Kigoma Region Tanzania
JF-Expert Member
- May 25, 2021
- 230
- 612
Rehabilitation of MV Liemba bado imekuwa ni historia, tangu mwaka 2017 Ziwa Tanganyika hakuna meli ya usafiri, na kuendelea kuongezeka kwa vifo vya wanachi kufia kwenye maji kwa kutumia mitumbwi na maboti ya mbao kama usafiri.
Tumepoteza ajira mbalimbali kwa vijana waliokuwa wakitegemea meli hiyo, wafanyabiashara mitaji imekufa na wengine wamehamia mkoa wa Mwanza. Achilia mbali ukame wa wafanya biashara kutoka DRC Congo na Burundi, hatuwaoni tena siku za leo wakasai, wote wanakimbilia mkoani Mwanza. Wazungu watalii wa kwenda Gombe na Mahale hatuwaoni tena kutokana na usafiri hakuna. Hali yetu inazidi kuwa ngumu sana.
Ikiwa hakuna uwezo wa kupata Meli Mpya kwasasa, basi tunaomba ukarabati walau kwa meli hiyo iliyopo au mtutafutie wawekezaji ambao wataweza kuweka meli ya usafiri ziwa Tanganyika.
Tunakuomba Rais wetu na makamo wa Rais, mtusaidie sisi watu wa Kigoma tunapata shida sana, hadha ya usafiri wa maji ni changamoto kubwa ziwa Tanganyika. Wamama wajawazito wanafia njiani kwasababu hakuna usafiri uliosalama kwa wao kufikia huduma za Afya kwa haraka mwambao wa Ziwa Tanganyika.