Rais Samia Suluhu Hassan wakumbuke walimu wa masomo ya sanaa (arts)

Rais Samia Suluhu Hassan wakumbuke walimu wa masomo ya sanaa (arts)

MANYORI Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2012
Posts
462
Reaction score
343
Tangu utawala wa Mh. Hayati Dr. John Magufuli uingie mwaka 2015 huo ndio ukawa mwisho wa ajira kwa walimu wa Arts.

Kwa heshima kubwa na taadhima ninakuomba Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan uwaajiri. Idadi yao ni kubwa kwa sababu walitengwa kwenye mfumo wa ajira tangu mwaka 2015 hadi sasa. Jitahidi sana Mh. Rais, hali ya watu hawa ni dhoofu kupita maelezo. Umasikini umewapiga vilivyo tangu wahitimu. Shule binafsi wamejaa ndugu na watu wasio na sifa ila ukaribu na wamiliki au wakuu wa shule hizi na pana hadi ubaguzi wa dini na jinsia!

Kwa kweli Mh. Rais ninakosa maneno sahihi ya kuelezea hali za wahitimu wa shahada za ualimu masomo ya Arts. Ni fedheha kubwa.

Wasomi hawa wanaonekana kama walifeli chuo, maisha yamewapiga vilivyo. Inatosha! Kama ni adhabu walipewa inatosha! Wamejifunza inatosha Mh. Rais. Sema neno moja tu na roho za watu hawa zitapona.

Mh.Kikwete aliwaajiri hadi 42,000 kwa mkupuo kila mwaka bila kujali masomo yao! Wewe pia unaweza.Hali ya maisha imekuwa ngumu wakati watu waliwekeza huko, mama ona namna.

Wasitokee wakukudanganya kama kina Jafo na wenzake kuwa walimu wa masomo haya wapo wengi wanatosha kwa hiyo hakuna uhaba. Waongo! Waongo wakubwa! Walimdanganya hata Mh. Hayati Magufuli na bila kujiridhisha akasitisha kuwaajiri hadi mauti yamemkuta.

Maisha yameenda kasi sana kwa muda wote ambao vijana hawa watoto wa masikini hawana ajira. Hadi sasa, hawana hata familia tu imekuwa shida. Wametengwa na ndugu na jamaa na wengine wameamua kujiua kuepuka fedheha katika jamii.

Rais Samia Suluhu waokoe. Kama wengine wanavyoajiriwa, walimu wa masomo ya arts pia waajiriwe!

Ahsante sana Mama Samia. Imani yangu kwako ni kubwa kuliko hofu niliyonayo juu yako.
 
Ni matumaini yangu atasikia hiki kilio chako lakini mkuu wewe sio miongoni mwao? Mbona hata mwandiko wako unaonyesha wewe ni miongoni mwao?
 
Siyo kosa mimi kuwa miongoni mwao.Tofauti iliyo kubwa ni kuwa mimi siyo mbinafsi kama wewe.
Walimu wengi hawajikubali hasa wa arts,Wana inferiority complex waliyojengewa na jiwe kujiona hawana thamani,kwa Hilo amefanikiwa
 
Hilo nalo tatizo mkuu.. Ila kiuhalisia hili bomu wanalotengeneza serikali, likilipuka itakua kizaazaa kikubwa mno
Na ninafikiri ni kwa kuwa tu huku hakuna hivi vikundi vya kigaidi.Ila kikitokea,lazima watu wa kwanza wawe wahitimu wa vyuo vikuu hasa walimu wa arts.
 
Walimu wengi hawajikubali hasa wa arts,Wana inferiority complex waliyojengewa na jiwe kujiona hawana thamani,kwa Hilo amefanikiwa
Mimi siyo miongoni mwa hao unaowaita inferior.Anayenifahamu ananifahamu hivyo.
 
Nyie si ndio mlikuwa mnalala saa mbili wenzenu tulivyokuwa tunakesha
Wewe umeajiriwa? Shukuru kwa hilo! Maana hata walimu wa masomo ya sayansi nao wamejazana mtaani.

Kabla ya magufuli kuingia madarakani, ilikua ni ngumu sana kumkuta mhitimu wa masomo ya Hisabati, Fizikia, Kemia na Bailojia akisubiria ajira mtaani!

Ila kwa sasa, wapo lukuki wakifanya mpaka kazi za kujitolea kwa posho ya laki 1 mpaka laki 1 na nusu kwa mwezi!
 
Back
Top Bottom