunge maalumu la katiba namna alivyookuwa anasimamia bunge lile lililokuwa limesheheni vichwa vya kila aina, wabobezi wa kila nyanja na watu wa Rika zote toka makundi ya aina zote na jinsi mh mama Samia suluhu Hassani alivyowezaga kulimudu na kulituliza vizuri,

Hakika utakubaliana nami kuwa mh Rais alizaliwa Ni kiongozi, Ni mama mwenye Hekima na busara zisizo na kifani, Ni kiongozi asiye na mihemuko,Ni kiongozi mwenye utulivu katika maamuzi, Ni kiongozi asiye hamaki Wala kukurupuka katika Jambo lolote lile, Ni kiongozi anayejuwa kuchuja kauli zake kabla ya kutoka, Ni kiongozi mwenye breki ya ulimi wake

Ndugu zangu kauli za kiongozi au ulimi wa kiongozi unaweza ukaligawa Taifa au kuliunganisha Taifa, ulimi wa kiongozi hasa Rais unaweza kuleta umoja na mshikamano au mtafaruko katika Taifa,ulimi na mdomo wa Rais unaweza kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa au kuwakimbiza, ulimi wa kiongozi unaweza Jenga ujirani mwema au kuubomoa

Ndugu zangu Ni kauli na matendo mema ya mh Rais wetu yaliyosababisha kuona Leo hata viongozi wa upinzani wakisimama mahali kutoa neno uone wakihubiri Aman mshikamano na uzalendo kwa nchi yetu, Kuna wakati baadhi ya viongozi wa upinzani walikuwa wakitoa maneno mpaka unashaangaa, maana yalikuwa ni maneno yaliyoonyesha mioyo yao ilikuwa Ina majeraha ,vidonda, maumivu, machungu, simanzi,visasi, ndio maana uliona wakawa wanaomba hata mabaya yatupate Kama Taifa

Ndugu zangu lakini mh Rais kwa Sasa amelituliza Taifa, Ambapo kila mmoja anaona ananafasi katika ujenzi wa nchi hii, mioyo ya wengi Ina amani, Na Sasa Kuna kuaminiana Kama Taifa na kusikilizana katika kutafuta muafaka kwa mstakabali wa Taifa letu


Hongera Sana mh Rais mama Samia suluhu Hassani na pole Sana kwa kazi kubwa unazofanya kututumikia sisi watanzania Hadi unakosa muda wa kupumzika, wananchi tunaendelea kukuunga mkono na kuzidi kukuombea Afya njema, Songa mbele Wala usikatishwe Tamaa na wachachee maana umeleta matumaini kwa wengi na wengi tuna Imani na wewe mh Rais wetu, Maana tunaona dhamira yako ya dhati katika kulijenga Taifa letu
Ni kweli ukizingatia na Mwigulu anamng'arisha Mama zaidi na zaidi.
 
Wewe mwqmba kila siku unakuja na uzi mpya wa kumpongeza rais...

Sio kitu kuna bure... Either wewe ni yeye kbsa au utakuwa wa buku 7
 
Samia ni Kiongozi sio Mtawala ila anaharibiwa na Mwigulu.
Kwa hiyo ana kosa sifa za uongozi. Imagine nchi hii ingekuwa na katiba bora au wananchi wake wangekuwa 50% wanajitambua, kwa hii hali ya maisha inayo endelea angekuwepo hapo ofisini?
Hata wanaccm wenzake walio funguka ubongo wamemchoka kwa kufail kwake
 
Hiyo Wizara ya fedha ilimfaa sana January Makamba.
 
Back
Top Bottom