Rais Samia Suluhu tupunguzie mateso, tumecheleweshwa sana ajira mpya

Rais Samia Suluhu tupunguzie mateso, tumecheleweshwa sana ajira mpya

Bugsy wewe wacha hayo mambwembwe na mabombastic ya economic theories, ukiamua kufanya jambo utayajua hayo.

Ikiwa akina mama ntilie na wajasiriamali wadogo wanafundishwa abc za biashara, mwenye degree atashindwaje kujiongeza?

Ukianza kujiwekea vikwazo kabla ya kuanza lazima utashindwa.

Pathetic ni wewe ambaye umefunga mikono unasubiria tu.
Ignorant! hayaja kukuta ww..
 
Watanzania inabidi tusisubiri ajira za serikali. Tufungue miradi zaidi mpaka leo hii kuna upungufu wa ngano, sukari, mafuta lakini unataka upate ualimu ambao pesa yenyewe ni ndogo badala ya kuwekeza.
Biashara sio hobby au professional kusema utafanya na kusurvive kirahisi.....

Si kila mtu kazaliwa kufanya biashara....
 
Juzi hapa niliandika uzi na kupendekeza kuwa muda umefika sasa kwa Tanzania tuanze kutumia mfumo wa malipo ya lisaa kwa wafanyakazi.....

Tukitumia huu mfumo kutakuwa na faida nyingi kuliko hasara.

1. Masaa ya kazi au kukaa kazini yatapungua. Kwa wastani mfanyakazi wa serikali huwa anatumia siku nzima kazini. Na hii humfanya ndani ya muda mfupi kuwa demoralized na kuboreka hatimae kukosa ufanisi kiutendaji.

Kwa mfano tukiweka mkataba kuwa mfanyakazi atafanya masaa wastani ni matano kwa siku au sita hii itampa nafasi ya kufanya mambo yake mengine na hata kufanya kazi na kampuni nyingine aidha za serikali au binafsi na kujiongezea ujira na kipato kizuri.

2. Kupungua kwa masaa ya kazi kutaweka gepu la uhitaji wa wafanyakazi, mfano, shirika likiwa na mtendaji ataeingia kazini kuanzia saa kumi na mbili then ikifika saa tano amemaliza shift yake anatoka kazini. Then kuanzia hiyo saa tano kwenda mbele kutakuwa na vacancy au nafasi itayohitaji mtu mwingine ashike shift ya saa tano hadi kumi na moja jioni kutimiza masaa sita mengine. Kutokea kumi na moja jioni masaa sita mengine ni hadi tano usiku, kutokea tano usiku hapo kama kampuni inakesha ni hadi kumi alfajiri, mzunguko unaendelea hivyo.

Hapo tayari kuna gape na wafanyakazi wangapi unaona......?!

Sasa zidisha mara idadi ya ajira zilizopo sasa..... Hivi tutatengeneza ajira ngapi na watu wangapi watasaidiwa kupata ajira ......?!

3. Ufanisi utaongezeka..... Mtu anae kaa ofisini masaa kumi na kitu siku nzima na ambae anakaa nusu au robo siku wanautendaji wa tofauti sana sababu ya kuwa na muda mchache wa kufocus na kazi.... Hii inawapa watu ari ya kuchapa kazi sana..... Na kuwa na hamu ya kuja kazini na kutopoteza muda wakiwa kazini sababu masaa yao yanatathiminiwa na kutazamwa namna wanazalisha....
 
Km kuna awamu vijana wamechezea bakora za maisha basi n awamu ya tano. Kijana umenyimwa ajira bas ukisema ngoj nijiajiri niombe mkopo kwa ndugu zangu watumishi wa umma nao wanakwambia hawana sent mana mishahara haijaongezwa mwaka wa 6 sasa hvo n hawawez ata ku top up mkopo, ukisema bas aya ngoja ukamkope mfanyabishar unaemjua akupe ata mtaji nae anajuta analia na kodi balaa hana mia... Ukisema ngoj usubirie labd mbunge wako atakutetea Bungeni anakwambia kijana kajiajiri, ukisem aya ngoj usikilize wataalam wanasemaj juu ya hili janga wanakwambia nenden veta wote tuwe mafund umeme, yan hii awamu ya tano ctaisahau kwa ukatili wake kwa vijana.
 
