Optimist_Tz
JF-Expert Member
- Jan 11, 2024
- 1,543
- 1,860
Kwa Mama Samia ndio anasimamia au Mchengerwa?
Kwani hao ni wana familia wa familia moja ??
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa Mama Samia ndio anasimamia au Mchengerwa?
Huyu ni mwehuHakuna jema litakalifanywa na Mama Samia mkakubali. Ageweza tu kukausha na lolote lisitokee. Saa nyingine muwe waelewa.
Kuna mahali kuna shida......ccm wala isilaumiwe.Tatizo sio samiah ,Bali ni dola ambayo Hadi Leo imetoa baraka kwa chama kimoja TU kuwa chenye uhalali wa kushika serikali nacho ni CCM!
Hata kama ungekua wewe ungelazimishwa kuhakikisha chama kinashinda Kwa vyovyote vile !ndicho kinachofanyika kwa sasa!
Mkuu figganigga , kwanza tujifunze appreciation kila mazuri yanapofanyika.
Hili alilofanya Rais Samia ni jambo jema na jambo zuri.
Uamuzi huo ni kama utekelezaji wa ushauri huu Kuelekea 2025 - LGE2024 - Ombi Maalum, Kwa Mtu Maalum Achana na Hizi Mutatis Mutandis Kwenye Chaguzi za SM2024 & U/Mkuu2025, Tumia Ceteris Peribus, Utabarikiwa, Tutabarikiwa!
Hiki alichokifanya Rais Samia, nilikishauri kwa JPM Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi humo nilishauri
Hili Rais Samia amelifanya na anastahili pongezi za dhati.
P
Kila jambo lina chanzo, muasisi na watekelezaji. Wala hakusingiziwa. Wakati wa Mkapa na Mrema, hayakuwepo mauaji. Wakati wa Kikwete mbinyo wa upinzani ukaongezeka,, ndipo mauaji ya akina Mwangosi yakaanza. Wakati wa Magufuli ikatangazwa operation ya mauaji na kukamatwa kwa hao wapinzani. Sasa ni mwendelezo. Kama ni gari ilianza speed ya gia kidogo na sasa imepamba moto kabisa na kurudi gia ndogo wakati wa Mkapa itachukua muda sana, maana watu wamezoea kunywa damu. Ninachoona wapinzani wangejiondoa ili laana ya damu iendelee ndani ya chama chetu cha CCM sababu ni sheria ya asili. Ukizoea kuua hutajali ni nani aliyeko mbele yako ili mradi anakupinga. Tukumbuke yule katibu wetu wa ccm Njombe aliyeuwawa hivi karibuni.JPM alisingiziwa mabaya mengi sana
Are u serious?Tatizo sio samiah ,Bali ni dola ambayo Hadi Leo imetoa baraka kwa chama kimoja TU kuwa chenye uhalali wa kushika serikali nacho ni CCM!
Hata kama ungekua wewe ungelazimishwa kuhakikisha chama kinashinda Kwa vyovyote vile !ndicho kinachofanyika kwa sasa!
Juhudi kibao zenye kuumiza watu ni za Nini!!?kama Dola ingeamua chama chochote Cha siasa chenye sera nzuri na wameimplant watu wakuaminika kwenye hivyo vyama unafikiri kungekua na sarakasi zote hizo!!?Are u serious?
Uko sahihi kabiasa, CCM kupitia vyombo vya dola hawako tayari kuona demokrasia inachukua mkondo wake, hivyo njia pekee inayoweza kuwaondoa madarakani ni matumizi ya nguvu. Laiti wanajeshi wetu wangekuwa na uchungu na nchi hii wangefanya kama wenzao wa nchi za Afrika ya Magharibi kuinusuru nchi kutoka mikononi mwa hawa makaburu weusi. Mkataa pema pabaya panamuita, CCM wanakataa njia ya kistaarabu ya kufanya mabadiliko basi wanakaribisha machafuko na matumizi ya nguvu.Hii nchi mpaka hapa ilipofikia, inahitaji watu jasiri sana wa kuiondoa CCM madarakani kwa nguvu. Kinyume na hapo, tutaendelea tu kulalamika mpaka siku ya kiama.
Hao wanaolazimishwa wahakikishe ccm inashinda wanalazimishwa na nani kama siyo Samia? Na tunapomtaja Samia kwenye matatizo pia mkubali kama mnavyopenda kumsifia kwa kumtaja yeye kwenye miradi inayotekelezwa kwa fedha za serikali kwa sababu yeye ndiye kiongozi wa nchi na ndiyo maana ukiona sehemu kumetokea machafuko wananchi wanashinikiza Rais kuondoka madarakani kwa sababu yeye ndiyo serikali yenyewe hivyo akiondoka madarakani maana yake itatoa nafasi kwa mtu mwingine kuunda serikali upya itakayoweza kuleta ufumbuzi wa tatizo lilojitokeza.Tatizo sio samiah ,Bali ni dola ambayo Hadi Leo imetoa baraka kwa chama kimoja TU kuwa chenye uhalali wa kushika serikali nacho ni CCM!
Hata kama ungekua wewe ungelazimishwa kuhakikisha chama kinashinda Kwa vyovyote vile !ndicho kinachofanyika kwa sasa!