Rais Samia Suluhu: Kila mwenye nia 2025 aache mara moja

Rais Samia Suluhu: Kila mwenye nia 2025 aache mara moja

Mama Samaia Hassan Suluhu anazidi kuthibitisha kuwa, Kwenye uumbaji Mwenyezi Mungu alituumba Wanaume wa Kwanza lakini AKAWAPA WANAWAKE HEKIMA, UPENDO NA NIDHAMU KAMA UPENDELEO KWAO NA KUTUTOFAUTISHA NA SISI (wanaume)..
wanaume sisi tukipata madaraka tunakuwa jeuri na kusababisha Mabalaa na mitafaruku
ndio maana wakasema hakuna kama MAMA
 
Rais Samia Suluhu amewataka mawaziri na watendaji wote kuwajibika na kufanya kazi na rekodi zao zitawafata katika maisha yao. Rais amesema pamoja na macho yake kulegea, yanaona na atakuwa na jicho kubwa kuangalia rekodi zao.

"Inapoingia kipindi cha pili cha Rais aliepo, watu kidogo mnakuwa na lile na hili kuelekea mbele, nataka kuwaambia acheni. Twendeni tufanye kazi, hili na lile tutajua mbele, sawa ndugu zangu?" Alisema Rais Samia.

Huo ni ujumbe kwa yule rais wa kwenye mawe..
 
Hamna kitu hapo anawapigia mbuzi gitaa tu.

CCM wanajua wakishapitishwa na chama chao kuwa wagombea urais basi automatically wanakuwa wameshashinda urais wenyewe, kwasababu hii katiba mbovu iliyopo itawapa ushindi.

Ndio maana wao hutumia nguvu nyingi na muda mwingi kuwekeza kwenye chama chao ili wapitishwe kuwa wagombea, hapo mwenyekiti asipoteze muda wake kuwashauri nini cha kufanya.
 
Mama anakaba rofu.

Ngoja tuone kwanza kama kazi anaiweza.
 
Rais aache kitumia hizo lugha za mzaha na ajiamini,kama vipi ajifunze kwa Angel Merkel,Jasinda Aden,Christine Lehard na wanawake wengi waliowwhi kuwa wakuu wa nchi au ma ceos wa mashirika makubwa duniani
 
Waitupie macho account ya Veronica France huko Facebook,ina nia mbaya sana na Mama wakitumia kivuli cha 'wafia chama' ni genge hatari sana lenye nia ovu kwa Taifa letu.
 
Uchaguzi wa ndani wa Chama mwaka 2022 watu wanaanza kupanga safu zao.
 
Yeah,..... ndio hayo Pascal Mayalla aliwahi "kusema" humu kuwa anayapenda?
p
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom