Rais Samia Suluhu tupunguzie mateso, tumecheleweshwa sana ajira mpya

Rais Samia Suluhu tupunguzie mateso, tumecheleweshwa sana ajira mpya

Hello JF,

Hongera mama Samia kuwa kiongozi wetu mpya...
Naona unampangia cha kufanya Tena kea msisitizo.

Kawani we ndo unampangia ainze na kipi, apache kip na asifanye kipi?

Kama ndivyo we ndo president na fanya kama unavyo mwagiza.

#We believe in you Ma Samia
 
Rebeca 83 leo umesikia maneno ya Dr Mpango kwamba nitafuata falsafa za magufuli! Mwingine akasema tuweke sanamu la Magufuli sasa kwa aina hii ya wabunge unafikiri wanawaza hayo matatizo ya ajira?

Serikali ya Magufuli ndiyo iliyokuwa inaongoza kwa kupika takwimu na huyu Mpango ndio alikuwa kinara wa kupika; Leo hii tunaambiwa tupo uchumi wa kati, hivi wananchi kama sisi ambao miaka arobaini au ishirini tunakula visamvu,dagaa,mihogo ya kukaanga hadi leo unatuaminishaje tupo kwenye huo uchumi?

Maana tunangonjera zile zile miaka nenda miaka rudi.Nilitegemea leo Makamu wa Rais aje na maneno ya angalau ya kuona maeneo ambayo walikosea na sasa watabadilisha kwa haraka haraka .
 
Simshauri hata kidogo mama kuajiri, waajiriwe wa serikali ni mzigo mkubwa kwa serikali alafu ufanisi hakuna ofisi ni vijiwe vya kupiga soga.
Aacha kabisa mawazo ya kuajiri,Maendeleo ya nchi hayataletwa kwa serikali kuajiri ajiri tu
Afanye hivi;
  • aweke Sera nzuri za kuvutia wawekezaji wengi Sana na kuwawekea mazingira rafiki
  • apeleke maji nchi nzima na yawe kwa bei nafuu sana
  • umeme uwe nafuu sana, nusu ya Sasa hivi
  • huduma za hospital ziwe nafuu na kila mtu awe na bima Kama ilivyo kitambulisho Cha kura.
  • barabara zote ziwe zinaunganisha wilaya na kata
 
"SIKIA SAUTII YA WANYONGE':

Tangu awamu ya mheshimiwa hayati Magufuli ilipoanza,mfumo wa ajira ulipinduliwa.

Tulikuwa tunategemea kila mwaka ajira zipo hasa kwa idara ya afya,walimu, na kilimo na mifugo...
sipendi watu wanao lia lia, mjiajiri
 
Mods Naona mmeunganisha topic yangu Sijui mnapata commission mkiunganisha topics eti???
 
Nilijua peke yangu nipo confused kumbe topic zimeunganishwa
 
Watanzania inabidi tusisubiri ajira za serikali. Tufungue miradi zaidi mpaka leo hii kuna upungufu wa ngano, sukari, mafuta lakini unataka upate ualimu ambao pesa yenyewe ni ndogo badala ya kuwekeza.
Uwekezaji bila mtaji?
 
Vijana tumelia sana kipindi cha magu ni wakati muafaka sasa wa mama kufuta machozi yetu
 
"SIKIA SAUTII YA WANYONGE':

Tangu awamu ya mheshimiwa hayati Magufuli ilipoanza,mfumo wa ajira ulipinduliwa.

Tulikuwa tunategemea kila mwaka ajira zipo hasa kwa idara ya afya,walimu, na kilimo na mit'o....
Ukisubiri ajira serikalini mkuu utasubiri sana,jiajiri.Serikali ita ajiri wangapi,mbona wahitimu mko wengi.Serikali itaajiri kufuatana na uwezo wake kifedha na kama nafasi za ajira zipo.Jiongeze mkuu.Serikali hailazimiki kukupatia ajira,imechangia kwenye kukupa elimu huo ni msaada mkubwa.
 
Hivi kila mtu hapa JF ni mfanya biashara, kumbe tuna mastockist wengi sana humu JF, hakika humu wamekaa business tycoons maana kila mtu anawaambia magraduates jiajiri.... Business tycoons my foot [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Job seekers tunapitia ishuz nyingi. Sitaenda deep ila ni upuuzi.
 
Exactly ni upuuzi tu, lijitu linajua kusema JIAJIRI tu,... Usikute hata hawajui maana ya business plan, hawajui hata laws of demands and supply, hawajui hata market research, hawajui hata terms and conditions za credit policies kwenye financial institutions, hawajui ya kwamba baadhi ya government policies hususan zinazo husu investment zinachangia ku affect wafanya biashara wakubwa na wadogo kuyumba wanao toa ajira kwa wingi...wanaishia kusema Jiajiri Jiajiri Jiajiri... Pathetic
 
Aisee suala la ajira ni suala la serikal kulitilia sana mkazo ,kama hali itabak hivi hivi tutazalisha vijana wenye msongo wa mawazo na pia tutazalisha watu wenye roho mbaya hata ya kuwa magaidi sababu hawana cha kupoteza

Vijana wengi wameshindwa hata kuanzisha familia sababu ya kukosa mwelekeo wa kimaisha wanaishi uchumba sugu tu .

Sahv MTU anayesoma anachukuliwa anapoteza mda hata na wale dropouts wanamdharau

Kiufupi tunatengeneza tatizo kubwa sanaa la washambuliaji wa serikal kwa kutofikiria kuajir hawa wasomi ambao wako mitaan

Mama samia achana na falsafa za jiwe ( r.i.p) dunia hatujaja tuteseke wape vijana ajira wamalizie kipindi cha kuishi hapa duniani kwa raha .
 
Usitegemee kumaliza masomo ndo uajiriwe, find means za kuishi usitegemee serikali kukidhi utoaji wa ajira kwa wahitimu wote nchi hii, elimu uliyopata changanya na za kwako.

Hata na mimi nimewaza hawa vijana wanaomaliza masomo ya degree wanatarajia kuajiriwa na Serikali, jee hiyo serikali itaajiri wangapi?

Vijana sasa hivi jaribuni kuwaza kujiajiri na siyo kusubiria ajira ya serikali.
 
Exactly ni upuuzi tu, lijitu linajua kusema JIAJIRI tu,... Usikute hata hawajui maana ya business plan, hawajui hata laws of demands and supply, hawajui hata market research, hawajui hata terms and conditions za credit policies kwenye financial institutions, hawajui ya kwamba baadhi ya government policies hususan zinazo husu investment zinachangia ku affect wafanya biashara wakubwa na wadogo kuyumba wanao toa ajira kwa wingi...wanaishia kusema Jiajiri Jiajiri Jiajiri... Pathetic

Bugsy wewe wacha hayo mambwembwe na mabombastic ya economic theories, ukiamua kufanya jambo utayajua hayo.

Ikiwa akina mama ntilie na wajasiriamali wadogo wanafundishwa abc za biashara, mwenye degree atashindwaje kujiongeza?

Ukianza kujiwekea vikwazo kabla ya kuanza lazima utashindwa.

Pathetic ni wewe ambaye umefunga mikono unasubiria tu.
 
Back
Top Bottom