Samiaagain2025
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 3,626
- 3,869
"SIKIA SAUTI YA WANYONGE':
Tangu awamu ya mheshimiwa hayati Magufuli ilipoanza,mfumo wa ajira ulipinduliwa.
Tulikuwa tunategemea kila mwaka ajira zipo hasa kwa idara ya afya,walimu, na kilimo na mifugo.
Tangu mwaka 2015,tupo mtaani tunahangaika,Tena sisi wanufaika wa HESLB tunazalishiwa deni kila mwaka
(Retention fee)
Hivi mtu umemaliza chuo mwaka 2015 ukitegemea mwaka 2016 utaajiriwa, halafu bado upo mtaani!
Si utakuwa umeharibiwa mipango mingi sana,ikiwemo ya kijamii(ndoa,
n.k),kiuchumi na hata kisaikolojia.
Bora kama hakuna pesa, mtuajiri sisi ambao tuliokuwa tayari tumechagua kazi za kusomea kabla ya awamu ya tano(2015,2016 na 2017),maana tungejua hakuna ajira tusingesoma au tungesomea kazi zingine!
Ila tunaamini kwa serikali ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan,tutaajiriwa. Japo tunaumia kusikia mtanzania mwenzetu anakaa na dola za kimarekani 1.6+ milioni nyumbani kwake(pesa ya umma),huku sisi hatuna ajira.
Tunakuomba mama Samia, tuhurumie na sisi wahitimu wa vyuo, especially 2015,2016,na 2017.
NB; Ni ombi tu lakini.
By Sauti ya wanyonge
Tanzania.