Rais Samia Suluhu umeanza kuwa Dikteta mapema kuliko hayati John Pombe Magufuli

Rais Samia Suluhu umeanza kuwa Dikteta mapema kuliko hayati John Pombe Magufuli

Chama chochote kishike dola mambo ni hayo hayo wacha Samia akupigeni spana hamtaki kumuheshimu na mnamzonga,ndio Kwanza miezi minne mnampanda kichwani
Time will tell
 
Ebu tutajie nchi moja tu duniani baada ya uchaguzi na serikali kutangazwa vyama vya siasa vinaendelea kufanya mikutano ya hadhara? Ata hiyo mikutano mkiruhusiwa mnazungumza Nini zaidi ya kueneza chuki? Mmesharuhusiwa kufanya mikutano ya ndani fanyeni matangazo na watu watakuja..magu nilikuwa simpendi lakini kwa hili nilimuunga mkono maaana haiwezekani mtu anafanya kazi wengine wanaangaika kufanya mikutano ya kuharibu....
Chadema sasa washtakiwe kwa kuhatarisha amani ya Nchi, huko Mwanza wamekamatwa tena
 
CHADEMA wamekamatwa tena huko Mwanza, na M/kiti Freeman kakamatwa tena
wangekubali kupumzika mbona kipindi cha Uchaguzi bado
mambo ya Corona hawayaoni?
kila kitu kwao ni siasa, Tozo za simu wameibuka nazo
mbona ACT wapo kimya? ulimbukeni utawaponza CDM
 
CHADEMA wamekamatwa tena huko Mwanza, na M/kiti Freeman kakamatwa tena
wangekubali kupumzika mbona kipindi cha Uchaguzi bado
mambo ya Corona hawayaoni?
kila kitu kwao ni siasa, Tozo za simu wameibuka nazo
mbona ACT wapo kimya? ulimbukeni utawaponza CDM
Yametimia
 
Bado nina imani na mama! Pengine kapotoka kidogo lakini hajaharibu kabisa. Tumpe muda zaidi naye ni binadamu si mkamilifu. KUKOSEA KUPO!
Nyota njema huonekana asubuhi. huyu mama ni hatari maana hata magufuli alitupeleka kidogo karibu mwaka ndio akaanza ubabe. Huyu anataka asubuhi asubuhi aeleweke yuko hivyo.
 
Nyota njema huonekana asubuhi. huyu mama ni hatari maana hata magufuli alitupeleka kidogo karibu mwaka ndio akaanza ubabe. Huyu anataka asubuhi asubuhi aeleweke yuko hivyo.
Ameshaeleweka amepoteza mvuto ndani ya mwezi mmoja
 
Kujadili katiba kunaivuruga vipi nchi. mbona bunge la katiba lilifanyika na nchi haikuvurugika? mbona warioba juzi alisema Katiba ni muhimu na nchi haikuvurugika. Huyu mama anogopa tu kivuli na nina wasiwasi kama hatapoteza dira siku si nyingi. Atahama kuzungumzia maendeleo na kupambana na akina Mbowe. wao ndio walioruhusu upinzani kwani hawakujua kazi ya upinzani ni kuja na wazo mbadala . kama mpinzani ataongea yale yale ya CCM basi maana yake haipo.
 
Bado nina imani na mama! Pengine kapotoka kidogo lakini hajaharibu kabisa. Tumpe muda zaidi naye ni binadamu si mkamilifu. KUKOSEA KUPO!
Leo bado una imani

Kesi ya ugaidi iyoooooo
 
Kauli ya Rais Samia kuminya uhuru wa Raia na vyama vyao vya siasa kwa kutozingatia katiba na sheria ameingia kwenye rekodi mpya kama Rais Mwanamke wa kwanza Africa kuwa Dikteta.

Siku ya 101 madarakani, Rais Samia Suluhu tayari ameanza kulewa sifa na mapambio. Ameamua kuendelea kuminya uhuru wa vyama vya siasa kufanya mihadhara kwa kutumia utashi wake na siyo katiba iliyomfanya Yeye awe Rais bila kupigwa kura za wananchi.

Hakuna uchumi bila haki na uhuru wa watu, Tangu tupate uhuru kwa miaka zaidi ya ishirini na nne ya chama kimoja hakuna Uchumi wowote uliosimama, Uchumi ulianza kusimama wakati wa vyama vingi vya kisiasa na huu ni wakati wa Hayati Ben Mkapa, Hayati Ben Mkapa alisimamia uhuru na kujenga mfumo wa kitaasisi.

Mama Samia ameanza kuonyesha sura yake halisi ya udikiteta mapema sana, Atambue na akumbuke hakuna aliyempigia kura kwenye sanduku kama Rais wa nchi bali amepata Urais kwa kufuata katiba ya nchi, Wananchi wa Tanzania ni waelewa ndio maana Mama alipoapishwa kwa kufuata katiba hakuna aliyelalamika kwenye mitandao ya kijamii, Kuanza kuvunja katiba siku ya 101 kisa umesifiwa sana Jiandae kisaikolojia kwa watu kukusema kimataifa kama mtangulizi wako na kitakachofuatwa ni wewe kuhojiwa maswali Magumu na vyombo vya kimataifa ukajikuta unadhalilika na kutafuta mchawi nani.

