Rais Samia Suluhu kufanyia kazi hoja za Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) Bandarini

Rais Samia Suluhu kufanyia kazi hoja za Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) Bandarini

Getrude Mollel

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2022
Posts
270
Reaction score
362
Mamlaka ya Bandari (TPA) imefanya upembuzi wa mifumo yake ili kushughulikia hoja za Mdhibiti wa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2022/21 ya kuwa mifumo inasomana na hivyo kudhibiti upotevu wa mapato.

Vilevile, imebainisha kuwa kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi Juni 2022, mapato ya TPA yameongezeka kutoka Bilioni 910.4/- mwaka uliopita hadi Sh. Trilioni 1.095 mwaka 2021/22 huku ikitarajia kukusanya Sh. trilioni 1.224 kwa mwaka 2022/23.

Kwa sasa TPA inafanya maboresho makubwa katika mifumo yake ya kukusanya mapato ili kuondokana na mifumo ya kizamani ikiwemo kutumia karatasi. Ubadilishwaji wa mifumo utasaidia TPA kufuatilia kwa ukaribu mapato yote yanayokusanywa na kiasi kinachotumika katika wakati unaohitajika.
 
Back
Top Bottom