Mkuu kunywa Soda moja nitalipa. Mimi nawashangaa. Hivi issue mara ya Vifaranga, je wanajua Wakenya Wametufanyia mangapi sisi? Je ni Magufuli alisema chomeni vifaranga? Wanaokoteza vitu vidogo vidogo mno.
Hayati Dr. Magufuli kipenzi cha Watanzania walio wengi hayupo wao wanapambana naye. Ni aibu. Chadema tunawakumbusha 2025 si mbali, mjipange msijeanza kulia. Mnakomaa na Hayati, kule Samia anatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, 2025 atakiwaleza wananchi nini amefanya kama atagombea yeye kura chungu nzima kwake ama kwa mgombea wa CCM wa wakati huo, ninyi mnabaki kulalama.
Badilikeni basi. Msitafte cheap politics, jipangeni 2025 mtakuwa na Sera gani Mbadala wa Sera za CCM ili Mshinde. Kitu ambacho mnasahau ni kwamba Hayati JPM alikuwa ni Kipenzi Cha wengi, mkimsema vibaya tu kura zinapungua zaidi, hebu mkomae na mambo ya Msingi.
Mwenyekiti Mbowe kawasababisha chungu ya Matatizo, ninyi mmekaa kimya mpo tu. Hangaikeni naye, acheni mambo ya Hayati Dr. JPM, Mwamba wa Mageuzi nchini Tanzania na Africa.