"SIKIA SAUTII YA WANYONGE':

Tangu awamu ya mheshimiwa hayati Magufuli ilipoanza,mfumo wa ajira ulipinduliwa.

Tulikuwa tunategemea kila mwaka ajira zipo hasa kwa idara ya afya,walimu, na kilimo na mifugo.

Tangu mwaka 2015,tupo mtaani tunahangaika,Tena sisi wanufaika wa HESLB tunazalishiwa deni kila mwaka
(Retention fee)

Hivi mtu umemaliza chuo mwaka 2015 ukitegemea mwaka 2016 utaajiriwa, halafu bado upo mtaani!
Si utakuwa umeharibiwa mipango mingi sana,ikiwemo ya kijamii(ndoa,
n.k),kiuchumi na hata kisaikolojia.

Bora kama hakuna pesa, mtuajiri sisi ambao tuliokuwa tayari tumechagua kazi za kusomea kabla ya awamu ya tano(2015,2016 na 2017),maana tungejua hakuna ajira tusingesoma au tungesomea kazi zingine!

Ila tunaamini kwa serikali ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan,tutaajiriwa. Japo tunaumia kusikia mtanzania mwenzetu anakaa na dola za kimarekani 1.6+ milioni nyumbani kwake(pesa ya umma),huku sisi hatuna ajira.

Tunakuomba mama Samia, tuhurumie na sisi wahitimu wa vyuo, especially 2015,2016,na 2017.

NB; Ni ombi tu lakini.

By Sauti ya wanyonge
Tanzania.
yataisha ASAP Mama Samia yuko Vizuri
 
Hello JF,

Hongera mama Samia kuwa kiongozi wetu mpya.

Swala la ajira kwanza hamna evidence kuwa lilikua tatizo kubwa kipindi cha Magufuli.

Ila hata hivyo kuna tatizo la documentation kwa mfano data zilizopo hazionyeshi specific kati ya wangapi wahitimu walipata ajira.

So kwa vile malalamiko ni mengi kati ya wahitimu na wengine tumeishi nao,then tatizo lipo hata kama data hazisemi hivyo.

Mimi nakuomba mama hili liwe moja ya matatizo ya awali utakayotatua.

Kama unaweza tenga fungu special kwa ajili ya ku deal na hili tatizo.

Kuwe na incentives paid kwa employers watakaoajiri mhitimu wa miaka mitano nyuma.

Priority iwe kwa wale waliohitimu zamani kwa sababu wamekaa muda mrefu kwenye hali ngumu ya kutokua na ajira.

Kingine unachoweza kufanya kama huna enough funds.

Ni kuweka mfuko maalumu wa dharula watu wachangie.

Wapewe wahitimu wanaotaka kujiajiri/hii iwe ya wazamani na wa sasa wanaotaka kujiajiri

Yeyote atakayeandika proposal nzuri itakayowasadia vijana/watu wengine kupata ajira then wapewe priority.

Mengine wana JF changieni ipi unadhani ni njia ya kutatua hili swala la ajira ambalo linawezekana kufanyika ndani ya muda mfupi ujao, ku-rescue wahitimu ambao hawana ajira?

Mods naomba msiunganishe hii.

Becky...
Imeunganishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simshauri hata kidogo mama kuajiri, waajiriwe wa serikali ni mzigo mkubwa kwa serikali alafu ufanisi hakuna ofisi ni vijiwe vya kupiga soga.
Aacha kabisa mawazo ya kuajiri,Maendeleo ya nchi hayataletwa kwa serikali kuajiri ajiri tu
Afanye hivi;
  • aweke Sera nzuri za kuvutia wawekezaji wengi Sana na kuwawekea mazingira rafiki
  • apeleke maji nchi nzima na yawe kwa bei nafuu sana
  • umeme uwe nafuu sana, nusu ya Sasa hivi
  • huduma za hospital ziwe nafuu na kila mtu awe na bima Kama ilivyo kitambulisho Cha kura.
  • barabara zote ziwe zinaunganisha wilaya na kata
Inawezekana wewe ni msukuma ambaye mmeajiriwa kwa ule mpango wa rise Sukuma, mpango ambao ulikuwa unasubiri wasukuma wajilundike mtaani, then atoe ajira kuwachukua wote. Namchukia huyu shujaa wa Africa na dunia kwa ujumla.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hili la ajira hususani kwa walimu tunalikuza sana kuliko uhalisia,kuna walimu kibao wamejazana sehemu za mijini na kwenye majiji na bado watazidi kuongezeka na gia yao siku hizi ni kuwa wanafuata huduma za matibabu mijini, wanajitengenezea ugonjwa feki.Ninao mfano mdogo wa walimu watatu wa history jijini mwanza ambao wanafundisha kidato kimoja yaani wamegawana topic!!!! NINACHOKIONA HAPA NI POOR DISTRIBUTION OF MAN POWER NA SIO UHABA hususani kwenye sekta ya elimu sijajua kwa sekta nyingine.Serikali iwahamishe walimu kutoka mijini ni wengi na wapelekwe kwenye upungufu.
 
