Daraja la Kigogo Busisi ni halina maana yoyote ile. Matumizi mabovu mno ya fedha ambayo yangeelekezwa pengine.
Nakusihi Rais Samia Suluhu. Piga chini huu mzigo. Hakuna fedha zinazotolewa kama takrima. Eti kisa sijui kina fulani wanatokea hapo ndiyo iwe kigezo. Piga chini mama.
Lingine kwenye taasisi karibu zote za umma angalia sana viongozi wake. Kuna kigezo kimetumika kuwaweka pale. Kwa sasa nikupe muda ufanye kazi huku nikikuangalia kwa umakini mkubwa.
Mimi huwa naamini asilimia kubwa ya members humu ni waelewa,lakini kumbe kuna wajinga wa kiwango cha juu kama wewe Sam!
Kwanza umeonyesha ubaguzi na chuki ya wazi kwa Mpendwa mwendazake.
Pili umeonyesha jinsi ulivyo mbumbu wa elimu.
MANUFAA YA DARAJA LA BUSISI.
Hivi sasa serkali inaendeza miradi ya kimkakati ya maendeleo ya miundombinu kote nchini.
Mojawapo ya miradi hiyo ni reli ya SGR kutokea Dar es salaam hadi mwanza.
Reli hii ya kisasa ni mradi wa kimkakati hasa kuiimarsha biashara ya Bandari ya Dar es salaam ili kuzifikia nchi za ukanda wa maziwa makuu ambazo ziko land locked (haziko katika pwani ya bahari).
Nchi hizo jirani zetu ni kama vile Uganda, Burundi,Congo DRC, na Rwanda.
Kwa kuimarisha SGR yetu hadi Bandari kavu ya Fela pale mwanza.na kwa kulitumia daraja la Kigongo na Busisi,itawarahishia na pia kuwapuguzia gharama hao wateja wa bandari ya Dar es salaam kwa kuwafupishia safari kutoka Tinde junction pale Shimyanga hadi Dar es salaam takriban kilomita 1200 ambapo kwenda na kurudi inakuwa 2400kms.
Huo ni umbali mrefu sana kwa lori. Pia unawapunguzia usumbufu kwenye vizuizi na mizani.pamoja na msongamano wa misururu ya magari jijini Dar es salaam.
Badala ya kwenda umbali huo wote,malori hayo yatachukuwa mizigo yao kutokea Fela dry port ya SGR station Mwanza kwa kutumia daraja la kigongo-Busisi.ambapo ni takriban umbali usiozidi kilomita 250 kutokea pale Tnde Junction.
Hayo ndio manufaa ya kujengwa kwa daraja hilo JPM aliona mbele zaidi.
Ndio maana hata ndege watu walizikashifu ila sasa walewale waliozikashifu nimewasikia jana walizisifia kupitia BBC SWAHILI.news bulletin ya jioni wakati wakitoa maoni yao kuhusu upokewaji wa zile Airbus mbili mpy,zilizoingia jana.
My take:
Kama mtu jambo huna uelewa nalo ni vema ukafanya utafiti au badala ya kukimbilia keyboard kuponda, basi ukatumia keyboard hiyohiyo kuuliza wenye uelewa wakueleweshe.
Karibu TANZANIA [emoji1241] [emoji813]