figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salaam Wakuu,
Nimesikitishwa sana na Kitendo kilichofanywa na Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Siasa kinachogombea, kuingilia Mchakato wa Uchaguzi Serikali za Mitaa.
Huwa amekuwa akijipambanua Dunia na Chawa wake wameandika articles nyingi wakidai Dkt. Suluhu Hassan ni mwanademokrasia kwa Ulaghai wa 4R's.
Kitendo cha kutoa Maelekezo kwa Tume ya Uchaguzi Serikali za Mitaa aliyoiunda yeye(TAMISEMI) kwamba Wawarudishe wagombea eti wenye "Makosa Madoko', hii kisiasa haikubaliki.
Hii inamanisha hata yeye haiamini Tamisemi. Anaona TAMISEMI inaweza kuonea watu.
Rais Samia angekuwa Muungwana kama angeiacha TAMISEMI ifanye kazi kwa mujibu wa Sheria. Kama mtu hajafuata Sheria aenguliwe tu wala asiogopa kwa kigezo cha kuona aibu kwenye Jumuia za kimataifa.
Aiache TAMISEMI ifanye kazi kama Sheria zilizotungwa na CCM zinazovyota.
Ameingilia kati ili kunusuru aibu ambayo ameipata kwa mataifa rafiki. Awaache TAMISEMI wamvue nguo. Sivyo alivyotaka? Yeye ndo alisaini Sheria hii ya Uchaguzi.
Alitaka Chai sasa kwanini alalamike anaungua?
Awaache TAMISEMI wafanye kazi kwa mjibu wa Sheria ili matundu na Uonevu na ubovu wa Watunga Sheria uonekane. Na Maovu ya TAMISEMI yaonekane.
Huyu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan ameingilia kati malalamiko ya vyama vya upinzani kudai wagombea wao wameenguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 27, mwaka huu.
Rais Samia ameielekeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupuuza kasoro ndogo ndogo zilizofanywa na wagombea wa vyama vya siasa wakati wa kujaza fomu kwa ajili ya uchaguzi huo unaohusu serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Emmanuel Nchimbi, alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uwapo wa wagombea wengi wa vyama vya siasa kuenguliwa kutokana na makosa madogo waliyoyafanya wakati wa kujaza fomu.