"SIKIA SAUTI YA WANYONGE':

Tangu awamu ya mheshimiwa hayati Magufuli ilipoanza,mfumo wa ajira ulipinduliwa.

Tulikuwa tunategemea kila mwaka ajira zipo hasa kwa idara ya afya,walimu, na kilimo na mifugo.

Tangu mwaka 2015,tupo mtaani tunahangaika,Tena sisi wanufaika wa HESLB tunazalishiwa deni kila mwaka
(Retention fee)

Hivi mtu umemaliza chuo mwaka 2015 ukitegemea mwaka 2016 utaajiriwa, halafu bado upo mtaani!
Si utakuwa umeharibiwa mipango mingi sana,ikiwemo ya kijamii(ndoa,
n.k),kiuchumi na hata kisaikolojia.

Bora kama hakuna pesa, mtuajiri sisi ambao tuliokuwa tayari tumechagua kazi za kusomea kabla ya awamu ya tano(2015,2016 na 2017),maana tungejua hakuna ajira tusingesoma au tungesomea kazi zingine!

Ila tunaamini kwa serikali ya mheshimiwa rais Samia Suluhu Hassan,tutaajiriwa. Japo tunaumia kusikia mtanzania mwenzetu anakaa na dola za kimarekani 1.6+ milioni nyumbani kwake(pesa ya umma),huku sisi hatuna ajira.

Tunakuomba mama Samia, tuhurumie na sisi wahitimu wa vyuo, especially 2015,2016,na 2017.

NB; Ni ombi tu lakini.

By Sauti ya wanyonge
Tanzania.
Na sie tunasubiri increment zetu na Madaraja.Mheshimiwa kazi anayo.
 
Kipato 300000 kwa mwezi,HESLB-15% income tax,NSSF-10%,
Bado wategemezi,n.k,

Utaweza kuishi ?
Kama nimeweza kuishi bila huo mshahara kabisa, nikiupata nitaishi pia, usitake makuu kuliko uwezo wako mkuu!
Halafu hayo makato na hiyo 300k, ni kwa mtazamo wako tu, ila sio malipo kwa ngazi ya shahada (ualimu)
 
Tatizo hili la ajira hususani kwa walimu tunalikuza sana kuliko uhalisia,kuna walimu kibao wamejazana sehemu za mijini na kwenye majiji na bado watazidi kuongezeka na gia yao siku hizi ni kuwa wanafuata huduma za matibabu mijini, wanajitengenezea ugonjwa feki.Ninao mfano mdogo wa walimu watatu wa history jijini mwanza ambao wanafundisha kidato kimoja yaani wamegawana topic!!!! NINACHOKIONA HAPA NI POOR DISTRIBUTION OF MAN POWER NA SIO UHABA hususani kwenye sekta ya elimu sijajua kwa sekta nyingine.Serikali iwahamishe walimu kutoka mijini ni wengi na wapelekwe kwenye upungufu.
Na kwenye masomo ya sayansi napo ikoje, wanagawana topic pia!? Uhaba upo kwa namna flani, watuajiri tu!
 
Kipato 300000 kwa mwezi,HESLB-15% income tax,NSSF-10%,
Bado wategemezi,n.k,

Utaweza kuishi ?
Ni kweli ni unyonge lakini usikuze mambo tofauti na uhalisia, mshahara wa laki tatu ni kuwa level gani ya elimu?!, Tusiongee pasipo uhalisia, serikali ililiona hili ndo maana watu wa Diploma veta na certificate hawapewi mkopo wa bodi
 
Back
Top Bottom