Chuki ambayo umejenga kwa kauli yako ya kusema hakuna vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara umeitoa kwa kutumia sheria na katiba ipi? Wewe uliapishwa kwa kufuata katiba kwanini umeanza kuharibu na kupindisha katiba ya nchi?

Kauli yako ya kuminya uhuru wa siasa imekuharibia kila kitu na sasa mjadala umeanza kuwa mkali zaidi, Jiandae Kwa watu kukusema hovyo na kukudhalilisha zaidi ya mtangulizi wako.

Kila kauli ina madhara yake, Kauli yako ya kuwa unajenga Uchumi, Hayati Magufuli alisema analeta Maendeleo. Leo hakuna anayemkumbuka Magufuli na habari zake za Maendeleo bali anakumbukwa kwa kuminya na kukandamiza haki za Raia.

Serikali iwape watu uhuru wao, Kuna tetesi zilizagaa kuwa hata wewe watu walitaka usipewe Urais kwani waliona hutaweza lakini kuna kundi likasimamia katiba na ukaapishwa kuwa Rais, Kwanini wewe unavunja katiba?

---
UPDATE tarehe 02/07/2021
Mkutano wa wanawake wa Chadema (Bawacha) uliokuwa unafanyika kwenye ukumbi mikocheni umevamiwa na polisi kwa amri toka juu, Wamefukuzwa ndani ya dakika 30

Serikali ya Samia Suluhu ni ya kidikiteta kuliko ya Magufuli, Hawajaangalia gharama za ukumbi, Polisi kwa amri toka juu wameuvuruga mkutano


Updates 17/07/2021

Sasa ni marufuku kujadili mambo ya tozo za miamala ya simu iliyokuwa ya kinyonyaji, Mama amezuia mjadala wa katiba mpya, Ukitaka kujadili katiba mikusanyiko inavamiwa na polisi kwa amri toka kwa Rais Samia

Update 21/07/2021
Mbowe na wenzake wavamiwa hotelini kwa amri toka juu, Hawajulikani walipo

Ni amri toka juu, Wakiwa wa najiandaa kujadili katiba mpya


UPDATE 22/07/2021

Mbowe abambikiwa kesi ya ugaidi na Mamlaka
Toeni ujingaa bhana..hamna mana nyie wapinzani..hamna akili..kabisaaa..hii nchi CCM wameishika pabaya..ccm n wezi kila kona..lakin ukiangalia upinzani wanaotaka kuchukua nchi ndo wajingaaaa kabisaaaa...yaan wacha CCM waiendeshee hii nchii tuu
 
Bado nina imani na mama! Pengine kapotoka kidogo lakini hajaharibu kabisa. Tumpe muda zaidi naye ni binadamu si mkamilifu. KUKOSEA KUPO!
Subirini..nakuhakikishiaaa mtamkumbuka jpm.tena ww mzee wa puree lazimaa umkumbukee mana ulimnangaaa mnooo
 
Mikutano ya kisiasa hadharani sasa hv ya kazi gani mkuu? kama sio kuleta fujo tu!

Mama yupo sahihi kbs. Amani ndo kipaumbele. Kama katiba inasema tofauti basi iangaliwe upya!

Mikutano ya kisiasa hadharani ifanywe miaka ya uchaguzi
2024- Serikali za mitaa
2025- uchaguzi mkuu
Ila sisi CCM tufanye lakini wapinzani wasifanye!??
Pia vipi Katiba inatamka ayo?
 
Mshana my brother
Hivi uhuru ni lazima kuwe na maandamano?

Au uhuru ni kulazimisha rais afanye yale ambayo vyama vya siasa yanataka ?
Kuna shida gani kama hayo maandamano yanafanyika kwa mujibu wa Sheria?.
Na kuna ubaya gani kumtaka rais aheshimu na afuate Katiba aliyoapa kuilinda?.
 
Kuna shida gani kama hayo maandamano yanafanyika kwa mujibu wa Sheria?.
Na kuna ubaya gani kumtaka rais aheshimu na afuate Katiba aliyoapa kuilinda?.

Shida ipo kubwa tu
 
Ana uwezo mdogo sana alianza kubatizwa kuwa mama wa taifa lakini kwa upumbavu wake kaamuwa kuonyesha makucha yaudictetor mapema mno harafu alivyokosa akili unaanzanaprominentfigure wachamakilichosambaa Tanzania nzima si unaeneza kazi zake bila yeye kufika maeneo husika na hata samia akiridhia Mbowe maisha yake yaondolewe anadhani yeye ataishi milele
 
Back
Top Bottom