Rais Samia Suluhu, tumia ziara yako nchini Kenya kuomba radhi kwa kuchomwa vifaranga na awamu iliyopita nchini mwako

Yaani serikali ya kenya wakosee halafu waombwe msamaha, wangethibiti hayo magendo ya vifaranga huko mipakani mwao vingefikaje bongo, ningekuelewa kama watetezi wa haki za wanyama ndo wangeombwa msamaha siyo hao manyang'au...
Kenya ilikosea wapi ?
 
Labda useme “hivi ndivyo tulivyokuwa tunawashughulikia watu walioleta mchezo kwenye nchi za watu!” Kumbuka zama zimebadilika!
kubadilika kwa zama hakuna uhusiano wowote na wahalifu, bado wataendelea kushughulikiwa kama kawaida
 
Kenya ilikosea wapi ?
Sasa Tanzania iliwakosea wapi Wakenya mpaka unataka mama akaombe msamaha kwa Kuchomwa vifaranga? wakati vifaranga ni vya wahuni tuu kutoka Kenya waliotaka kufanya biashara za magendo
 
Halafu cha kusikitisha mwenye vifaranga aliomba avirudishe Kenya wakamkatalia. Kilichofuata ni kuvipiga kiberiti.
 
kubadilika kwa zama hakuna uhusiano wowote na wahalifu, bado wataendelea kushughulikiwa kama kawaida
Hakuna kifaranga hata mmoja aliye kuwa na kosa au uhalifu wowote! Lakini hata kama wangekuwa waalifu, hukumu ya kuwachoma moto, ni zama za kale, sasa hivi Mazaa anashughulikia Suluhu na Uhuru kati yetu na Kenya, if you know what I mean!
 
Hakuna kifaranga hata mmoja aliye kuwa na kosa au uhalifu wowote! Lakini hata kama wangekuwa waalifu, hukumu ya kuwachoma moto, ni zama za kale, sasa hivi Mazaa anashughulikia Suluhu na Uhuru kati yetu na Kenya, if you know what I mean!
Kwani kuku au mbuzi wakichinjwa kwa ajili ya vitoweo wanakuwa wamefanya kosa? tumechoma vifaranga elfu 5000 ili kunusuru ndege wetu wengine, kama unataka biashara Fata utaratibu, ukileta uhuni tutaaribu biashara yako na maumivu makali tutakuachia, nafikiri somo lilieleweka baada ya kuchoma vile 5000 hakuna aliethubutu kuleta vifaranga bila utaratibu, hatuna undugu na wahalifu wala bidhaa zao , kuhusu Mama leteni magendo halafu uone kitakacho Fata
 
Wao mbona wametuibia sana madini yetu ya Tanzanite na hawajawahi kutuomba radhi wala kulipa fidia yoyote😞😞
 
Hii ni dhambi kubwa ambayo iliufanya utawala wa marehemu Magufuli, na ulijidhihirika kuwa ulikuwa ni utawala wa shetani.

Makonda na wenzake waliokuwa wakisimamia mambo haya, hata kama si leo au kesho, siku moja ni lazima wasimame mahakamani kujibu, na kupewa hukumu sawasawa na matendo yao.

Tunaomba Mungu awajalie pumziko jema marehemu wote waliouawa wakati wa utawala dhalimu wa marehemu Magufuli, na walio hai kwa namna yoyote iwastahiliyo, wapate kinachowastahilia. Ni ushetani mkubwa kuua binadamu wenzako.

Muuaji, hata atende jema gani, hubakia kuwa shetani.
 
Baada ya hotuba ya Jana ya SASHA sijui bado Una msimamo huu?
 
Kila ubaya utalipwa
 
Loo, mada hizi sasa zitatufikisha wapi?

Imebidi haya sasa ndiyo tuyashikie bango wakati huu?

Najishangaa kwamba nimechangia kwenye mada hii!
Mkuu umemsikia Mtemi Hangaya jana ?
 
Njoo uandike leo tena huu upuuzi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…